Monday, April 30, 2018

NHC YAFIKIA MAKUBALIANO NA HALMASHAURI YA MONDULI KUHUSU NYUMBA ZILIZOJENGWA MJINI HUMO

Shirika limefikia makubaliano na Halmashauri ya Monduli kuhusu nyumba tulizojengwa mjini Monduli. Katika makubaliano hayo yalioongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Hazina na Maendeleo ya Biashara, Ndugu William Genya, Baraza la Madiwani limeafiki kununua nyumba 10 zenye thamani ya Sh.1.1bn/- na kuruhusu Shirika kuuza nyumba 10 zilizobaki kwa watu wengine. Picha hapo inamwonyesha Mwenyekiti wa Halmashauri, Ndugu Isack J. Copriano akipeana mkono na Kaimu Mkurugenzi William Genya. Wanaoshuhudia ni baadhi ya madiwani pamoja na Meneja wa Mkoa wa Arusha, Ndugu Ladislaus Bamanyisa
Picha ya pamoja mbele ya nyumba mojawapo iliyokamilika tayari kwa kukabidhiwa kwa Halmashauri wakati wowote. Ujumbe wa Shirika ulimshirikisha pia Katibu wa Shirika, Ndugu Martin Mdoe (hayuko pichani).



Picha ya pamoja mbele ya nyumba mojawapo iliokamilika tayari kwa kukabidhiwa kwa Halmashauri wakati wo wote. Ujumbe wa Shirika ulimshirikisha pia Katibu wa Shirika, Ndugu Martin Mdoe (hayuko pichani).



Meneja wa Mkoa wa Arusha, Ndugu Ladislaus Bamanyisa akipeana mkono na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha, Isack Joseph (kulia) Wengine kwenye picha ni Pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Monduli,  Mama Rose Mhina na Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Arusha, Ladislaus Bamanyisa.

Kikao cha maamuzi kati Shirika na Baraza la madiwani kikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri. Karibu nae ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri, Mama Rose Mhina. Kushoto ni ujumbe wa Shirika ukiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Hazina na Maendeleo ya Biashara. Wengine ni Meneja wa Mkoa na Mwanasheria wa Shirrika, ndigu Martin Mdoe.

No comments: