Thursday, November 03, 2016

SPIKA WA KWANZA WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI, KATIBU MKUU WA CCM, ABDULRAHMAN KINANA AKUTANA NA WABUNGE WA BUNGE HILO LEO


Spika wa kwanza wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akizungunguza na wabunge wa Bunge hilo, walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam, ili umsalimia na kupata mawazo kutokana na uzoefu wake hasa alipokuwa Spika wa Bunge hilo la Afrika Mashariki. Wa Kwanza kulia upande wa mstari wa kushoto, ni Mwenyekiti wa Wabunge hao, Makongoro Nyerere, Shayrose Bhaji, Yves Nsabimana, Maryam Ussi, Twaha Tasilima, Wilime Asheri ambaye ni mratibu EALA, na kutoka kulia, mstari wa kulia ni, Katibu wa NEC Oganaizesheni, Mohammed Seif Khatib, na Wabunge wa EALA, Adam Kimbisa, Bernard Murunya, Abdulla Mwinyi,Angela Kizigha na mwisho Msemaji wa CCM, Christopher Sendeka.
Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere, akiwasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, kuongoza msafara wa wabunge hao kumsalimia Spika wa kwanza wa Bunge hilo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, leo 
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shy-rose Bhanji, akiwasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, wakati msafara wa wabunge yeye na wabunge wenzake wa Bunge hilo, walipofika kumsalimia Spika wa kwanza wa Bunge hilo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, leo 
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shy-rose Bhanji, akiwasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, wakati msafara wa wabunge yeye na wabunge wenzake wa Bunge hilo, walipofika kumsalimia Spika wa kwanza wa Bunge hilo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, leo. Kulia ni Mbunge Bunge hilo, Yves Nsabimana. 
Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere, akiteta jambo na Mbunge wa Bunge hilo, wakati wakimsubiri kuingia ukumbini, Spika wa kwanza wa Bunge hilo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, leo
Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Mohammed Seif Khatib akisalimiana na Mbunge wa Bunge la Afika Mashariki Bernard Murunya, alipowasili wakati Wabunge wa Bunge hilo, walipofika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumbai Dar es Salaam, kumsalimia Spika wa kwanza wa Bunge hilo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, leo. Katikati ni Adam Kimbisa. 


Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Mohammed Seif Khatib akifurahia jambo na Makongro Nyerere wakati wakisalimiana ukumbini, kabla ya Kinana kuwasili
Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Mohammed Seif Khatib akisalimiana na Mbunge wa Bunge la Afika Mashariki Shy-Rose Bhanji, alipowasili wakati Wabunge wa Bunge hilo, walipofika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumbai Dar es Salaam, kumsalimia Spika wa kwanza wa Bunge hilo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, leo.
Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Mohammed Seif Khatib (kulia), akiwa na Wabunge wa Bunge la Afika Mashariki, Adam Kimbisa, Bernard Murunya, na Abdulla Mwinyi, wakati wakimsubiri Kinana kuingia ukumbini 
Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki Yves Nsabimana na Maryam Ussi, wakibadilishana mawazo ukumbini
Mbunge wa Afrika Mashariki Angela Kizigha akimsalimia Mbunge mwenzake wa Bunge hilo, Bernard Murunya alipowasili ukumbini

Spika wa kwanza wa Bunge la Afrika Mashariki, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsalimia Mweneyekiti wa Wabunge wa Bunge hilo, Makongoro Nyerere alipowasili ukumbini
Kinana akimsalimia Shy-Rose Bhanji
Spika wa kwanza wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akizungunguza na wabunge wa Bunge hilo, walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam, ili umsalimia na kupata mawazo kutokana na uzoefu wake hasa alipokuwa Spika wa Bunge hilo la Afrika Mashariki.
Spika wa kwanza wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akizungunguza na wabunge wa Bunge hilo, walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam, ili umsalimia na kupata mawazo kutokana na uzoefu wake hasa alipokuwa Spika wa Bunge hilo la Afrika Mashariki. 
ukumbini
Spika wa kwanza wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akiwa katika picha ya pamoja baada ya kuzungunguza na wabunge wa Bunge hilo, walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam, ili umsalimia na kupata mawazo kutokana na uzoefu wake hasa alipokuwa Spika wa Bunge hilo la Afrika Mashariki.
Shy-Rose Bhanji akimshukuru Kinana.
Kisha akapozi naye kwa picha ya kumbukumbu
Halafu akapozi na Msemaji wa CCM, Ole Sendeka
Baadaye tena akajipiga selfie, akiwa na Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Zakia Meghji
Spika wa kwanza wa Bunge la Afrika Mashariki, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiagana na Makongoro Nyerere
Spika wa kwanza wa Bunge la Afrika Mashariki, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiagana na Twaha Tasilima. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO-theNkoromo Blog

