Thursday, November 27, 2014

MHE. KAMANI AZINDUA MRADI WA UFUGAJI WA SAMAKI NDANI YA ZIWA VICTORIA


Mgeni Rasmi Waziri wa Maendeleao ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (MB) akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mradi wa Ufugaji wa Samaki ndani ya Ziwa Viktoria Kiteule cha Bulamba kwa kutumia teknolojia mpya ya vizimba (Cages). Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mhe.John Henjewele, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael M. Muhuga.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani akipandikiza vifaranga vya samaki ndani ya Ziwa Victoria, mradi unaotekelezwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Wilaya ya Bunda, Kiteule cha Bulamba kwa kutumia teknolojia mpya hapa nchini ya kuzalisha samaki kwenye vizimba.
Picha ya vizimba ambavyo ufugaji wa samaki umeanza mara baada ya Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kuzindua mradi huo na kupandikiza vifaranga vya samaki. Mradi unatekeleza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Wilaya ya Bunda, Kiteule cha Bulamba kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Economic Social Research Foundation (ESRF), Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Ufugaji wa samaki kwa kutumia teknolojia ya vizimba ndani ya Ziwa Victoria, umekuwa ukitekelezwa pia na wenzetu wa Kenya na Uganda ambao wamepiga hatua kubwa.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (mwenye Kaundasuti nyeusi) akionyesha umahiri wake wa kucheza ngoma ya asili mara baada ya uzinduzi wa mradi huo.
Mgeni Rasmi Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (wa tatu kushoto) pamoja na wageni wengine waliohudhuria Sherehe hizo. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Uchumi, Jeshi la Kujenga Taifa Kanali Felix Samilani, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Raphael M. Muhuga, Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mhe. John Henjewele, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara, na Mkuu wa Kiteule cha Bulamba Meja David Msakulo.
Mkuu wa Kiteule cha Bulamba, Meja David Msakulo akitoa neno kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja (JKT) Jenerali Raphael M. Muhuga ili azungumze na wananchi wa kijiji cha Bulamba.
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Mratibu Mwandamizi wa Mradi Bw. Nehemia Murusuri (wa kwanza kulia) pamoja na Mwakilishi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Mratibu wa Mradi wa Kuondoa Umaskini, Kukuza Uchumi na Utunzaji Endelevu wa Mazingira, Bw. Telesphory Kamugisha (wa pili kulia). Wengine ni baadhi ya wageni waliohudhuria sherehe hizo.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael M. Muhuga akiongea na wananchi wa Kijiji cha Bulamba wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Ufugaji wa samaki katika Ziwa Victoria kwa kutumia teknolojia ya vizimba (Cages) ambayo ni teknolojia mpya ndani ya nchi yetu.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani akitoa hotuba kwa wananchi wa kijiji cha Bulamba (hawapo pichani) mara baada ya kuzindua Mradi wa Ufugaji wa Samaki ndani ya Ziwa Viktoria. Aliwasisitiza wananchi kujiunga katika vikundi ili kujijengea uwezo wa kuanza kutumia teknolojia ya kisasa ya kuzalisha samaki kwa kutumia vizimba (Cages) katika ziwa Victoria.

Ripoti ya GAG kuhusu akauti ya ESCROW yawasilishwa Bungeni


Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali,Mhe Zitto Kabwe akiongozana na Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini,Mhe. Ismail Aden Rage wakati akiwasili bungeni kuwasilisha Ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (GAG) kuhusu akauti ya ESCROW.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Anne Makinda akifafanua jambo wakati akiendesha Bunge hilo jana mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Mhe Zitto Kabwe akienda kusoma Ripoti ya GAG kuhusu akauti ya ESCROW.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali Mhe Zitto Kabwe akisoma Ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (GAG) kuhusu akauti ya ESCROW Bungeni Mjini Dodoma jana.

