Friday, August 01, 2014

CHUO CHA CBE CHAZINDUA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 JIJINI DAR, WADAU MBALIMBALI WAPONGEZA UBORA WA ELIMU INAYOTOLEWA

         Picha_na_1[1]
Mbunge wa Ilala Mh. Mussa Zungu ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa Uzinduzi wa Maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) akikata utepe kuashiria uzindunzi wa maadhimisho ya chuo hicho kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Picha_na_2[1]
Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) wakiangalia moja ya picha ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyopigwa wakati akifungua Chuo hicho Januari, 1965. Kutoka kushoto ni Mkuu wa chuo hicho Prof. Emanuel Mjema, Mh. Musa Zungu (Mb) jimbo la Ilala,Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda,Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho Prof. Mathew Luhanga na Prof.Eliuta Mwageni Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha.
Picha_na_3[1]
Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) wakiwa katika picha ya pamoja wakiongozwa na Mbunge wa Ilala Mh. Mussa Zungu na Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (katikati). Nyuma ni bango lenye picha ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyopigwa wakati akifungua Chuo hicho mwaka 1965.
Picha_na_4[1]
Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Tunu Pinda kwa niaba ya wanafunzi waliosoma katika chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam akizungumza na wadau na wanajumuiya wa Chuo hicho wakati wa  uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo hicho jijini Dar es salaam. 
Picha_na_5[1]
 Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam Prof. Emanuel Mjema (kulia) akiwaongoza wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho jijini Dar es salaam.
Picha_na_6[1]
Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Tunu Pinda (katikati) akizungumza akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam Prof. Mathew Luhanga (kushoto).Wengine Mkuu wa Chuo hicho Prof. Emanuel Mjema.
Picha_na_7[1]
Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam wakiendelea na shughuli mbalimbali chuoni hapo
Picha_na_8[1]
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam Prof. Emanuel Mjema (kulia) akiwakaribisha wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho jijini Dar es salaam.
Picha_na_9[1]
Wadau mbalimbali  na Wanajumuiya wa Chuo Cha Elimu ya Biashara wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho jijini Dar es salaam.
Picha_na_10[1]
Kikundi cha ngoma kutoka Jeshi la Polisi kikiongozwa na Afande Juma Boha Mnyaa kikitoa burudani ya ngoma ya asili ya ya Kibati kutoka Kusini Pemba wa uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) jijini Dar es salaam.

MKUTANO MKUU WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA KIKAPU AFRIKA WAFANYIKA MADAGASCAR

photo_1[1]
Rais wa FIBA Yvan Mainini akiwa na baadhi ya wadau wa kikapu dunianiphoto_2[1]
Makamu wa Rais wa NBA Akitoa mada kwenye mkutano huophoto_4[1]
Ndg. Magesa akisalimiana na Rais wa FIBA Ndg.Yvan Mainini
photo_5[1]
Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Rais wa TBF Ndg.Bandiye na Katibu Mkuu Zonga

LHRC YATOA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI YA NUSU MWAKA KUANZIA JANUARY HADI JUNI 2014

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Helen Kijo-Bisimba
Mtafiti wa Tafiti mbalimbali wa LHRC, Wakili Pasience Mlowe.
Mkurugenzi wa Uwezeshashi na Uwajibikaji wa LHRC, Imelda Urrio
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Helen Kijo-Bisimba (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leoasubuhi, wakati akitoa taarifa ya kituo hicho ya kipindi cha nusu mwaka kuanzia Januari hadi kufikia Juni 2014. Kulia ni Mkurugenzi wa Uwezeshashi na Uwajibikaji wa LHRC, Imelda Urrio na Mtafiti wa LHRC, Pasience Mlowe.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.

Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakiwachua picha za utoaji wa taarifa hiyo.
Mtafiti wa Tafiti mbalimbali wa LHRC, Wakili Pasience Mlowe (kushoto), akisoma taarifa hiyo kwa wanahabari. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Helen Kijo-Bisimba
Wanahabari wakiwachua picha za utoaji wa taarifa hiyo. Imeandaliwa na www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
 
Dotto Mwaibale
 
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimesema kuwa hadi kufikia Juni 2014 wanawake na wasichana 2878 wamebakwa nchini kutokana na vitendo vya ukatili dhidi yao.
 
Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Dk. Helen Kijo-Bisimba wakati akitoa taarifa ya kipindi cha nusu mwaka kuanzia Januari na Juni mwaka huu kwa vyombo vya habari Dar es Salaam leo.
 
“Vitendo hivyo vya kikatili dhidi ya makundi hayo vilivyoripotiwa polisi kwa nchi nzima vilikuwa 3,633″ alisema Kijo -Bisimba.
 
Kijo-Bisimba alisema taarifa hii inatoka na tafiti zilizofanywa na kituo hicho ili kufuatilia ukiukwaji wa haki za binadamu kutoka kwa waangalizi wa haki za binadamu, wasaidizi wa sheria, taarifa rasmi kutoka taasisi za Serikali, Bunge, Mahakama,vyombo vya habari na asasi mbalimbali zisizo za kiserikali.
Akizungumzia kuhusu taarifa ya Sensa ya watu na makazi inaonesha idadi kubwa ya watu wanaishi vijijini huku wakiwa na huduma duni za kijamii kama za afya, maji, umeme, umeme na shule.
 
