Wednesday, December 02, 2015

WAZIRI MKUU AAGANA NA BALOZI MPANGO WA DRC

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo nchini, Mhe. Juma - Alfani Mpango   ambaye alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 2, 2015.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya kinyago Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo  nchini, Mhe. Juma-Alfani Mpango ambaye alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 2, 2015 kuaga.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mhe.  Juma- Alfani  Mpango  ambaye alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 2, 2015 kuaga.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambaye anamaliza muda wake, Bw. Juma-Alfani Mpango.

Akizungumza na balozi Mpango leo (Jumatano, Desemba 2, 2015), ofisini kwake, Magogoni jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu alimshukuru balozi huyo kwa pongezi zake na kumuomba aendelee kuwa balozi mzuri wa kuitangaza Tanzania hata baada ya kurejea nyumbani.

Pia alitumia fursa hiyo kuwaombea heri wananchi wa DRC pamoja na Rais Joseph Kabila katika maandalizi ya uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika nchini humo mwakani.

Kwa upande wake, Balozi Mpango ambaye alisema amekaa hapa nchini kwa miaka 12, alimweleza Waziri Mkuu kwamba amejifunza mengi sana kutoka kwa viongozi wa Tanzania kubwa vikiwa ni uchapakazi na unyenyekevu. “Nimeona utawala wa Rais Benjamin Mkapa, Rais Jakaya Kikwete na sasa Dkt. John Pombe Magufuli. Ninavutiwa na hatua mnazochukua hivi sasa katika kupambana na rushwa na ufisadi,” alisema.

“Mambo niliyojifunza tangu nimekaa hapa ni uchapakazi na unyenyekevu. Unaona kabisa kwamba mtu anaamini kuwa madaraka siyo kitu cha kujivunia kwa mtumishi wa umma. Anachotakiwa kuwa nacho ni utayari wa kuwatumikia wananchi,” alisema kwa Kiswahili sanifu.

Balozi Mpango aliomba mahusiano ya nchi hizi mbili yaendelezwe kwani DRC imekuwa ikinufaika na matumizi ya bandari ya Dar es Salaam katika kusafirishia bidhaa zake kwenda nchi za nje.

“Bandari ya Dar es Salaam ni muhimu sana kwetu. Mwaka 2004 tulisafirisha tani za mizigo 200,000, mwaka 2014 ziliongezeka na kufikia tani milioni 1.3; na mwakani tunataraji zitaongezeka na kufikia tani milioni tatu,” alisema.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMATANO, DESEMBA 2, 2015.

HUDUMA ISIYOKUWA NA USUMBUFU YA MAWASILIANO YAZINDULIWA

          Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa huduma mpya inayojulikana kama Vodacom Red jijini Dar es Salaam leo.

 Ni  huduma ya Vodacom Red
 Inayotoa ofa nafuu na maalumu kwa wateja.

KAMPUNI ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania leo imezindua huduma mpya inayojulikana kama Vodacom Red ambayo imewalenga wateja wake wote wanaonunua muda wa maongezi kabla ya kupata huduma za mawasiliano ambayo ni bora zaidi,ina unafuu wa gharama na yenye kuwarahishia maisha.

Akiongea wakati wa uzinduzi jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao amesema“Vodacom tumebuni huduma tukiwa tumewalenga wateja wetu wote hasa wale wenye shughuli nyingi ambao wanakosa  muda wa kununua vifurushi vya muda wa maongezi vya siku,wiki na vya mwezi.

Huduma ya Vodacom Red itawapatia unafuu wa kupiga simu kwa mitandao yote kwa gharama ya shilingi 1.5 kwa sekunde na kwa gharama hiyo hiyo ya shilingi 1.5 kwa sekunde watawezeshwa kupiga simu katika nchi tano kubwa zenye mtandao mkubwa wa masuala ya biashara ambazo ni (China,Afrika ya Kusini,India,Canada na Marekani),Kuhusiana na  matumizi ya data alisema wateja watakaotumia huduma hii watapatiwa kifurushi chenye unafuu kitakachowawezesha kupata huduma za intaneti yenye  kukidhi mahitaji yao”.

