Saturday, March 22, 2025

TUWAPENDE, TUWAJALI NA TUWATUNZE WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM - MAJALIWA







Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa wanafunzi wa shule zote nchini kuwatunza, kuwapenda na kuwajali wanafunzi wenzao wenye mahitaji maalum ili nao waweze kutimiza ndoto zao.

Amesema Serikali imejenga miundombinu bora ambayo sasa inawawezesha wanafunzi wenye mahitaji maalum kusoma na kufaulu na kupata nafasi katika shule mchanganyiko na hivyo ni wajibu wa wanafunzi wengine kuwapenda na kuwasaidia.

"Nimevutiwa namna mnavyowajali na kuwapenda wanafunzi wenzenu wenye mahitaji maalum, ninaomba muendelee na upendo huo muwathamini na kuwapenda ili nao watimize ndoto zao".

Ameyasema hayo leo, (Jumamosi Machi 22, 2025 ) alipotembelea Shule ya Sekondari ya Mkoa ya Wasichana ya Njombe iliyoko Wilaya ya Wanging'ombe Mkoani Njombe.

Mheshimiwa Majaliwa amesema pamoja na mambo mengine ameridhishwa na ujenzi na mandhari ya shule hiyo na zaidi amevutiwa na mifumo ya TEHAMA iliyoko katika shule hiyo.

"Nimevutiwa na mindombinu ya TEHAMA iliyopo katika shule hii, wanafunzi mhakikishe mnaitunza  ili iwe na tija na kutimiza malengo yenu ya kujisomea."

Amesema Serikali ya awamu ya sita imefanya uwekezaji mkubwa katika shule za wasichana kwa kujenga shule kubwa zenye viwango mikoa yote nchini ikiwa ni maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

"Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amefanya uwekezaji mkubwa sana katika sekta ya elimu na hakika sasa tunaona matunda ya uwekezaji huo."

Naye, Naibu Waziri OR-TAMISEMI, na Mbunge wa Jimbo la Wanging'ombe Festo Dugange, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha upatikanaji wa shule hiyo sambamba na miradi mingine mingi ya maendeleo ikiwemo vituo vya afya, huduma za maji na miundombinu ya barabara.

Shule hiyo imegharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 4  ina vyumba vya madarasa 22, mabweni 9, bwalo na jiko pamoja na miundombinu mingineyo tayari imedahili wanafunzi 460 wa michepuo mbalimbali ya masomo.

BALOZI DKT. NCHIMBI AMLILIA BI. DAMARIS HAWASSI





Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ameungana na waombolezaji katika msiba wa Bi. Damaris Simeon Hawassi, mwenza wa Dkt. Frank Haule Hawassi, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Idara ya Uchumi na Fedha.

Balozi Nchimbi alifika nyumbani kwa marehemu, eneo la Mihuji, Dodoma, leo Jumamosi, Machi 22, 2025, ambapo alitia saini kitabu cha maombolezo na kumfariji Dkt. Hawassi na familia yake.

Mbali na hilo, akiwa pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Chama na Serikali, wa sasa na wastaafu, Balozi Nchimbi alitoa heshima za mwisho kwa marehemu, akitoa pole kwa familia na ndugu walioguswa na msiba huu mzito.

CCM inaendelea kuwa bega kwa bega na familia ya Dkt. Hawassi katika kipindi hiki kigumu, ikiwapa faraja na mshikamano wa dhati.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. 🙏🏽🕊️

#CCM #BaloziNchimbi #Maombolezo #MunguAilazeRohoYaMarehemuMahaliPema

Thursday, March 20, 2025

WIZARA YA MADINI KUANZA UTOAJI HUDUMA NDANI YA JENGO JIPYA KUANZIA MEI 15

 










* Kamati ya Bunge Yasema ina matumaini Makubwa na Hatua iliyofikiwa, Wapongeza Serikali kutoa fedha


* Ujenzi Wafikia Asilimia 92.8


📍 Dodoma

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde ameiambia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na  Madini kwamba, ifikapo Mei 15, 2025, Huduma zote za Wizara Makao Makuu, zitaanza kutolewa katika Jengo Jipya la Wizara Mji wa Serikali- Mtumba baada ya michakato yote kukamilishwa.

Amesema hayo leo Machi 20, 2025, wakati wa ziara ya Kamati hiyo ilipotembelea kukagua maendeleo ya mradi huo ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 92.8, huku kazi chache zilizobaki zikihusisha ukamilishaji wa masuala ya mifumo ya TEHAMA, zimamoto, rangi na samani za ndani ambapo tayari Wizara imekwisha kutangaza zabuni ya samani hizo.

