Thursday, April 26, 2007

Muungano oyeeeee!!!

Katika hali ya kawaida na hasa kwa vijitaifa vyetu hivi vichanga vya dunia ya tatu ni nadra sana kwa waheshimiwa walioshika mipini ya visu kama hawa kukaa na kucheka hivi, hebu mtizame Maalima Seif, Lipumba na kisha mzee mkali na kina Saleh Pamba walivyokenua meno, hapa ni katika sherehe za sikukuu ya muungano. Picha ya Deus Mhagale.

Thursday, April 19, 2007

Nini kisa cha kutumia fedha nyingi kujadili ubadhirifu?

POTELEA mbali, wakati mwingine ukweli inabidi uzungumzwe na hata kama unauma kiasi gani. Si bora hata kidogo kukaa kimya na kuchekacheka wakati mambo tukiyaona hayaendi sawa.

Hayaendi sawa sababu, kadiri siku zinavyoenda tunayaona yanajirundika, yanaongezeka, na kisha yanakuwa kama vile mazoea. Yanakuwa kama mambo ya kawaida kabisa kufanywa na wakuu wetu hawa wa nchi.

Tunawaheshimu sana na wakati mwingine tunawaonea huruma, kwa namna ambavyo wanakabiliana na maamuzi magumu kupita kiasi na mengine yanayokuwa yanazidi uwezo wa kibinadamu. Katika hayo tuko pamoja nao.

Lakini jamani hebu tufikirie, hivi wale wazazi wetu waliopo kule Nanyamba au Nachunyu au Nakasahenge na kwingineko wanavyotaabika ili kuhakikisha wanaendelea kuwapo katika dunia hii, wanaposikia haya yanayofanyika sasa wanajisikiaje! Bonyeza hapa

Monday, April 16, 2007

Miss Universe Tanzania


Miss Universe Tanzania, Flaviana Francis Matata, katika pozi baada ya kuvishwa taji hilo juzi kwenye Hoteli ya Movenpick Dar es Salaam. Hongera kwa ushindi huu mdogo wangu.

Thursday, April 12, 2007

Shule

Shule yetu nzuri.
Baadhi ya Wanafunzi wa shule ya msingi ya Kibogwa, tarafa ya matombo mkoani Morogoro wakiwa darasani. Mazingira duni ya kusomea kama haya, yatasababisha taifa kushindwa kutimia kwa malengo ya usawa katika elimu. Picha hii ni kwa hisani ya ndugu yangu Mathew Kwembe.

Wednesday, April 11, 2007

Soko jipya la Mchikichini

Sokoni Mchikichini mambo sasa shwari ni kwa wale wafanyabiashara waliohamishwa Mitaa ya Kongo,Swahili, Aggrey na kadhalika.

Saturday, April 07, 2007

Mnazi mmoja uko wapi vile

Mnazi Mmoja

Dar es Salaam: Jiji Kuu la Biashara na Utalii Tanzania

Dar es Salaam ni jiji kubwa na kitovu cha biashara cha Tanzania, likiwa na mchanganyiko wa tamaduni, fursa za kiuchumi, na vivutio vya utalii. Likiwa kwenye pwani ya Bahari ya Hindi, jiji hili lina historia ndefu kama bandari muhimu kwa biashara ya ndani na nje ya nchi.

Jiografia na Hali ya Hewa

Dar es Salaam ina mandhari ya kuvutia, ikiwa na fukwe safi kama Coco Beach na Kigamboni Beach. Hali ya hewa ni ya joto mwaka mzima, huku jiji likipata vipindi vya mvua hasa kati ya Machi-Mei na Oktoba-Desemba.

Maeneo Muhimu na Vivutio

  • Posta na Kariakoo: Eneo la biashara lenye maduka, masoko na huduma mbalimbali.
  • Masaki na Oysterbay: Maeneo ya kifahari yenye hoteli, migahawa na maisha ya usiku.
  • Makumbusho ya Taifa: Hifadhi ya historia ya Tanzania na tamaduni zake.
  • Mji wa Kale (Old Boma): Jengo la kihistoria lililojengwa wakati wa ukoloni wa Wajerumani.

Usafiri na Miundombinu

Jiji lina mfumo wa mabasi ya mwendokasi (DART), boda boda, bajaji, na huduma za usafiri wa majini kuelekea Kigamboni na Zanzibar. Dar es Salaam pia ina Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, unaounganisha jiji na mataifa mengine.

Fursa za Kibiashara na Maendeleo

Dar es Salaam ni kitovu cha uchumi wa Tanzania, ikiwa na makampuni makubwa, taasisi za kifedha, viwanda

Friday, April 06, 2007

Mbadala wa RVF



Kutokana na ongezeko la ugongwa wa homa ya bonde la ufa hivi sasa kuku ay vyuku vinalika ile mbaya, hapa lori lililojaa vyuku likiingia mjini. Picha ya Fredrick Felix.

*WATAFITI WA MIMEA VAMIZI WATUA SERENGETI

Na Sixmund Begashe - Serengeti  Ziara ya kikazi ya watafiti wa mimea vamizi kutoka Jamhuri ya Cuba walioungana na wataalam wa ikolojia kutok...