Posts

Showing posts from January, 2025

WAZIRI NDEJEMBI AKUTANA NA WAMILIKI WA SHAMBA LA KWASHEMSHI LA KOROGWE

Image
  WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi amekutana na kufanya kikao cha pamoja na Wamiliki wa Shamba la Sisal Estate “Kwashemshi” lililopo Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga kwa lengo la kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa muda mrefu baina ya wananchi wa eneo hilo na wamiliki hao. Kikao hicho kimefanyika Januari 03, 2025  Ofisi za Makao Makuu ya Wizara zilozopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma. Kikao hicho kimehudhuriwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Netho Ndilito, Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Mhe. Timotheo Mzava, Mkurugenzi wa Halmashauri ua Wilaya ya Korogwe Goodluck Mwangomango, Viongozi wa Sisal Estate wakiongozwa na Wakili Ndurumah Magembe na Mathew Kashindye pamoja na wajumbe wa Mejimenti na wataalamu wa wizara.

WAZIRI CHUMI APONGEZA JUHUDI ZA UPANDAJI MITI NA UHIFADHI MISITU ZINAZOFANYWA NA TFS

Image
Mbunge wa Jimbo la Mafinga na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Cosato Chumi (Mb) ametembelea TFS-Shamba la Miti Sao Hill ili kuona namna shughuli za upandaji miti na uhifadhi wa misitu zinazofanywa na Shamba leo Januari 03, 2025. Waziri Chumi ameipongeza TFS kupitia Shamba la Miti Sao Hill kwani imekuwa na mchango mkubwa kiuchumi kwa wakazi wanaolizunguka shamba kwani limekuwa likichangia uendelezaji wa miradi mingi ya maendeleo hususani katika Wilaya ya Mufindi na Taifa kwa ujumla. Aidha amesema kuwa Shamba la Miti Sao Hill limekuwa msingi mkubwa wa uzalishaji wa malighafi za viwanda hali iliyochangia kukua na kuongezeka kwa uwekezaji wa viwanda vya mazao ya misitu katika Wilaya ya Mufindi. Pamoja na hayo amewataka wahifadhi kuendelea kutoa elimu ya uhifadhi kwa wananchi wanaolizunguka shamba ili kuendeleza uhusiano mzuri iliopo baina ya Shamba na wananchi pamoja  na kuongeza jitihada za ulinzi wa rasilimali misitu dhidi ya majanga ya moto yanay...

JKCI imefungua tawi jipya katika jengo la Oyster Plaza

Image
  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imefungua tawi jipya kuwapa wananchi nafasi kuwa karibu na huduma ili pale wanapopata changamoto za kiafya wasichukue muda mrefu kufuata huduma zilipo. Tawi hilo lililopo katika jengo la Oyster Plaza Haile Salassie barabara ya Ali Bin Said limeanza kutoa huduma bobezi za moyo leo lengo likiwa kuwapa fursa wananchi kupata huduma katika maeneo tofauti na ilipo taasisi hiyo na kupunguza msongamano uliopo katika makao makuu ya taasisi Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alisema JKCI imekuwa ikiwafikia wananchi walipo kwa kuwafuata mikoani na kuwapa huduma bobezi za uchunguzi na matibabu ya moyo. “Tumekuwa tukiwafuata wananchi mikoani kuwapa huduma sasa tumeamua kuanzisha matawi ya Taasisi, hii pia ni sehemu ya kuwafuata wananchi mahali walipo kwani hapa tulipo leo tunawapa nafasi wananchi wa eneo hili kupata huduma kwa karibu la...

WAZIRI KOMBO AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA MAHAKAMA YA WILAYA YA MAGHARIBI B

Image
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amesema kuimarika kwa miundombinu ya Mahakama ni hatua muhimu itakayowawezesha wananchi kupata huduma katika mazingira mazuri, salama na rafiki. Ameyasema hayo leo Januari 1, 2025 wakati akiweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Jengo la Mahakama ya Wilaya ya Magharibi B huko Kisakasaka, Zanzibar. Balozi Kombo amesema, kwa miaka mingi mahakama zimekuwa na changamoto ya miundombinu ya majengo na Serikali inayoongozwa na Dkt. Hussein Ali Mwinyi imedhamiria kumaliza changamoto hizo kwa kujenga majengo mapya na ya kisasa. "Kwa mfano jengo lililokuwa likitumiwa na Mahakama ya Magharibi B pale Mwanakwerekwe lilikuwa finyu mno kiasi cha kusababisha msongamano mkubwa na kuwapa usumbufu waliofuata huduma mahali pale," alisema Mhe. Kombo. Waziri huyo ameongeza kuwa, pamoja na ufinyu huo, pia halikuwa rafiki kutokana na kukosekana nafasi kwa ajili ya maofisa wa Mahakama. Vilevile, kukosekana kwa ...

