Friday, July 21, 2006

Tumaini


Lecture Rooms Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa.

5 comments:

Christian Bwaya said...

Tanzania sasa, kama alivyosema waziri Msolwa imepiga hatua kwa idadi vya vyuo. Lakini suala linabaki pale kwenye za Bodi ya Mikopo. Hawa jamaa wa hapa, almanusura wapigwe nje ya kapu hilo. Nilisikia juzi juzi kwamba baadhi yao zaidi ya 200 hawatafanya mitihani! Sijui huko tuendako kama vyuo binafsi vitaendeka na watoto wa masikini walio wengi nchini kwetu.

mloyi said...

Chuo kizuri, kinatamanisha kusoma. Maendeleo kwa watanzania. tatizo ni jee, Watanzania wa kawaida wataweza kumudu gharama zake?. Kumbuka maneno ya Prof. Msolwa.

mzee wa mshitu said...

Ni kweli ndugu zangu Bwaya na Mloyi mmesema jambo muhimu sana, mimi nikiyaangalia majengo haya na hiyo future yetu naona sisi na hao wengine watoto wa wakulima hawatakuwa na fursa katika mahekalu kama haya. Haya yatakuwa maeneo ya matajiri. Chonde chonde Profesa Msola na Serikali yako msitutose watoto wa wenzenu.

Christian Bwaya said...

Nilikuwa nafikiri serikali inapomtaka mwanafunzi alipie 40% ya ada ya masomo inafikiri kitu gani? Hivi ni mzazi huyuhuyu aliyeshindwa kumalimalizia elfu 35,000 za sekondari ndiye tunayemtaka alipe hayo maelfu zaidi? Nini maana yake? Kwamba elimu, kama anavyosema Mloyi, "inatabakishwa" iwe ya wenye nacho, tusionacho tutajiju.

Nafikiri ni huu mtindo unaoendlea wa keki ya taifa kugawanywa kwa walioshikilia mipini ya visu. Nakumbuka sana makala yako ya Jumapili hii Charahani ulilizungumza ninagaubaga.

Swalio linakuwa: Nini kifanyike? Mwananchi wa kawaida afanyeje? Kijana anayenyimwa elimu hivi hivi huku akiona, afanyeje? Ajiunge na jeshi la mtaani?

mzee wa mshitu said...

yes Bwaya hili la kujiunga na jeshi la wananchi wa mtaani ndilo bila shala lililobakia hakua jinsi na tuombe mungu jeshi hili lisipate kamanda wa kuliongoza akipatikana tumekwisha.