Kampeni hii inawarahisishia maisha watumiaji wake  kwa kutoa ofa  kwa watumiaji ambapo watafanya mawasiliano  kwa  kupiga simu  za ndani kwa malipo nafuu ya shilingi 1.5 kwa sekunde kwa mitandao yote pia kwa gharama hiyo hiyo ya shilingi 1.5 wanaweza kupiga simu kwenda nje ya nchi zipatazo 5 pia wanaunganishwa na huduma ya intaneti ya Mpango Mzima ambayo ina kasi kubwa na inawawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi  kwa muda wote.Katika kusherehekea uzinduzi wa huduma hii wateja watakaotumia shilingi 4,000/-na zaidi kwa kupiga simu za ndani watanufaika na mrejesho wa  asilimia 10% ya fedha hizo kupitia akaunti zao za M-Pesa kwenye simu zao.

Akiongelea mkakati wa Vodacom kuwaunganisha watanzania wote katika mtandao wa mawasiliano,Ferrao alisema “Lengo letu ni kuendelea kubuni huduma za kurahisisha mawasiliano kwa wateja wetu tukiwa na dhamira ya kuwapeleka katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia.Vodacom Red ni mfano wa huduma ambayo imebuniwa  ikiwa ina ufanisi kubwa katika masuala ya biashara na yenye kuleta unafuu wakati huohuo kuwarahisishia maisha  wateja wetu”.

Wateja wa Vodacom wanaotumia huduma ya kuongeza salio kwenye simu zao kabla ya maongezi  wanaweza kuchangamkia huduma mpya na yenye unafuu mkubwa wa gharama.Ili mteja aweze kunifaika na huduma hii anachotakiwa kufanya ni kupiga *149*73# hapo mteja utapata frusa ya kuchagua anachokitaka kupitia huduma ya Vodacom Red.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na
Rosalynn Mworia
Head: Corporate Communications and PR
Mobile: +255754710661
Email: rmworia@vodacom.co.tz.

JESHI LA POLISI LA KABIDHI JENGO LA KISASA LA MICHEZO YA TAEKWONDO JIJINI DAR

 Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini DIGP Abdulrahman Kaniki, akikata utepe kuashiria ufunguzi wa jengo la kisasa litakalo tumika kwa ajili ya shughuli za michezo ya Taekwondo, lililofadhiliwa na serikali ya Korea kupitia kwa balozi wake hapa nchini Mh. II Chung, jana katika Chuo cha Taaluma ya Polisi DPA jijini Dar es salaam.
Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini DIGP Abdulrahman Kaniki, akimkabidhi cheti Bw. Shinyoung Pyeon, wakati wa sherehe za kukabidhi jengo la kisasa la michezo ya Taekwondo lililofadhiliwa na serikali ya Korea kupitia kwa balozi wake hapa nchini Mh. II Chung, jana katika Chuo cha Taaluma ya Polisi DPA jijini Dar es salaam.

 Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini DIGP Abdulrahman Kaniki, akiwa katika picha ya pamoja na timu ya taekwondo, mara baada ya ufunguzi wa jengo la michezo lililofadhiliwa na serikali ya Korea, kupitia kwa balozi wake hapa nchini Mh. II Chung. jana katika Chuo cha Taaluma ya Polisi DPA jijini Dar es salaam.

