Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akikaribishwa kwenya Shirika la Nyumba la Taifa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Feix Manyama Maagi muda mfupi baada ya kuwasili makao makuu ya Shirika na kufanya ziara kufuatilia utendaji wa Shirika hilo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akizungumza na menejimenti ya NHC leo hii.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Operesheni za Mikoa, Suzane Kyaruzi wakati alipotembelea Shirika.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akizungumza na menejimenti ya NHC leo hii.
Waziri Lukuvi akiangalia namna ya utunzaji wa nyaraka za serikali kwenye mojawapo ya ofisi ya Shirika

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William
Vangimembe Lukuvi amewahakikishia Watanzania kuwa Shirika la Nyumba la Taifa liko
imara kwaajili ya kutekeleza malengo lililopangiwa na serikali
Waziri Lukuvi ameyasema hayo leo wakati alipotembelea Shirika
la Nyumba la Taifa kujionea utendaji kazi na kuwatakia heri na kuhimiza
utendaji kazi wenye tija kwa Shirika.
Aliwataka wafanyakazi wa Shirika kufanya kazi kwa juhudi kubwa
na maarifa huku akiwahakikishia kwamba Serikali ipo nyuma yao na ina matarajio
makubwa ya kuhakikisha Wafanyakazi hao wanatimiza malengo ya Serikali ya
kujenga nyumba 50,000 kwaajili ya Watanzania.
“Shirika la Nyumba lipo, lilikuwapo, litaendelea kuwapo kwasababu
Serikali ipo, nyinyi endeleeni kuchapa kazi kwa bidii, tunawategemeeni
muendelee kuhakikisha Shirika linabaki salama. Mambo mengine yanayotuhusu
Serikali tuachieni sisi, siyo ya kwenu,” amesema.
Alitaka kila mfanyakazi atekeleze majukumu yake kwa tija ili
Serikali iendelee kuvuna faida na kupata matokeo chanya ambayo yatafaidisha
Watanzania wengi zaidi.
Alisema Shirika la Nyumba linaaminika na lina uwezo wa
kutekeleza majukumu yake kama kawaida na kutaka miradi yote iliyoanza kujengwa
ikamilishwe kwa wakati ili kusudi shughuli ya kuianza miradi mingine mingi
zaidi ifanyike.
Waziri Lukuvi amehimiza jitihada ziongezeke katika ubunifu wa
nyumba za gharama nafuu, ili nyumba zinazojengwa ili ziwe za gharama nafuu
kweli.” Nyinyi ndiyo Champion wa kusimamia ujenzi wa nyumba za gharama nafuu hatutarajii
Watanzania wakalalamikia nyumba zenu kuwa za bei juu.”
“Ni kweli mmejenga nyumba nyingi sana pale Iyumbu, Rais
Magufuli amewasifieni sana na amefurahi, lakini suala linabaki hapa hoja siyo kujenga
nyumba nyingi bali ni kujenga nyumba nyingi za gharama nafuu ziwafikie na kumilikiwa
na Watanzania wengi zaidi,”amesema.
Comments