Thursday, April 12, 2007

Baadhi ya Wanafunzi wa shule ya msingi ya Kibogwa, tarafa ya matombo mkoani Morogoro wakiwa darasani. Mazingira duni ya kusomea kama haya, yatasababisha taifa kushindwa kutimia kwa malengo ya usawa katika elimu. Picha hii ni kwa hisani ya ndugu yangu Mathew Kwembe.

3 comments:

mloyi said...

Ndiyo elimu yetu hiyo!
Sijui mtoto anawezaje kukaa siku yote ya masoma vile na akawamakini darasani? siwezi kuelewa!
Sijui sisi wazazi tuna akili gani? tunawachukuliaje hawa watoto wetu? watu wa hali ya chini kuliko sisi wenyewe? sababu hawawezi kulalamuka kwa "sauti" na sisi pia tunaacha kuwaonea huruma kwa "matendo"?
Labda babu zetu hawakutuachia maarifa ya kujitengenezea viti na meza kwa kutumia miti, nasisi pia tunashindwa kuwatengenezea hawa watoto meza na viti!
Turejee tunachoongea kila siku, alianza ndesanjo(Nestory McChair) kulilia wazungu warudi ikulu yetu ya magogoni, watu hawakumuelewa anachosema, wanasahau elimu ya kujitegemea iliyokuwa ni dhaambi kubwa kutoshiriki siku zetu za shule ya msingi, sasa tunahimizwa kupambana na utandawazi kwa kutumia maliasili zetu wenyewe lakini bado tunangojea vitu na meza vilivyotengenezwa kwa kutunia "uchafu" vitoke kwa wale jamaa zetu "waliotuzidi maarifa".
Kijiji chenye shule kama hii ni aibu kwa taifa na mababu zao waliowatangulia.
Tutafute muda tutulie na kuzisoma akili zetu zisizidi kutupotosha.

mzee wa mshitu said...

Eee bwana ndiyo hii ndiyo nimekubalihoja zako ni valid kabisa. Hivi hawa watoto tukiwaacha wapate elimu katika mazingira haya tunatarajia nini? Wakati kuna watu huko wanajisifu kuwa wamejenga madarasa eti ya maana je huku hawajafika au huku hakuna uongoz?i

Anonymous said...

Peleka hiyo picha ya kwenye blog ya Michuzi itapata watu wa kuisaidia nina uhakika maana blogu ile inasomwa na wengi ndani na nje ya nchi.