‘’Mhe. Mwenyekiti, kukamilika kwa jengo hili kutaiwezesha Wizara kuwahudumia watanzania na wageni kutokea eneo moja na hivyo  kutoa huduma kwa urahisi kuliko ilivyo sasa ambapo baadhi ya watumishi wako kwenye maeneo mengine ikiwemo katika eneo la ilipo Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na hapa Mtumba,’’ amesema Mhe. Mavunde.

Ametumia fursa hiyo kuishukuru Serikali kwa kwa kuweka nguvu ili kukamilisha mradi wa Mji wa Serikali na kuweza kutoa kiasi cha shilingi bilioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa mji huo na kueleza kuwa, uwepo wa mji huo utasaidia kurahisisha utoaji huduma kwa Serikali na kuongeza kwamba, umeongeza mwonekano  mzuri  wa mji  wa Dodoma huku akitolea mfano wa Nchi ya Malaysia kuwa na mfumo kama Mtumba.

Naye, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Dkt. David Mathayo amesema kwamba Kamati hiyo ina matumiani makubwa kutokana na hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa jengo hilo na hivyo kutoa pongezi kwa Serikali kwa kutoa fedha kukamilisha majengo yaliyopo katika mji huo na kusema kwamba  uwepo wa Wizara zote katika mji huo utarahisisha utoaji huduma kwa wawekezaji na watanzania  kama ilivyo kwa nchi ya Brazil.

Katika hatua nyingine, Mhe. Dkt. Mathayo ameumwagia sifa uongozi wa Wizara ya Madini kutokana na namna wanavyosimamia shughuli za Sekta ya Madini na kueleza kuwa, kitendo hicho kinatoa ahueni kwa kamati hiyo ambayo inasimamia Wizara za Madini na Nishati.

‘’Tunawafahamu namna mnavyochapa kazi, kamati yetu tuna furahi tuna viongozi walionyooka, ni viongozi, wazoefu na wachapakazi. Hatuna shaka kama kamati tunafurahi kwasaabu mnaisimamia wizara vizuri,’’ amesema Dkt. Mathayo.

Awali, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Madini, Festus Mbwilo akisoma taarifa ya maendeleo ya mradi, ameieleza kamati kuwa Wizara imeendelea kusimamia kwa karibuni utekelezaji wa mradi huo ulioanzamwaka 2021 ili ukamilike kwa wakati ikiwemo kuchukua hatua za kukabiliana na changamoto zinazojitokeza

Mkandarasi wa jengo la Wizara ya Madini ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na linajengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 22.8 na Mshauri Elekezi ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA



MAJALIWA: HAKIKISHENI BIDHAA ZINAZOZALISHWA NCHINI ZINAKIDHI VIWANGO








WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameziagiza taasisi za kudhibiti viwango nchini zihakikishe uzalishaji wa bidhaa  zote zinazozalishwa zikiwemo za afya zinakidhi ubora unaotakiwa na kuweza kushindana katika masoko ya kimataifa.

Ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Machi 20, 2025) baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa mitambo ya kuzalisha oksijeni kwa matumizi ya hospitali, ambapo amesisitiza kuwa soko linatakiwa liwe na bidhaa salama, bora, na zinazokubalika kimataifa. Mitambo hiyo inajengwa katika ofisi za TOL Gases, Temeke Dar es Salaam.

Amesema mradi huo utakapokamilika utazalisha lita milioni 4.1 za oksijeni ya matibabu kwa mwaka kuanzia mwaka 2026. “Hatua hii itaboresha upatikanaji wa oksijeni katika hospitali na vituo vya afya, pamoja na kupunguza gharama za oksijeni ya matibabu kwa asilimia 35 katika hospitali na vituo vya afya kote nchini, hivyo kuimarisha huduma za afya kwa wananchi”.

Aidha, Waziri Mkuu amesema mradi huu unaunga mkono juhudi endelevu za Serikali za kuhakikisha oksijeni kwa ajili ya matibabu inapatikana kwa urahisi katika kila kituo cha huduma za afya nchini. 

“Mradi huu utaongeza upatikanaji wa oksijeni katika hospitali na zahanati nchini na kupunguza vifo vitokanavyo na magonjwa ya kupumua ikiwa ni pamoja na kupunguza vifo vya akina mama na kuokoa ya watoto wa Taifa hili.”

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godfrey Mollel amesema mradi huo ni muhimu kwa sababu oksijeni inayozalishwa kwa njia hiyo inakuwa na viwango vya ubora, hivyo itasaidia kuimarisha huduma za afya zitolewazo nchini pamoja na kupunguza vifo.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa TOL Gases, Daniel Warungu ametumia fursa hiyo kuipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kujidhatiti katika kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa Watanzania.

