Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amewasili Songea

 

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro tayari amewasili katika Ukumbi wa Chandamali Songea kwa ajili ya Mdahalo wa Kitaifa wa Maadili leo Septemba 14, 2024, ikiwa ni kuelekea Tamasha la tatu la Utamaduni la Kitaifa kuanzia Septemba 20 hadi 23, 2024 Uwanja wa Majimaji Songea.
Mhe. Waziri akiwa ameambatana na baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Ruvuma amepokelewa na  baadhi Viongozi wa Wizara na Taasisi zake.

Mdahalo huo utahusisha mada mbalimbali  zitakazojadiliwa, makundi ya wazee, vijana pamoja na wanachuo.











Comments