ZOEZI LA KUHAMA KWA HIARI LIPO PALEPALE - WAZIRI CHANA

 



Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) amesisitiza kuwa zoezi la kuhama kwa hiari kwa wananchi wa Ngorongoro linaendelea huku akisisitiza kwamba Serikali inafanya maboresho mbalimbali ili kurahisisha zoezi hilo.

Ameyasema hayo Septemba 12, 2024 alipokuwa akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro katika Makao Makuu ya Ofisi za NCAA Wilayani Karatu Mkoani Arusha.

"Niseme tu kwamba zoezi la kuhama kwa hiari linaendelea  na maboresho yanaendelea na kuna maeneo ya Kitwai, Kilindi na sehemu nyingine ambazo watu wanapenda kwenda wanaenda kwa hiari " amesisitiza Mhe. Chana.

Amewataka Askari Uhifadhi kusimamia vyema zoezi hilo ili kurahisisha utekelezaji wake.Aidha, amewataka kuendelea kufuata  maelekezo mbalimbali ya Serikali ikiwa ni pamoja na kuboresha utoaji wa huduma za kijamii kwa wananchi kama geti na vyoo vya wanafunzi.

Comments