Amesema kampuni ya TOL inajivunia kushirikiana na Serikali katika miradi mbalimbali ya kuboresha huduma za afya, hususani upatikanaji na usambazaji wa gesi ya oksijeni kwa ajili ya matibabu ukiwemo mradi wa shilingi bilioni 9.8 wa ufungaji wa mifumo ya usambazaji gesi wodini katika vituo 129 vya huduma za afya nchini kote

MHE. RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA MJUMBE MAALUM WA RAIS WA MISRI






Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na kufanya mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Rais wa Misri, Mhe. Badr Abdelatty, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje, Uhamiaji na Wamisri Waishio Nje wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, tarehe 20 Machi 2025, katika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar.

Mazungumzo haya yamejikita katika kuimarisha uhusiano wa kihistoria na ushirikiano wa kimkakati kati ya Tanzania na Misri, hususan katika nyanja za biashara, uwekezaji, nishati, kilimo, miundombinu, na maendeleo ya sekta ya maji.

🌍 Ushirikiano wa Kidiplomasia na Kimaendeleo
Mkutano huu umeendeleza dhamira ya Mataifa haya mawili kushirikiana kwa karibu katika kukuza uchumi, kuimarisha amani na usalama wa kikanda, pamoja na kuhamasisha maendeleo endelevu kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania na Misri.

Mhe. Badr Abdelatty ameeleza dhamira ya Serikali ya Misri kuendelea kuwekeza Tanzania na kushirikiana katika miradi mbalimbali inayolenga kuinua sekta za kimkakati, hususan kupitia uwekezaji wa moja kwa moja (FDI), ushirikiano wa kiufundi, na mipango ya maendeleo ya pamoja.

Kwa upande wake, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amepongeza ushirikiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na Misri na kueleza kuwa Serikali yake itaendelea kuimarisha mazingira rafiki kwa uwekezaji na biashara baina ya mataifa haya mawili.

🤝 Tanzania na Misri Zinaimarisha Uhusiano wa Kihistoria!
Mazungumzo haya yameongeza msukumo mpya katika ajenda za maendeleo kati ya Tanzania na Misri, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha mataifa haya mawili yanajenga mahusiano thabiti na endelevu kwa ustawi wa wananchi wake.

#DiplomasiaYaUchumi 🇹🇿🇪🇬 #TanzaniaNaMisri #UshirikianoImara #TunajengaMataifaYet

TAZARA SASA KUENDESHWA NA WACHINA MIAKA 30



KITWE, Zambia MAMLAKA ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) imetangaza kuwa Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) itachukua usimamizi na uendeshaji wa reli hiyo kwa kipindi cha miaka 27. 

Makubaliano haya, yenye thamani ya Dola bilioni 1.4 yatatoa fursa ya kurekebisha miundombinu ya reli na kuboresha ufanisi wake.

Mkurugenzi Mtendaji wa TAZARA, Mhandisi Bruno Ching'andu amesema sehemu ya uwekezaji utajumuisha ukarabati wa reli, pamoja na ununuzi wa vichwa vipya na mabehewa. Hatua hii inatarajiwa kuboresha usalama na kupanua uwezo wa usafirishaji wa abiria na mizigo.

Mkataba huu wa miaka 30 utalenga kutoa huduma bora zaidi na kudumisha operesheni za TAZARA. Serikali za Tanzania na Zambia zinatarajia kuwa mradi huu utaongeza biashara na kuimarisha usafiri kati ya nchi hizi mbili.

Kampuni ya CCECC itasimamia uendeshaji wa reli hiyo kwa miaka 27 ijayo, huku TAZARA ikifanya kazi kwa karibu kuhakikisha utekelezaji mzuri wa mradi huu.

SOURCE: HABARILEO | KITWE, Zambia MAMLAKA: ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) imetangaza kuwa Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation... | Instagram

Monday, March 17, 2025

RAIS SAMIA AIMWAGIA SIFA WIZARA YA ARDHI KWA KUSIMAMIA USTAWI WA WATANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ameishukuru Wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi chini ya Waziri wake Mhe. Deogratius Ndejembi, kwa kusimamia na kuratibu vyema maandalizi ya sera ya ardhi, akiipongeza pia kwa kubadilika kiutendaji na kuwa kinara katika utatuzi wa changamoto za ardhi na maendeleo ya watu.

Rais Samia ametoa pongezi hizo mapema leo Jumatatu Machi 17, 2025 Jijini Dodoma, wakati akizindua sera ya ardhi ya mwaka 1995 toleo la mwaka 2023, sera ambayo inatajwa kuwa muarobaini wa changamoto mbalimbali za ardhi pamoja na silaha muhimu katika uongezaji wa thamani ya ardhi kwa maendeleo ya watanzania.

MTUHUMIWA WA “KUFUTA MADENI” YA MIKOPO AKIRI KOSA, AHUKUMIWA KIGOMA

KIGOMA, Septemba 4, 2026 — Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kigoma imemhukumu Nicholaus Komba Mahitana maarufu kama Abdallah Mahimbo baad...