EACJ CONGRATULATES DEPUTY PRINCIPAL JUDGE UPON HIS APPOINTMENT TO THE SUPREME COURT OF KENYA

 Justice Lenaola (R) taking the oath as a Judge of the Supreme Court of Kenya. Administering the oath is the Chief Registrar of the Judiciary, Ms. Anne Atieno Amadi.
 President Uhuru Kenyatta congratulates His Lordship Justice Lenaola upon his appointment as Supreme Court Judge.

EACJ congratulates the Deputy Principal Judge, Justice Isaac Lenaola, upon his new appointment as Judge of the Supreme Court Kenya

East African Court of Justice, Arusha, 31st October, 2016: The Judge President of the East African Court of Justice (EACJ), Hon. Justice Dr. Emmanuel Ugirashebuja, has on behalf of the Court congratulated Hon. Justice Isaac Lenaola upon his new appointment as a judge of the Supreme Court of the Republic of Kenya.

Justice Lenaola who has been a Judge at the High Court of Kenya has been promoted to the Supreme Court of Kenya after a rigorous recruitment process. His Lordship has replaced retired Justice Philip Tunoi, former Vice President of the EACJ. Until his appointment, Justice Lenaola was the head of the Constitutional and Human Rights Division at the High Court of Kenya.

The Summit of the EAC Heads of State appointed His Lordship Justice Lenaola as a Judge of the EACJ, First Instance Division, in April 2011 and consequently designated him as the Deputy Principal Judge of the same Division in November 2013, a position he still holds to date. Justice Lenaola replaced retired Hon. Lady Justice Mary Stella Arach Amoko from the Republic of Uganda with effect from 1st December, 2013.   

The President of the Court, Hon. Justice Dr. Ugirashebuja hailed Justice Lenaola upon his new appointment and wishes him success in his new role as a Supreme Court judge.

Hon. Justice Dr. Ugirashebuja said that Justice Lenaola’s elevation from the High Court to the Supreme Court demonstrates the judge’s industriousness and commitment to serve, thus his being entrusted with a greater assignment.   

His Excellency, President Uhuru Kenyatta swore in Justice Lenaola as a Judge of the Supreme Court on 28th October, 2016. Also sworn in at the same ceremony was Justice Philomena Mwilu as the Deputy Chief Justice of the Republic of Kenya.

Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje afungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Troika ya SADC

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Kikao cha Makatibu Wakuu na Maafisa Waandamizi wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC Troika), Balozi Dkt. Aziz Mlima akifungua rasmi Kikao cha Makatibu Wakuu na Maafisa Waandamizi kutoka Asasi hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupitia agenda mbalimbali zitakazowasilishwa na kujadiliwa kwenye Kikao cha Mawaziri kitakachofanyika tarehe 03 Novemba, 2016 katika Ukumbi huo. Asasi ya SADC inaundwa na nchi tatu ambazo ni Tanzania (Mwenyekiti), Angola (Makamu Mwenyekiti) na Msumbiji (Mwenyekiti aliyemaliza). Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika, Mhe. Dkt. Stergomena Tax. 
Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza wakati wa kikao cha Makatibu Wakuu. Kulia ni Balozi Mlima. 
Sehemu ya Makatibu Wakuu na Maafisa Waandamizi kutoka Tanzania wakifuatilia ufunguzi wa kikao. Kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi HassanYahya Simba, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Bw. Job Masima na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Innocent Shiyo. 
Sehemu ya Ujumbe wa Msumbiji wakifuatilia ufunguzi wa mkutano huo 
Sehemu ya ujumbe kutoka Angola wakati wa ufunguzi wa kikao cha Makatibu Wakuu 
Sekretarieti ya SADC .
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania wakati wa kikao hicho cha Makatibu Wakuu