Alisema takwimu zinaonesha bado vijijini kuna makazi duni ya wananchi kutokana na gharama kubwa za saruji na vifaa vya ujenzi, mfano katika suala la upatikanaji maji makazi 3,959,857 yanatumia vyanzo vya maji visivyo salama ukilinganisha na makazi 1,902,244 yanayotumia maji ya bomba nchi nzima.
 
Kuhusu kilimo alisema idfadi ya wananchi wengi wapatao 11,359,090 wanategemea kilimo kama shughuli kuu ya uchumi hata hivyo wakulima wengi bado wanatumia jembe la mkono.
 
“Uwekezaji katika mashamba makubwa wamepewa wawekezaji wakubwa mfano mashamba makubwa ya mpunga yaliyokuwa ya Shirika la NAFCO wilayani Mbarali mkoani Mbeya wamepewa wawekezaji na wakulima wazawa wametengewa yasiyofaa” alisema Kijo-Bisimba.

NAIBU WAZIRI MAKALLA AKAGUA MIRADI YA VISIMA VYA MAJI MKURANGA

 Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (kulia), akipata maerlezo kutoka kwa kiongozi wa Mafundi wa Kampuni ya CDM Smith, John Donoherth, kuhusu ujenzi wa kisima kilichopo Mkwalia Mkuranga ambacho ni moja kati ya visima 8 vinavyofanyiwa utafiti maji wilayani humo. Makalla alifanya ziara ya kukagua miradi ya maji wilayani Mkuranga mkoani Pwani leo. Pia alikagua mradi wa  kisima cha maji cha Nyamato chenye uwezo wa kutoa maji lita 26,000 kwa saa kitakachohudumia wakazi wa vijiji vya  Mvuleni, Nyamato na Kilimahewa. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Waziri Makalla akiangalia mradi wa kisima cha Mkwalia ambacho kinafanyiwa utafiti
 Maji yakitiririka kwenye kisima hicho
 Makalaa akijadiliana jambo na Mkandarasi wa kisima hicho,John Donoherth
Naibu Waziri Makalla akielezea namna Kisima kipya cha Nyamato kikianza kufanya kazi kuwa kitakuwa kinatoa lita 26,000 za maji kwa saa na kuhudumia sehemu kubwa ya wananchi wilayani Mkuranga, Pwani. Atakizindua kisima hicho mwanzoni mwezi ujao kitakapowekwa pampu iliyoagizwa Afrika Kusini. Kulia ni Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Nyamage, Abdallah Kiyewehe ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya maji kijijini hapo.
 Mama mkazi wa Kijiji cha Mvuleni, wilayani Mkuranga akielezea mbele ya waziri jinsi wanawake wa eneo wanavyopata taabu ya kuata maji karibu umbali wa Km 5, na kuonesha furaha ya kupata kisima hicho kitakachowaondolea adha waliyokuwa wanaipata.
 Eneo la Kisima cha Nyamato kilichogauliwa. Kisimamhicho kinasubiri pampu tu ili kianze kufanya kazi.
 Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mvuleni baada ya kukagua kisima cha maji cha Nyamato, wakati wa ziara yake wilayani Mkuranga leo.
Sehemu ya umati mkubwa wa wananchi ukimsikiliza Makalla akihutubia kwa kuwaeleza mikakati ya Serikali ya kuwaboreshea wananchi sekta ya maji., ambapo  zimetengwa zaidi ya Bilioni moja kwa ajili ya wilaya hiyo.
 Wananchi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Makalla
 Katibu wa Kamati ya Maji ya Mradi wa Nyamato, Ali Salum akielezea jinsi mradi wa Nyamato unavyosuasua kuzinduliwa, akidai anayesababisha hivyo ni Mkandarasi wa mradi huyo ambaye hatoi taarifa yoyote juu ya ucheleweshwaji huo.
 Mkandarasi wa mradi wa maji wa Nyamato, Jamila Chibwana wa Kampuni ya Mac Consultant  akitoa majibu ya ucheleweshwaji wa mradi huo, ambapo alisema moja ya sababu zilizosababishwa ni kutopewa fedga za ujenzi kwa wakati na uagizaji wa pampu kutoka Afrika Kusini.
Makalla akiagana na wananchi baada ya mkutano kumalizika.

UKAWA WAKUTANA NA WAANDHISHI WA HABARI JIJINI DAR

Mwenyekiti wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) Profesa Ibrahim Lipumba (katikati) akisisitiza jambo wakati akiongea na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutoa Tamko kuhusu Wito wa Viongozi wa Dini wa kurudi Bungeni.kushoto ni Mwenyekiti wa Chadema,Mh. Freeman Mbowe na wa pili kulia ni Mwenyeti wa NCCR-Mageuzi,Mh. James Mbatia.Kulia ni Katibu Mkuu wa Chadema,Dkt. Wilbrod Slaa.
Viongozi wakuu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wakishikana mikono kuashiria umoja mara baada ya kuongea na wandishi wa habari kutoa Tamko la Ukawa kuhusu Wito wa Viongozi wa Dini wa kurudi Bungeni.kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi,Mosena Nyambabe,Mwenyekiti wa Chadema,Mh.Freeman Mbowe ,Mwenyekiti wa CUF,Profesa Ibrahim Lipumba,Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi,Mh. James Mbatia na Katibu Mkuu wa Chadema,Dkt. Wilbrod Slaa wakiwa nje ya makao makuu ya cuf.

RUKWA SET FOR ECONOMIC BOOM AS TANZANIA PLANS TO EXPORT POWER TO NEIGHBOURING COUNTRIES

Rukwa Region is poised for a major economic transformation following the completion of the Malangali Power Substation, a project expected to...