Friday, October 28, 2016
RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKUU WA MFUKO WA MAENDELEO WA ABU DHABI MOHAMED AL SUWAIDI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi Mohamed Al Suwaidi aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu nchini Abdullah Ibrahim Al Suwaidi aliyefika Ikulu pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi Mohamed Al Suwaidi kwa ajili ya mazungumzo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi Mohamed Al Suwaidi mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.
Thursday, October 27, 2016
KAMPUNI YA SBL YASHEREHEKEA KUTIMIZA MIAKA 20,YAZINDUA MUONEKANO MPYA WA BIA YAKE
Pichani kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie, akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habaria,wakati kampuni hiyo ikitangaza kuanza kwa sherehe maalumu ya kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa bia ya Serengeti Premium Lager (SPL) mwaka 1996. Sherehe hizo zinaambatana na uzinduzi upya wa bia hiyo ikiwa katika muonekano mpya. Helene amesema kuwa kuonesha mafanikio ya bia ya Serengeti kwa kipindi cha miongo miwilil iliyopita, kampuni ya SBL itatumia kipindi hiki kuwashukuru wateja wake na umma wa Watanzania kwa kuikubali bia ya Serengeti kama chaguo lao la hivyo kuifanya kuwa mingoni mwa bia zinazoongoza hapa nchini.
PIchani kulia ndio muonekano mpya wa bia ya Serengeti ambayo imekuja na kauli mbiu mpya wa kinywaji hicho cha “Taifa Letu. Fahari Yetu. Bia Yetu.” SBL imewakaribisha wateja wake na wadau mbalimbali kutoka sekta za umma na binafsi katika hafla ya maadhimisho ya miaka 20 ya bia ya Serengeti yatakayofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumzwa na uongozi wa kampuni ya SBL, ilipokuwa ikitangaza kuanza kwa sherehe maalumu ya kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa bia ya Serengeti Premium Lager (SPL) mwaka 1996. Sherehe hizo zinaambatana na uzinduzi upya wa bia hiyo ikiwa katika muonekano mpya.Helene amesema kuwa kuonesha mafanikio ya bia ya Serengeti kwa kipindi cha miongo miwilil iliyopita, kampuni ya SBL itatumia kipindi hiki kuwashukuru wateja wake na umma wa Watanzania kwa kuikubali bia ya Serengeti kama chaguo lao la hivyo kuifanya kuwa mingoni mwa bia zinazoongoza hapa nchini.
Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imetangaza kuanza kwa sherehe maalumu kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa bia ya Serengeti Premium Lager (SPL) mwaka 1996. Sherehe hizo zinaambatana na uzinduzi upya wa bia hiyo ikiwa katika muonekano mpya.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie, amesema mbali na kuonesha mafanikio ya bia ya Serengeti kwa kipindi cha miongo miwilil iliyopita, kampuni ya SBL itatumia kipindi hiki kuwashukuru wateja wake na umma wa Watanzania kwa kuikubali bia ya Serengeti kama chaguo lao la hivyo kuifanya kuwa mingoni mwa bia zinazoongoza hapa nchini.
“Tunawashukuru wateja wetu, wafanya biashara, wasambazaji, mashirika ya sekta binafsi, serikali na wadau wote ambao kimsingi wametusaidia na kuwa nasi katika safari yetu hii ya mafaniko,” amesema Weesie.
Bia ya Serengeti Premium Lager ni ya kwanza kutengenezwa kwa kimea kwa asilimia 100 hapa nchini ikiwa ni ubunifu wa Mpishi Mkuu mtanzania aitwaye Winston Kagusa ambaye alichanganya mbinu ya utengenezaji wa bia za kijerumani na vionjo vya hapa nchini kupata kupata kinwaji hiki kinacopendwa na wengi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu, bia ya Serengeti ilizalishwa kwa mara ya kwanza ikilenga kufikia sehemu ndogo maalumu ya soko lakini azma hii ilibadilishwa na kuzalishwa kwa wingi kutokana na ongezeko kubwa la mahitaji ya bidhaa hiyo jambo ambalo lilisababisha kuanzishwa uzalishaji zaidi katika viwanda vya SBL vilivyoko Moshi na Mwanza.
Aidha Mkurugenzi huyo ameendelea kusema kwamba katika kipindi chote cha miongo miwili bia ya Serengeti imekuwa na vifungashio vya muonekano tofauti tofauti vinavyoakisi mabadiliko ya kinyakati na mahitaji ya wateja wake. “muonekano mpya tunaouzindua leo hii ni muendelezo wa kielelezo hiki kwamba daima SBL tunajali mahitaji ya wateja wetu na tuko karibu nao, amesema Weesie.
