Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi ameagiza ujenzi wa Jengo la Paradise Commercial Complex ukamilike mapema kabla ya mwezi Novemba ili liweze kufunguliwa kwa matumizi ya ofisi na biashara mapema Desemba mwaka huu. Pia amesifu Shirika la Nyumba la Taifa kwa ujenzi wa jengo hilo kubwa na zuri la aina yake mkoani Katavi.
Comments