Wednesday, November 02, 2016

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA NA MATUKIO BUNGENI DODOMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Waganga wa Tiba Asili Tanzania waliotembelea Bunge kwa mwaliko wa Makamu Mwenyekiti wao ambaye pia ni Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephene Hillary Ngonyani maarufu kwa jina la Profesa Maji Marefu, Novemba 2, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Novemba 2, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum, Kunti Majala kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma Novemba 2, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya wabunge kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Novemba 2, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Asilimia 85 ya Ardhi nchini haijapimwa,Watu wengi wanaendelea kuishi katika makazi holela-Waziri Lukuvi

Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akifungua mkutano mkuu na Kongamano la Wapimaji Ardhi linalofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia leo Novemva 2-3, 2016.
Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akionyeshwa moja ya vifaa vinavyotumika katika upimaji wa Ardhi mapema leo katika Mkutano mkuu na Kongamano la Wapimaji Ardhi unaofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akipewa maelezo jinsi mambo yalivyobadirika katika mfumo wa Kidigitali.
Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akiwa amebeba moja ya kifaa kinachotumika katika upimaji.
Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akionyeshwa kifaa cha kisasa kinachotumika katika upimaji.
Wapimaji wa Ardhi wakiwa katika mkutano Mkuu na Kongamano la Wapimaji Ardhi.
Wapimaji wa Ardhi wakiwa katika mkutano Mkuu na Kongamano la Wapimaji Ardhi.
Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akitoa cheti cha shukrani kwa makampuni yaliweza kusaidia kufanikisha mkutano Mkuu na Kongamano la Wapimaji Ardhi. Pembeni kushoto ni Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani, Bw. Justo Lyamuya.
 
Na Chalila Kibuda, Globu ya jamii.
 
Hayo ameyasema leo Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi wakati akifungua Mkutano Mkuu na Kongamano la Wapimaji Ardhi uliofanyika jijini Dar es Salaam, amesema kuwa wataalam wafanye kazi ya kupima ardhi ili kuweza kuondokana na makazi holela.

Amesema kuwa serikali inapoteza mapato kutokana na kuwa na sehemu kubwa ya ardhi kutopimwa.Lukuvi amesema wapimaji wa sekta binafsi wamekuwa wakifanya vizuri kuliko wale ambao wameajiliwa na serikali.

Amesema lazima kuondokana na mfumo wa hati kwenye karatasi na kuingia katika mfumo wa kieletroniki katika kusaidia wananchi kudhulumiwa ardhi kwa kushirikiana na watumishi wasio waaminifu.

Waziri Lukuvi amesema ni marufuku kwa wapimaji ardhi walioajiliwa na serikali kuwa kampuni za upimaji wa ardhi ili kuondokana na mgongano wa kimasilahi. Amesema katika miaka 10 ijayo kuwa kila mtu kuwa hati na kiwanja au shamba kiwe kimepimwa.Lukuvi amesema katika kuondoa migogoro ya wafugaji ni kuondokana na uchungaji wa mifugo.

Amesema kufika mwishoni mwa mwaka huu wawe wamepima ardhi viwanja 400.Nae Rais IST, Martins Chodata amesema kuwa watashirikiana na serikali katika masuala ya upimaji ardhi.Amesema wapo baadhi ya wapimaji ardhi hawana maadili na kusababisha kuwepo migogoro. 

UN NA EU ZATOA EURO LAKI NANE KUSAIDIA WATOTO WA KIKE

Shirika la Umoja wa Mataifa la UN kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU) wametoa Euro laki nane kuwasaidia watoto wa kike wanaoishi katika mazingira magumu na wahanga wa mimba za utotoni waishio kwenye kituo cha Faraja Young Women Development Unit .

Mwakilishi wa EU ambaye ni Afisa Miradi Anna Muro amesema kuwa msaada huo utasaidia kuwawezesha wanawake Waweze kushiriki kwenye maendeleo ya jamii .

