NAIBU WAZIRI DK MABULA AICHAGIZA NHC KATIKA UJENZI WA MJI WA SERIKALI MTUMBA

Mhandisi Peter Mwaisabula ambaye anasimamia mradi wa ujenzi wa jengo la Wizara ya Nishati linalojenga katika mji wa serikali katika eneo la Mtumba Jijini Dodoma akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula aliyetembelea mradi huo wa ujenzi leo asubuhi.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula akitembelea mradi wa ujenzi wa jengo la Wizara ya Fedha na Mipango linalojenga katika mji wa serikali katika eneo la Mtumba Jijini Dodoma, Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Sophia Kongela akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa Shirika la Nyumba la Taifa, Abdallah Migilla.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula akielekea kutembelea mradi wa ujenzi wa jengo la Wizara ya Viwanda na Uwekezaji linalojenga katika mji wa serikali katika eneo la Mtumba Jijini Dodoma,
Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa, Haikamen Mlekio  akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula aliyetembelea mradi huo wa ujenzi leo asubuhi,



Mhandisi wa Matengenezo wa Shirika la Nyumba la Taifa, Julius Ntoga akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Sophia Kongela kwenye mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango lililopo eneo la Mtumba jijini Dodoma.


Mhandisi Peter Mwaisabula ambaye anasimamia mradi wa ujenzi wa jengo la Wizara ya Nishati linalojenga katika mji wa serikali katika eneo la Mtumba Jijini Dodoma akimsindikiza Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Sophia Kongela  aliyetembelea mradi huo wa ujenzi leo asubuhi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Sophia Kongela akisalimiana na mmoja wa waratibu wa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu akati alipotembelea mradi wa ujenzi wa jengo la Wizara ya Fedha na Mipango linalojenga katika mji wa serikali katika eneo la Mtumba Jijini Dodoma wanaoshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani (Kushoto)
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Sophia Kongela akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani mbele ya mradi wa jengo la Nishati.
Jengo la Wizara ya Viwanda na Biashara likiwa katika hatua za mwiszho za ujenzi.



Jengo la Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi likiwa limeshaanza kuwekwa madirisha na kenzhi kwaajili ya kuanza kuezeka linavyoonekana kwa sasa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Sophia Kongela akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Nyumba ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Pius Tesha.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani akiangalia ramani ya jengo la Makao Makuu ya Mamlaka ya Udhibiti wa. Huduma za Nishati na Maji (EWURA) wakati alipotembelea maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani akiangalia ramani ya jengo la Makao Makuu ya Mamlaka ya Udhibiti wa. Huduma za Nishati na Maji (EWURA) wakati alipotembelea maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo.
Jengo la Makao Makuu ya Mamlaka ya Udhibiti wa. Huduma za Nishati na Maji (EWURA) likiwa limeanza kuinuka kuelekea ghorofa ya kwanza.
Mmoja wa wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa Ewura, Hassan Bendera akiwaelekeza jambo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Sophia Kongela  na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani,
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula ameendelea kufurahishwa na maendeleo mapya na hatua zinazopigwa kila kukicha katika ujenzi wa ofisi za wizara katika mji wa serikali ya Mtumba mkoani Dodoma unaojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Dk Mabula alitoa kauli hiyo leo tarehe 28 Januari 2019 wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa ofisi za Serikali katika mji wa Mtumba mkoani Dodoma unaojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambalo liko chini ya Wizara yake.
Alisema kazi inayofanywa na shirika la Nyumba la Taifa kujenga ofisi za Serikali katika mji huo kwa sasa unaenda kwa kasi na unatia moyo kwani kila kukicha kila mhandisi anayesimamia mradi anakuwa anafanya ubinifu wake ambao ni tofaujti na wamwingine na hivyo kuchagiza maendeleo ya ujenzi wa majengo hayo.
Katika mradi huo Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kupitia kampuni yake ya ujenzi inajenga ofisi za Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Nishati pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara.
Aidha, Dk Mabula amefurahishwa na ufuatialiaji wa ujenzi wa ofisi hizo unaofanywa na Wizara ya Fedha pamoja na Viwanda na Biashara na kueleza kuwa hatua hiyo inalifanya Shirika hilo kufanya kazi kulingana na mahitaji ya wateja wake.

Comments