Waheshimiwa Wabunge wakimsikiliza Mhe. Zitto Kabwe (hayupo pichani) wakati akisoma ripoti ya CAG.
Baadhi ya wahudumu wa Bunge wakigawa Ripoti ya GAG kuhusu akauti ya ESCROW kwa Wabunge
Waheshimiwa Wabunge wakipitia ripoti ya GAG kwa makini wakati ikisomwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Mhe Zitto Kabwe.
Baadhi ya waandishi wanaoripoti habari za Bunge wakifuatilia mjadala kwa makini.
Naibu katibu wa Bunge, John Joel akijadiliana jambo na Mhe. Spika Anna Makinda.
Wabunge wakiwa wamesimama kuashiria kuunga mkono taarifa iliyosomwa Bungeni leo na Mhe. Zitto Kabwe.
Mhe Said Arfi akimpongeza Mhe.Zitto Kabwe ,mara Baada ya kumaliza kusoma ripoti ya GAG.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali,Mhe DEO Filikunjombe akiwasilisha maazimio ya kamati yake.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Anne Makinda akitoka ndani ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya kuahirisha Bunge mpaka leo ambapo Serikali inatarajiwa kutoa majibu.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mhe. Stephen Masele akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Bunge kuahirishwa. Picha zote na Deusdedit Moshi wa Globu ya Jamii kanda ya kati

BILIONEA DANGOTE AKAGUA TENA UJENZI WA KIWANDA CHAKE CHA SARUJI MTWARA


 Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Industries Group), mfanyabiashara maarufu Afrika, Alhaji Aliko Dangote akitumia gari kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda chake kikubwa cha saruji katika Kijiji cha Msijute, mkoani Mtwara.
 Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Industries Group), mfanyabiashara maarufu Afrika, Alhaji Aliko Dangote (kushoto) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Dangote nchini, Esther Baruti kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara .
 Ndege ya bilionea huyo wa Afrika, Alhaji Dangote ikitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara
 Alhaji Aliko Dangote kutoka Nigeria, akilakiwa na Mwakilishi Mkazi wa Dangote nchini, Esther Baruti alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara leo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Balozi wa Nigeria nchini, Dk. Ishaya Manjanbu akimlaki Alhaji Dangote.
 Dangote akiwa na Mwakilishi Mkazi wa Kampuni yake hapa nchini, Esther Baruti

Dangote akikaribishwa na viongozi wa kampuni ya Dil & Sinoma alipowasili eneo la Kiwanda cha simenti cha Dangote.
 Alhaji Dangote akiwa na maofisa wake  katika kikao na viongozi wa kampuni inayojenga kiwanda hicho ya Dil & Sinoma kwa ajili ya kupewa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho ambacho kitakuwa cha tatu kwa ukubwa Afrika.



 Waandishi wa habari wakimhoji Dangote kuhusu maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho
                                                                      Alhaji Aliko Dangote
 Alhaji Dangote akiwa kwenye msafara wa magari akikagua maendeleo ya ujenzi ya kiwanda cha saruji Mtwara





 Mwakilishi Mkazi wa Kampuni hiyo ya Dangote hapa nchini, Esther Baruti akiwa na mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni ya Dangote
 Alhaji Dangote akisindikizwa kwenda kupanda ndege kwenda nchini Ethiopia kuendelea na ziara yake
 Ofisa Mnadhimu wa Poilisi Mkoa wa Mtwara, George Salala akiagana na Alhaji Dangote
 Alhaji Dangote akipanda ndege tayari kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara
 Mwakilishi Mkazi wa Dangote hapa nchini, Esther Baruti akiondoka baada ya kuagana na Dangote
Ndege iliyombeba Alhaji Dangote ikipaa

NAIBU WAZIRI SALOME AKUTANA NA KAMPUNI ZA CHINA KUJADILI UWEKEZAJI KATIKA MAFUTA, GESI ASILIA NA NISHATI JADIDIFU

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa kampuni mbili kutoka China kwa lengo la kujadil...