Akizungumza katika kituo hicho kinacholelea watoto 30 wenye watoto ambao walipata mimba katika umri mdogo na kushindwa kuendelea na masomo ambapo wanasaidiwa na kituo hicho kupata elimu ya ufundi wa ushonaji na mapishi ili kupata stadi zitakaowasaidia kujikwamua kimaisha.

Mwasisi wa Shirika la Faraja Young Women Development, Martina Simon Siara akitoa maelezo kwa Maafisa wa UN na EU wakati walipotembelea kituo shirika hilo. Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama, Mwakilishi wa EU ambaye ni Afisa Miradi, Anna Muro (wa pili kulia) pamoja na Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu (kulia).(Picha na Ferdinand Shayo).

Anna amesema kuwa watoto wengi wanakabiliwa na changamoto ya usafirishaji wa binadamu jambo ambalo ni kinyume cha haki za binadamu na haki za watoto hivyo amewataka Jamii na serikali kupiga vita usafirishwaji wa watoto.

Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama amewataka watoto wanaoishi katika kituo hicho kutumia fursa ya mafunzo wanayoyapata kujiendeleza kielimu na kukua kiuchumi ili kutokomeza umasikini na mimba za utotoni kwa watoto wa kike.

Muasisi wa kituo hicho Martina Simon Siara ameshukuru ugeni kutoka UN na EU uliofika kituoni hapo kwa ajili ya kutazama shughuli mbalimbali zinazofanywa na kituo hicho pamoja na kuwaunga mkono ili waweze kuongeza tija katika kuisaidia jamii.
Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama (wa pili kulia) na Mwakilishi wa EU ambaye ni Afisa Miradi, Anna Muro (wa pili kushoto) wakipata maelezo kutoka kwa Muasisi wa Shirika la Faraja Young Women Development, Martina Simon Siara (kulia) walipotembelea shirika hilo lililopo jijini Arusha.
Wawakilishi kutoka EU na UN wakitazama shughuli za mikono zinazofanywa na watoto wanaoishi katika kituo cha Faraja Young Women Development Unit walipotembelea kituo hicho hivi karibuni kilichopo jijini Arusha.
Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama na Mwakilishi wa EU ambaye ni Afisa Miradi, Anna Muro wakishirikiana kuingiza shanga ambazo hutumika kushona mavazi ya utamaduni yanayoshonwa na watoto wa kike wanaoshi katika kituo cha Faraja Young Women Development Unit (katikati) ni mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Rosemary Innocent.
Binti mwenye ulemavu wa ngozi, Rosemary Innocent na wenzake wakiendelea na darasa la kutengeneza vitu mbalimbali kituoni hapo.
Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama (kushoto) na Mwakilishi wa EU ambaye ni Afisa Miradi, Anna Muro katika picha ya pamoja na binti aliyeshona vazi la kuvutia la kimasai lililonakshiwa na shanga walipotembelea kituo hicho.
Wawakilishi wa UN na EU wakitazama kitengo cha elimu ya mapishi katika Kituo cha Faraja Young Women Development Unit.
wanafunzi wanaojifunza ushonaji katika Kituo cha Faraja Young Women Development Unit.
Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama akitazama mabinti wanaojifunza ushonaji nguo kituo cha Faraja Young Women Development Unit walipokitembelea kituo hicho kilichopo jijini Arusha.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu akifafanua jambo kwa vijana na watoto wanaoishi katika kituo hicho walipokitembelea jijini Arusha.
Mwakilishi wa EU ambaye ni Afisa Miradi, Anna Muro akizungumza na wale, vijana pamoja na watoto wanaoishi kwenye kituo cha Faraja Young Women Development Unit walipokitembelea kituo hicho kilichopo jijini Arusha.
Wawakilishi wa UN na EU katika picha ya pamoja na walezi na watoto wanaoishi kwenye kituo hicho.

RAIS SAMIA AZINDUA TUME YA UCHUNGUZI KWA AJILI YA KUIMARISHA AMANI, HAKI NA UWAJIBIKAJI

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Wajumbe wa Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Wahusi...