DC MALINYI:ZOEZI LA KULIPA FIDIA WANANCHI NGOMBO LINAKWENDA VIZURI

Image
  Na Beatus Maganja, Malinyi Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Sebastian Waryuba amesema zoezi la kuwalipa fidia wananchi wa Kijiji cha Ngombo kilichopo ndani ya Pori la Akiba Kilombero Mkoani Morogoro linaendelea vizuri ambapo asilimia 93 ya wananchi wote tayari wamekwishalipwa fidia zao kwa ajili ya kupisha shughuli za uhifadhi katika Hifadhi hiyo na asilimia 7 ya wananchi waliosalia wanaendelea kushughulikiwa ili kukamilisha malipo yao. Akizungumzia zoezi hilo jana Desemba 31, 2024 wilayani humo Mhe. Sebastian amesema Serikali imetoa zaidi ya shilingi billioni 6.9 kulipa wananchi 1,056 ili waweze kuhama kwa hiari kutoka maeneo ya Hifadhi huku akitoa maelekezo kwa watendaji wa vijiji 32 wilayani Malinyi kuwapokea ili waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku. “Kwanza si kweli kwamba wananchi wa Ngombo hatujawaambia mahali pakwenda. Katika barua yangu ya tarehe 4 Disemba, 2024 niliyowaandikia watendaji wa vijiji 32 vilivyo ndani ya wilaya ya Malinyi, nilitoa maeleke...

NMB yadhamini kombe la Mapinduzi 2025, yafadhili Siku ya Mazoezi Kitaifa Z'bar

Image
  BENKI ya NMB, imetangaza udhamini wa Sh. Milioni 50 wa michuano ya Kombe la Mapinduzi ya Zanzibar (Mapinduzi Cup 2025), inayotarajia kuanza Januari 03, 2025 kwenye Uwanja wa Gombani visiwani Pemba, ambayo itashirikisha timu za Taifa, badala ya klabu za Tanzania Bara na Zanzibar kama ilivyozoeleka Sambamba na udhamini huo, NMB pia imekabidhi 'tracksuit' 100 zenye thamani ya Sh. Mil. 9 za kuvaa viongozi wa Serikali ya Zanzibar katika Siku ya Kitaifa ya Mazoezi (Januari 1, 2025), ambayo ni sehemu ya Shamrashamra za Miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ambayo inafanyika chini ya kaulimbiu: 'Amani, Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo Yetu - Mapinduzi Daima.' Hafla ya makabidhiano ya hundi ya udhamini na 'tracksuit' hizo, imefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar, ambako Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Zanzibar, Ahmed Jumaa Nassor, alimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi. Fatma Hamad Rajabu, m...

WHO Yaitaka China Kueleza Chanzo Cha Uvico 19

Image
  Mkurugenzi Mkuu wao Dkt.Tedros Adhanom Ghebreyesus Shirika la Afya Ulimwenguni – WHO bado linasubiri ushirikiano kamili kutoka kwa serikali ya China ili kufafanua chanzo cha janga la UVIKO-19 pia katika salamu zake za mwaka mpya akisisitiza amani duniani. Hii ni miaka mitano baada ya visa vya kwanza vya ugonjwa mpya wa mapafu (Uvico 19) kuripotiwa katika mji wa China wa Wuhan. WHO imesema jijini Geneva kuwa hilo ni sharti la kimaadili na kisanyasi. Shirika hilo la Afya Ulimwenguni linaloongozwa na Mkurugenzi Mkuu wao Dkt.Tedros Adhanom Ghebreyesus (pichani)  limeitaka China kutoa data zote ili wanasayansi waelewe chimbuko la janga hilo lililotikisa dunia na kusababisha vifo vya maelfu ya watu. Taarifa ya WHO imesema kuwa bila uwazi na ushirikiano miongoni mwa nchi tofauti, dunia haiwezi kuzuia na kujiandaa vya kutosha kwa magonjwa ya milipuko na majanga ya siku za usoni. Wakati huo huo Dkt.Tedros Adhanom Ghebreyesus ametoa wito kwa ...

Uhamiaji Yatakiwa Kuimarisha Udhibiti Wa Wahamiaji Haramu

Image
  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani Dkt. Tulia Akson Idara ya Uhamiaji nchini imetakiwa kuimarisha udhibiti wa Wahamiaji haramu na baadhi ya wageni wanaoingia na kufanya biashara haramu huku wakiwa na lengo lililojificha la kuvunja amani yetu kukamatwa na kuwachukulia hatua kali za kisheria pindi wanapobainika Hayo yamesemwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani Dkt. Tulia Akson katika hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la Jengo la Afisi za Uhamiaji Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja Desemba 29, 2024 Dkt.Tulia amesema usafirishaji haramu wa binadamu umekuwa ukipigwa vita duniani na hapa nchini hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kuendelea kupambana nalo ili kuweza kulitokomeza kabisa. “Kwa kusema hayo ndugu zangu hatua tumepiga ni kweli lakini tunataka hatua ipigwe zaidi hasa katika hili eneo la Uhamiaji kwanini kwasababu wako wale watu huwa wanaitwa wahamiaji haramu tunataman...