UJENZI WA BARABARA YA MOROCO -MWENGE WAANZA

MOR1
MOR2Afisa Habari Mkuu kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Aisha Malima akipata maelekezo kutoka kwa mfanyakazi wa Kampuni ya Ujenzi ya Estim bw. Joseph Shauri kuhusu ujenzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco.
MOR3Vifusi vikiwa vimekusanywa katika maeneo ya Mwenge ikiwa ni hatua za awali za ujenzi wa Barabara ya kutoka Mwenge hadi Morocco kazi iliyoanza Desemba Mosi, mwaka huu na inatarajiwa kuisha baada ya miezi sita chini ya Kampuni ya Ujenzi ya Estim jijini Dar es Salaam.
MOR4Afisa Habari Mkuu kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Aisha Malima akionesha alama zilizowekwa katika maeneo ya Bamaga ikiashiria kuwa tayari ujenzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco imeshaanza kufanya kazi tangu Desemba Mosi, mwaka huu na inatarajiwa kuisha baada ya miezi sita.
MOR5Afisa Habari Mkuu kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Aisha Malima akiongea na mmoja wa wachuuzi wa vyungu vya maua maeneo ya Bamaga Bw.Emmanuel Kilua ambaye tayari ameshapewa maelekezo ya kupisha eneo hilo ili kupisha ujenzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco inayojengwa na Kampuni ya Ujenzi ya Estim na inatarajiwa kuisha baada ya miezi sita.
MOR6Vifusi vikiwa vimekusanywa katika maeneo ya Mwenge ikiwa ni hatua za awali za ujenzi wa Barabara ya kutoka Mwenge hadi Morocco kazi iliyoanza Desemba Mosi, mwaka huu na inatarajiwa kuisha baada ya miezi sita chini ya Kampuni ya Ujenzi ya Estim jijini Dar es Salaam.
MOR7Mafundi wakiendelea na harakati za ujenzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco ikiwa ni moja ya hatua ya upanuzi wa barabara hiyo kutoka njia mbili hadi kuwa barabara ya njia tano lengo ni kupunguza msongamano wa foleni.
MOR9Barabara ya Mwenge hadi Morroco inavyoonekana katika picha kwa sasa ambayo inatarajiwa kuwa barabara ya nia tano badala mbili kama ilivyo sasa lengo ikiwa ni kupunguza msongamano wa foleni kwa watumiaji wa barabara hiyo. (Picha na Lorietha Laurence –Maelezo)