“Tunaona fahari kuzalisha Bia ya Serengeti Premium Lager katika ubora uleule wa hali ya juu katika viwanda vyote vitatu, na huu ni uthibitisho halisi kutokana na kutambuliwa na wateja wetu wa ndani pamoja na medali zaidi ya 10 za kutambulika kimataifa ambazo bia hii imeshinda. Tunaahidi wateja wetu kwamba tutaendelea kuzalisha Serengeti Premium Lager katika ubora wa hali ya juu kwa kuzingatia vigezo vya ubora vilivyoanishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO),” amesema Weesie.
Uzinduzi wa muonekano mpya wa bia ya Serengeti pia umekuja na kauli mbiu mpya wa kinywaji hicho cha “Taifa Letu. Fahari Yetu. Bia Yetu.” Aidha kampuni hiyo imewakaribisha wateja wake na wadau mbalimbali kutoka sekta za umma na binafsi katika hafla ya maadhimisho ya miaka 20 ya bia ya Serengeti yatakayofanyika leo jijini Dar es Salaam.
WAZIRI LUKUVI ATOA TAARIFA KUHUSU UTAPELI UNAOFANYWA KWA KUTUMIA NYARAKA ZA KUGHUSHI ZA BARUA ZINAZODAIWA KUTOLEWA NA HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM
Waziri wa ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi Mhe. William Lukuvi akionesha nyaraka zilizoghushiwa na mmoja wa raia wa kigeni Bw. Hamant Patel alizotumia kujipatia fursa ya kumiliki ardhi kama raia. 
Waziri wa ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi Mhe. William Lukuvi akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake.
……………………………………………………
Katika siku za hivi karibuni kumetokea wimbi kubwa la matapeli wanaotumia nyaraka za kughushi zinazodaiwa kuwa ni Barua za Toleo zilizotolewa na iliyokuwa ofisi ya ardhi ya Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam. Nyaraka hizo za kughushi zimesababisha wananchi kupoteza fedha na mali na kuongezeka kwa migogoro mingi ya ardhi katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Dare es salaam.
Napenda kuwatahadharisha watendaji na umma wote kwa ujumla kuwa waangalifu wakati wa kuingia kwenye miamala ya mauziano au utayarishaji wa hati milki kwa kutumia nyaraka za aina hiyo. Hivyo kuanzia sasa kusifanyike muamala wala utayarishaji wa hati yoyote kwa kutumia nyaraka za aina hiyo mpaka ziwe zimehakikikwa na Kamishna wa Ardhi. Aidha, kwa wananchi wanaojihusisha na utumiaji au utayarishaji wa nyaraka za kughushi watambue kuwa hilo ni kosa kisheria na watakaobainika Wizara itahakikisha sheria inachukua mkondo wake.
Ninaagiza wananchi wote wenye nyaraka halali zilizotolewa na iliyokuwa Ofisi ya Ardhi ya Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam, wazirejesha kwa ofisi ya Kamishna wa Ardhi. Ofisi hiyo itaweka mpango maalumu wa kuhakiki na kutoa Hati Milki. Atakaye leta nyaraka za kughushi atakamatwa na kupelekwa kwenye vyombo vya dola.
B: UVAMIZI WA MAENEO YA UMMA, MASHAMBA NA VIWANJA VYENYE HATI MILKI
Nimepokea taarifa za kuwepo kwa uvamizi mkubwa wa mashamba na viwanja vinavyomilikiwa kisheria. Uvamizi huo unafanywa kwa vizingizio mbalimnbali ikiwemo wavamizi kudai kuwa ni mapori, uhaba wa ardhi na sababu nyinginezo zisizo za kisheria. Kuvamia shamba au kiwanja ni kosa la jinai kwa mujibu wa fungu la 175 la Sheria ya Ardhi Na. 4 (1999).
Ninazo taarifa pia za uvamizi mkubwa katika maeneo ya Mabwepande, Pugu Kajiungeni na maeneo ya Bagamoyo na maeneo mengine nchini. Ninazo taarifa pia baadhi ya viongozi wanashiriki katika kusaidia uvamizi wa viwanja na mashamba ya watu. Na wavamizi hawa wamethubutu hata kuwatisha maofisa wetu wanapokuwa kazini. Tabia hii haiwezi kuvumiliwa na lazima hatua kali za kisheria zichukuliwe. Sheria inaweka wajibu wa msingi kwa vyombo vya dola, Halmashauri na wamiliki kulinda haki za kumiliki ardhi.