Nafasi Za Kazi 24 Taasisi Mbalimbali Za Umma, Mwisho wa kutuma Januari 2, 2025

Image
Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Kituo cha Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Kituo cha Tiba cha Bugando (BMC), Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI), The Public Service Recruitment Sekretarieti (PSRS), inawaalika Watanzania mahiri na wenye sifa stahiki kujaza ishirini na nafasi nne (24) zilizoachwa wazi zilizotajwa hapa chini. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 02 Januari, 2025; FUNGUA HAPA >>> NAFASI ZA KAZI 24 TAASISI MBALIMBALI ZA UMMA

MAHAKAMA YAMUACHIA HURU ALEX MSAMA

Image
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni Kinondoni imemuachia huru Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha mashtaka ya kughushi nyaraka za kiwanja dhidi yake. Katika kesi hiyo ya jinai namba 275 ya mwaka 2022 imetolewa hukumu leo na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Isihaka Kupwa ambapo Msama alikuwa anakabaliwa na mashtaka matano. Hakimu Kupwa alisema mahakama hiyo ilipokea na kupitia vielelezo na ushahidi wa pande zote mbili pasina kuacha. Hakimu Kupwa amesema baada ya mahakama hiyo kupitia ushahidi wa pande zote mbili, imeona upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake hivyo inamuachia huru na kumpa ushindi. Miongoni kwa sababu alizozitaja Hakimu Kupwa ni kwamba Jamhuri ilishindwa hata kuwasilisha cheti cha kifo cha marehemu aliyetajwa katika kesi hiyo, pia kukosekana kwa mtaalamu wa kuthibitisha maandishi yaliyoghushiwa. “Mahakama hii inamuachia huru Alex Msama Mwita, haki ya kukata rufaa ipo wazi,”. Miongoni mwa mash...

DKT. SAMIA AMEIHESHIMISHA TANZANIA MATUMIZI YA NISHATI SAFI-MAJALIWA

Image
  -Asema Watanzania tunapaswa kumuunga mkono WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameiheshimisha Tanzania katika hamasa ya matumizi ya nishati safi ya kupikia kutokana na umuhimu wake kwenye afya ya binadamu na utunzaji wa mazingira. Amesema kuwa kutokana na jitihada hizo, mashirika ya kimataifa yameonesha nia ya kumuunga mkono ikiwemo kufanya mkutano mkubwa wa nishati safi Afrika hapa nchini. “Watanzania tumuunge mkono Rais Dkt. Samia katika kampeni hii na kuhakikisha tunaongoza kwenye matumizi ya nishati safi barani Afrika” Amesema hayo leo (Jumanne, Desemba 31, 2024) wakati wa Tamasha la Azimio la Kizimkazi ambalo lilienda sambamba na ugawaji wa majiko 1000 ya gesi kupitia kampeni ya matumizi ya nishati safi ya kupikia. Tukio hilo limefanyika katika eneo la Kilimahewa Majumbakumi, Ruangwa mkoani Lindi. “Tunapaswa kumuunga mkono kwasababu agenda imeanzishwa na Rais wetu, dunia lazima iitambue Tanzania kama ambavyo imetambua na kule...

SALAMU ZA MWAKA MPYA ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, KWA WATANZANIA

Image
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akilihutubia Taifa wakati akitoa Salaam za kuaga Mwaka 2024 na kuukaribisha Mwaka mpya wa 2025 Ikulu ndogo Tunguu Zanzibar tarehe 31 Desemba, 2024.  Ndugu Wananchi; Leo, tarehe 31 Disemba, tunauhitimisha mwaka 2024 na kuukaribisha mwaka 2025. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu, kwa neema ya uhai na afya njema. Wapo wenzetu wenye changamoto za kiafya, ambao tunaendelea kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awajaalie afya njema ili warudi kwenye shughuli zao za kujenga Taifa. Kuna ndugu na jamaa zetu ambao tungetamani kuwa nao leo hii, lakini kwa mapenzi yake Mola, haikuwezekana. Tuendelee kuwaombea mapumziko mema peponi. Amen Ndugu Wananchi; Mwaka 2024 ulikuwa mwaka wa kihistoria, wenye mafanikio na unaotupa matumaini zaidi tunapoitazama kesho ya Taifa letu. Katika jitihada za kutekeleza majukumu yangu, nilipata fursa ya kufanya ziara katika baadhi ya Mikoa, na kote nilikopita nimejione...