TASNIA YA FILAMU NCHINI YACHANGIA KUTOA AJIRA NA KUONGEZA PATO LA TAIFA

fl1Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo akielezea namna sekta ya Filamu ilivyo piga hatua hapa nchini wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Genofeva Matemu na kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari MAELEZO Bi. Fatma Salum.
fl2: Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutana wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo uliokuwa unahusu ukuaji wa sekta ya Filamu Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Frank Shija, WHVUM
……………………………………………………………………………………………
Na Jovina Bujulu-MAELEZO
Sekta ya filamu imekuwa na mchango mkubwa kwa kutoa jumla ya ajira 732,681ikiwa ni mchango wake katika kutatua tatizo la ajira nchini kwa mwaka wa fedha 2014/2015.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Joyce Fissoo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Fissoo alifafanua kuwa idadi hiyo ya ajira zilizotolewa inajumuisha wataalamu wa filamu 944 na wadau wengine wasio wataalamu 731,737 ikilinganishwa na takwimu zilizotolewa na Shirika la Milki Bunifu Ulimwengini liliripoti kuwa mwaka 2007 tasnia ya filamu iliajiri watu 36.
‘Katika kipindi cha miaka ya 2000 utengenezaji wa filamu umebadilika kutoka ule wa awali wa kuburudisha na kuelimisha na kuwa biashara inayoingiza kipato na kutoa ajira katika jamii hivyo kuongeza kipato cha Taifa letu”. Alisema Fissoo
Aidha, kuanzia miaka ya 2000 sekta binafsi ilianza kutengeneza filamu hivyo filamu zilianza kufadhiliwa, kutengenezwa, kumilikiwa na kusambazwa kwa kiasi kikubwa na wadau na makampuni binafsi hivyo kupelekea ongezeko kubwa la makampuni ya uzalishaji na usambazaji kutoka kampuni 1 miaka ya 2000 hadi kufikia makampuni 250 mwaka 2015.
Tasnia hiyo imechangia kukuza uchumi wa nchi na ule wa mtu binafsi ambapo kwa mujibu wa Shirika la Milki Bunifu Ulimwenguni (WIPO) kwa mwaka wa 2007 ilichangia shilingi 2,134,860 na kufikia mwaka 2010 ilichangia shilingi 11,398,440, ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 433.9.
Akizungumzia ukuaji huo wa tasnia ya filamu, Fissoo alisema kuwa ukuaji wa teknolojia umepelekea utumiaji wa vifaa vyenye teknolojia ya hali ya juu vilivyowekezwa na baadhi ya wadau vinavyopatikana kirahisi kama vile kamera za kisasa, na mashine za kufungashia kazi za filamu hivyo kupunguza gharama za uzalishaji wa filamu nchini.
Aidha, kumekua na uuzaji wa filamu kwa njia ya mtandao suala linalopanua wigo wa masoko na kuitangaza nchi kwa wepesi zaidi hivyo kupelekea umahususi wa mandhari ya Tanzania kutumika na watengenezaji wa ndani na makampuni ya nje yapatayo 169 kutengeneza filamu mbalimbali.
Tasnia ya filamu nchini imeendelea kukua na kushamiri kwa kushirikiana na Washirika wa Maendeleo na wadau wa ndani ya nchi ikiwemo kuandaa, kuratibu  na kuendesha matamasha na Tuzo za Filamu za Tanzania (TAFA),Tamasha la Filamu la Bara la Ulaya, Tamasha la Filamu la Misri, Tamasha la Filamu la India, Tamasha la Filamu la Bara la Asia, Tamasha la Filamu la Brazil na Arusha African Film Festival.

MHE. NDUGAI AKUTANA NA MKURUGENZI MKAZI WA TAASISI YA KIMATAIFA INAYOJISHUGHULISHA NA MASUALA YA KIDEMOKRASIA NA UTAWALA BORA (THE INTERNATIONAL REPUBLICAN INSTITUTE).

ga1Mkurugenzii Mkazi wa Taasisi ya kimataifa inayojishughulisha na masuala ya kidemokrasia na utawala bora (The international Republican Institute) Bi. Robina Namusisi akisalimiana na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai alipomtembea Ofisini kwake Dar es Salaam leo kuelezea mipango ya taasisi yake inayokusudia kushirikiliana na Bunge katika kutoa mafunzo ya kidemokrasia kwa Wabunge vijana na wanawake.
ga2Mkurugenzii Mkazi wa Taasisi ya kimataifa inayojishughulisha na masuala ya kidemokrasia na utawala bora (The international Republican Institute) Bi. Robina Namusisi akimweleza Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai mipango ya taasisi yake inayokusudia kushirikiliana na Bunge katika kutoa mafunzo ya kidemokrasia kwa Wabunge vijana na wanawake. Bi. Namusisi alimtembea Mhe. Ndugai Ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.
ga3Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na Mkurugenzii Mkazi wa Taasisi ya kimataifa inayojishughulisha na masuala ya kidemokrasia na utawala bora (The international Republican Institute) Bi. Robina Namusisi alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.  Taasisi hiyo inayokusudia kushirikiliana na Bunge katika kutoa mafunzo ya kidemokrasia kwa Wabunge vijana na wanawake.
ga4Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya kimataifa inayojishughulisha na masuala ya kidemokrasia na utawala bora (The international Republican Institute) Bi. Robina Namusisi (kulia kwake)alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.  Taasisi hiyo inayokusudia kushirikiliana na Bunge katika kutoa mafunzo ya kidemokrasia kwa Wabunge vijana na wanawake.  Wengine katika picha ni maafisa kutoka taasisi hiyo.
Picha na Hassan Silayo, Idara ya Habari Maelezo.