Ninamwagiza Kamishna wa Ardhi, na Makamishna Wasaidiziwa Kanda kuweka mkakati maalum wa kukomesha tabia hiyo ya uvamizi kwa kushirikiana na vyombo vya dola na ofisi za Halmashauri.
C: UDANGANYIFU WA URAIA KWA AJILI YA KUJIPATIA MILIKI ZA ARDHI
Sheria za ardhi zinaelekeza kuwa ardhi ya Tanzania itamilikishwa kwa raia wa Tanzania. Wageni wanayo fursa ya kupata ardhi hiyo ikiwa wataihitaji kwa ajili ya uwekezaji kupitia Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC).

Tunazotaarifa kuwa baadhi ya wageni (foreigners) wakishirikiana na raia hufanya udanganyifu na kughushi nyaraka za uraia ili kujipatia miliki za ardhi kama raia. Udanganyifu huo umekuwa pia ukifanywa na makampuni ambayo hujisajili kama makampuni raia kwa kutoa hisa nyingi kwa raia na mara baada ya kupata ardhi huhamisha hisa zote kwenda kwa wageni.
Kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi Na. 4 (1999) Kampuni ni raia iwapo tu hisa nyingi (majority shares) katika kampuni hiyo zinamilikiwa na raia. Inapotokea mabadiliko ya umiliki wa hisa kwenye kampuni kupelekea hisa nyingi kumilikiwa na wageni, Kampuni hiyo inakoma kuwa raia kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi Na. 4 (1999) na inakosa sifa ya kumiliki ardhi kama raia tangu siku ambayo itasomeka hisa nyingi zinamilikiwa na wageni.
Tumeanza sasa kazi ya kuhakiki kwa kushirikiana na Msajili ya Makampuni (BRELA) makampuni yote yanayomiliki ardhi kama raia ili kubaini kama bado yana sifa ya kumili ardhi kama raia. Na iwapo itabainika kuwa kampuni imepoteza sifa ya uraia, hatua za kisheria zitachukuliwa juu ya miliki ya ardhi inayomilikiwa na Kampuni hiyo ikiwemo kurejesha ardhi hiyo mikononi mwa serikali.
Kwa wageni ambao wameghushi nyaraka za uraia na kujipatia fursa ya kumiliki ardhi kama raia, tumeweka mkakati maalum kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji kuwabaini na mara ikithibitika tutafuta miliki zao.
Nawatakia Siku Njema
William Vangimembe Lukuvi (Mb)
WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

Tamasha la Uhondo wa Zantel lazidi kupasua anga
Msanii maarufu wa muziki wa ‘singeli’ Rajabu Selemani ‘virusi mdudu’ (kushoto), akikonga nyoyo za wakazi wa kimara na maeneo ya jirani katika tamasha la Uhondo za Zantel katika viwanja vya Rhino, Kimara, Dar es Salaam juzi, ikiwa ni moja ya kampeni za kampuni ya simu za mkononi ya Zantel kuwa karibu na wateja wake ikiwajulisha bidhaa na huduma zao zilizopo sokoni.

Baadhi ya watu waliojitokeza katika tamasha la Uhondo wa Zantel wakiselebuka wakati mmoja wa wasanii waliopamba tamasha hilo akitumbuiza.
Tamasha la Uhondo wa Zantel linalodhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Zantel limeendelea kukonga nyoyo za wakazi wa sehemu mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam mara hii ikiwa ni zamu ya wakazi wa Kimara na maeneo ya jirani kama inavyoonekana katika picha hizi hapa chini.
WAZIRI MAKAMBA AKAMILISHA ZIARA KATIKA MKOA WA KATAVI
Bibi Josephine Rupia, Mkuu wa Idara ya Maliasili Halmashauri ya Mpanda akitoa maelezo ya Mto Katuma kupoteza mwelekeo wa kutiririsha maji katika mkondo wake kama ilivyokuwa hapo awali. Wengine katika picha ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akihutubia wananchi wa kijiji cha Kabage kilichopo Mkoani Katavi na kuwasisitizia umuhimu wa Hifadhi ya Mazingira
Mmiliki wa Kiwanda cha kutengeneza chumvi cha Nyanza Mining akitoa maelezo kwa Waziri Makamba juu uzalishaji wa chumvi hiyo kwa kutumia nishati ya jua.
