Monday, September 09, 2024

VODACOM TANZANIA YATANGAZA WASHINDI WA DROO YA SITA YA KAMPENI YA NI BALAA!

 

Mkuu wa Kanda ya Kati wa Vodacom Tanzania Plc, Joseph Sayi (Kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 20 kwa mshindi wa mwezi wa kampeni ya Ni Balaa! Amina Gwila mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha Tawi la Dodoma mwishoni mwa wiki katika hafla iliyofanyika duka la Vodacom jijini Dodoma. Amina amepata nafasi ya kuchagua shule ambayo Vodacom watasaidia kukarabati maktaba yake ili kukamilisha adhma ya kusaidiana na Serikali katika kuboresha elimu nchini.
Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania Plc Mkoa wa Dodoma, Balikulije Mchome (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi 500,000/- mshindi wa droo ya sita wa kampeni ya Ni Balaa! Kila mtu ni mshindi, bw. Peter Sheka katika duka la Vodacom lililopo jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. Endelea miamala kupitia M-pesa nawe uwe mshindi.
Afisa wa M-Pesa kutoka Vodacom Tanzania Plc, Mkoa wa Dodoma, Musa Kushoka (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi 500,000/- kwa mshindi wa droo ya sita ya kampeni ya Ni Balaa! Kila mtu ni mshindi, bw. Felician Mgimba (Kulia) katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi iliyofanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. Endelea kufanya miamala na kununua vifurushi ili uweze kuibuka mshindi.
Afisa Mauzo wa Vodacom Tanzania Plc mkoa wa Dodoma, Athumani Ngoma (kushoto) akimkabidhi mshindi wa wiki ya sita wa kampeni ya Ni Balaa! Kila mtu ni mshindi, Angel Bahingali (Kulia) mfano wa hundi ya shilingi 500,000/- katika duka la Vodacom lililopo jijini Dodoma mwishoni mwa mwiki Endelea kufanya miamala na kununua vifurushi kupitia M-pesa ili uweze kuibuka mshindi.

No comments:

WAZIRI NA NAIBU WAZIRI WA ARDHI WASHIRIKI KIKAO CHA KWANZA CHA MKUTANO WA 19 WA BUNGE LA 12 KWA AJILI YA KUJADILI BAJETI YA SERIKALI 2025/2026

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi (MB), leo tarehe 8 Aprili 2025, ameshiriki kikao cha kwanza cha Mku...