WACHINA WAONYESHA UTAMADUNI WAO TANZANIA

ci1Kikundi cha wanamuziki kutoka China kikitumbuhiza wakati wa Tamasha la Forbidden City Chamber Orchestra lililofanyika katika ukumbi wa maonyesho wa Makumbusho ya Taifa jana jijini Dar es Salaam.Tamasha hilo lilikuwa maalumu kufuatia kuzinduliwa rasmi kwa Kituo cha Utamaduni wa China hapa nchini.
ci2Msanii wa kundi la Zijincheng kutoka Chuo Kikuu cha Sanaa cha China Di Yang akionyesha umahiri wa kutumia vifaa vya muziki wakati wa Tamasha la Forbidden City Chamber Orchestra lililofanyika katika ukumbi wa maonyesho wa Makumbusho ya Taifa jana jijini Dar es Salaam.Tamasha hilo lilikuwa maalumu kufuatia kuzinduliwa rasmi kwa Kituo cha Utamaduni wa watu wa China hapa nchini.
ci3Msanii wa kundi la Zijincheng kutoka Chuo Kikuu cha Sanaa cha China Yang Jing akionyesha umahiri wa kutumia vifaa vya muziki wakati wa Tamasha la Forbidden City Chamber Orchestra lililofanyika katika ukumbi wa maonyesho wa Makumbusho ya Taifa jana jijini Dar es Salaam.Tamasha hilo lilikuwa maalumu kufuatia kuzinduliwa rasmi kwa Kituo cha Utamaduni wa watu wa China hapa nchini.
ci4Mkuu wa Kituo cha Utamaduni wa Watu wa China nchini Tanzania Bw. Gao Wei (watano kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wanamuziki wa kundi la Zijincheng kutoka Chuo Kikuu cha Sanaa cha China. Kundi hilo linaundwa na wanazuoni na watafiti wa muziki wa asili nchini China.
Picha na Frank Shija, WHVUM
…………………………………………………………………………..
Na Jacquiline Mrisho
Maonesho ya utamaduni wa watu wa China yalifanyika jana usiku maeneo ya Makumbusho ya TaifaJijini Dar es salaam baada ya ufunguzi rasmi wa Kituo cha Utamaduni wa watu wa China uliofanyika mchana.
Maonesho hayo yalifunguliwa na Mkurugenzi wa kituo hicho cha Utamaduni wa watu wa ChinaTanzania Bwana GAO Wei ambapo alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wageni waalikwakuangalia utamaduni wa wachina kupitia muziki wao.
Hafla hiyo ilipambwa na wanamuziki mahiri wa kundi la watafiti wa muziki wa asili linaloitwa Zijincheng kutoka Chuo Kikuu cha Sanaa cha China kilichopo Beijing. 
Wanamuziki hao walianza kwa kupiga vyombo vyao vya muziki kwa pamoja bila kuimbachochote na baadae kila mmoja wa wanamuziki hao alipiga chombo kimoja cha muziki ilikuwaonyesha wageni waalikwa sauti na mdundo wa kila chombo cha muziki.
Mwishoni walipiga vyombo vyao kwa pamoja kwa kupiga mapigo ya wimbo wenye asili yakitanzania unaoitwa ‘Malaika Nakupenda’.
Kituo cha Utamaduni wa China nchini Tanzania ndio kituo cha kwanza kufunguliwa kwa Afrika Mashariki. Kimefunguliwa rasmi jana saa nne kamili asubuhi.Kituo hicho kipo Barabara ya Hassan Mwinyi maeneo ya Upanga Jijini Dar es Salaam.

MAKATIBU WAKUU WAKAGUA AICC MAANDALIZI YA MWISHO MKUTANO WA IPU, ARUSHA

Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali pamoja na Kamati ya Wataalamu ya Maandalizi ya Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), wamefan...