TAARIFA YA ZIARA YA MHE. JANUARY MAKAMBA KATIKA MKOA WA KATAVI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe January Makamba hii leo ameendelea na ziara yake katika Mkoa wa Katavi kwa kutembelea kijiji cha Kabege ambapo aliangalia mradi Mkubwa wa Umwagiliaji wa Mwamkulu katika Manispaa ya Mpanda ambao kwa sasa umesitisha kutoa huduma zake kwa kukosekana kwa maji ya kutosha katika Mto Katuma.
Katika kikao cha Majumuisho ya Ziara yake ya siku mbili katika Mkoa wa Katavi, Waziri Makamba ameutaka uongozi wa Mkoa huo kudhibiti yafuatayo:
1. Ongezeko la watu na mifugo ambayo kwa kiasi kikubwa inachangia uharibifu wa mazingira.
2. Kusitisha uchepushaji kwa Mto Katuma ambapo taarifa ya Mkoa ilieleza kuna jumla ya mabanio 40 ambayo yanatumiwa na watu kuchepusha maji kwa ajili ya manufaa yao binafsi.
3. Uchimbaji hatari wa Madini usiofuata taratibu
4. Kuhuisha sheria ndogo ndogo za mazingira katika ngazi mbalimbali za Serikali za mitaa
5. Kuanisha maeneo maalumu ambayo yatatangazwa katika Gazeti la Serikali kama mazingira nyeti ili kuyapa ulinzi zaidi
6. Kusimamia uondoshwaji wa wavamizi katika Vyanzo vya maji
7. Kufanyika kwa sensa ya mifugo ili kujua Mkoa una mifugo kiasi gani na kubuni namna bora ya kuhumudimia mifugo hiyo bila kuathiri mazingira
8. ameahidi kuaanda andiko maalumu la Mradi wa Ziwa Katuma
9. Mmiliki wa Jema Sitalike Project kutafutwa popote alipo, leseni yake ya madini isitishwe, apigwe faini na kurekebisha eneo alilokuwa akitumia awali kwa shughuli za uchenjuaji wa dhahabu.
10. Waziri Makamba meagiza Watendaji kata na Vijiji kutotoa vibali vya uchimbaji wa madini bila kufuata utaratimu wa Wizara ya Nishati na Madini
Mara baada ya Majumuisho Waziri Makamba alipata fursa ya kuongea na wanakijiji cha Kabage na kusisitiza yafutayo:
1. Wananchi kutunza mazingira kwa kutofanya kilimo cha kuhamahama, Ukataji Ovyo wa Miti na Uchomaji wa misitu.
2. kuwakumbusha wananchi kuwa rasilimali ya maji ni ya watu wote hivyo isiwanufaishe watu wachache
3. Serikali inaangalia namna bora ya kurudisha Mto Katuma katika njia yake ya awali ambayo ilipotea baada ya kutokea kwa mafuriko mwaka 1998
4. Kuundwa kwa jumuiya za watumia maji na kuzingatia Sheria ya Mazingira ya kutofanya shughuli zozote za kibinadamu ndani ya mita sitini za chanzo cha maji
5. Kuundwa kwa Kamati ya Mazingira katika Kijiji hicho
6. Kuondokana na Makazi holela kwa kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi.
Waziri Makamba amewasili Katika Mkoa wa Kigoma na kutembelea kiwanda cha Nyanza Mines na kuwapongeza kwa kuzalisha chumvi kwa kutumia nishati ya jua ambapo awali kiwanda hicho kilifungiwa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kutokana na uharibifu wa Mazingira kwa kutumia magogo mengi mwaka 2015. Kiwanda hicho kwa sasa kinazalisha tani 20,000-25,000 ndani ya miezi mitatu.
Subscribe to:
Posts (Atom)
RAIS SAMIA AZINDUA TUME YA UCHUNGUZI KWA AJILI YA KUIMARISHA AMANI, HAKI NA UWAJIBIKAJI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Wajumbe wa Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Wahusi...
-
Hapa mmoja wa watoto hao akiwa na kijana mwenzake mwenye miaka 18, wote wako sawa lakini yeye hawezi kuzungumza kama watu wa kawaida. Mama S...
-
Nadhani mtakumbuka kibwagizo maarufu katika TV ambacho kinaimbwa perupe pepero perupe pepero hawa ni vijana wa Sisi Tambala waliokuwapo kati...
-
Mdau Julius Samwel hivi karibuni alikuwa huko Mwanza na hizi ndizo alizofanikiwa kutumegea, wadau hebu someni hicho kibao mniambie kuna nini...