Wednesday, May 16, 2007

Jengo hili la walimu wasio na hadhi, inachekesha

KAMA kuna kitu ambacho pengine kimenipa faraja, lakini wakati huo huo kunipatia simanzi, basi ni lile jengo linaloitwa Mwalimu House, likibeba maana ya ‘Nyumba’ au ‘Jumba’ la mwalimu, ambalo lilizinduliwa wiki chache zilizopita.

Jengo hili la Mwalimu lilizinduliwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete, ni la kisasa na lenye kila kitu na hadhi kubwa, lakini bahati mbaya wamiliki wake wenyewe ni watu hohehahe, taabani, wanaoishi kwa taabu na shaka na yote inatokana na fani hiyo kukosa mwelekeo.

Matokeo yake, faini hiyo imepoteza heshima, haiheshimiki tena na hivyo kufanya kila anayehitimu chuo au elimu ya juu kufikiria mara mbili kabla ya kuichagua.

Sina budi kuanza kwa kuweka wazi kwamba kamwe siwaonei wivu wale wanaofaidi mavuno yaliyopandwa katika ghorofa hilo na wala lengo si kuwashambulia, wala sina nia mbaya na yeyote yue, bali ni kujaribu kufikiri kwa kina. Hivi, najiuliza, kwanini hali ya mwalimu inabakia kuwa hivi hadi leo.

Mmejenga jengo zuri, safi! Mnazungumzia matatizo yao, sawa. Lakini, kwanini hamsimamii haki za walimu hao wanaoishi kwa shida! Bonyeza hapa

No comments: