Friday, October 08, 2010

Redet: Kikwete aongoza kura za maoni


MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete amewaacha mbali wapinzani wake kwenye kinyang'anyiro hicho baada ya kupata asilimia 71.2 ya kura za maoni katika utafiti uliofanywa na Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia (Redet).

Matokeo hayo yamekuja katika kipindi ambacho kuna mzozo mkubwa baina ya taasisi nyingine inayofanya utafiti wa masuala ya kijamii, kisiasa na kiuchumi ya Synovate na Chadema ambayo inadai kuwa mgombea wake wa urais, Dk Willibrod Slaa aliongoza kwenye kura ya maoni iliyofanywa na taasisi hiyo.

Synovate imekana kufanya utafiti wa aina hiyo na kwamba hadi sasa imefanya utafiti kuhusu mwenendo wa vyombo vya habari katika kuripoti habari za uchaguzi mkuu, lakini Chadema imesema inao ushahidi kuwa taasisi hiyo iliendesha utafiti ulioonyesha kuwa Dk Slaa alipata asilimia 45 dhidi ya 40 za Kikwete.

Jana, Redet ilitangaza matokeo ya utafiti wake ambayo yanaonyesha kuwa Kikwete bado anaongoza, licha ya umaarufu wake kushuka kwa asilimia chache.

"Tukianzia uchaguzi wa rais wa Serikali ya Muungano, asilimia 71.2 ya wahojiwa wote walisema watamchagua mgombea urais wa CCM. Ilifuatiwa na Chadema ambayo asilima 12.3 walisema watamchagua mgombea wa Chadema na asilimia 10.1walisema watamchagua mgombea wa Cuf," alisema Dk Benson Bana ambaye ni mwenyekiti mwenza wa mpango huo.
Hata hivyo Kikwete anaonekana kupata kura nyingi zaidi kuliko asilimia za kura za wabunge ambazo ni 66.7 zikipungua kwa asilimia 4.5 kwa kulinganishwa na za kura za urais, huku madiwani wakipata asilimia 66.

Kwa mujibu wa Redet, matokeo yangekuwa hivyo iwapo uchaguzi mkuu ungefanyika kati ya Septemba 20 hadi 28 mwaka huu.

Akitoa matokeo ya utafiti huo wa 17 uliofanyika katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara na Visiwani katika kipindi hicho cha Septemba, Dk Bana alisema jana kuwa waliohojiwa walitakiwa kutoa maoni kuhusu uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani.

Alisema katika utafiti huo wahojiwa waliulizwa: "Mwezi Oktoba mwaka huu utafanyika uchaguzi mkuu.
Kama uchaguzi huo ungefanyika leo, je wewe ungemchagua mgombea wa chama gani?"
Alifafanua kuwa kutokana na swali hilo vyama vitatu vya CCM, CUF, Chadema vilipata alama nyingi kwa wagombea wake wa urais, wabunge na madiwani.

Hata hivyo, Dk Bana alisema kiwango cha asilimia za kura kimepungua kwa mgombea wa CCM kulinganisha na utafiti uliofanywa na Redet mwezi Machi wakati matokeo yalipoonyesha kuwa asilimia 77.2 wangemchagua mgombea urais wa CCM na tofauti na asilimia 71.2 alizopata safari hii.

"Itakumbukwa kwamba matokeo ya utafiti wa Redet wa hapo Machi mwaka 2010 yalionyesha wengi wangemchagua mgombea urais wa CCM asilimia 77.2. Katika utafiti CCM bado inaongoza, hata hivyo kiwango cha asilimia kimepungua," alisema Dk Bana.

Dk Bana alisema utafiti huo wa Redet ulifanywa kwa kuwahoji watu 2,600 katika wilaya 52 na kwamba watu 1,849 ndio waliosema watamchagua mgombea wa CCM, 263 wa CUF na 319 mgombea wa Chadema.
Ikilinganisha na utafiti wake wa mwezi Machi mwaka huu, Redet ilisema kuwa katika kipindi cha miezi sita kilichopita, idadi ya watu ambao wangemchagua mgombea wa Chadema imeongezeka kwa asilimia nane (8) kutoka 4.2 za mwezi Machi hadi 12.3.

Redet ilitaja pia kuongezeka kwa asilimia 0.9 kwa kura za urais wa CUF, asilimia 02 kwa TLP na 0.1 kwa NCCR-Mageuzi huku ikitaja sababu kuwa ni kampeni za uchaguzi zinazoendelea.

Lakini, taasisi hiyo ilisema mgombea urais wa CCM anaongoza kwa kutajwa jina lake kama mtu ambaye wangependa awe rais wa Tanzania na asilimia 68.5 ya wahojiwa wote akifuatiwa na Dk Slaa wa Chadema aliye na asilimia 11.9 huku Profesa Lipumba wa CUF akiwa wa tatu kwa asilimia 9.3 ya wahojiwa.


Dk Slaa
Taasisi hiyo ya utafiti wa kitaalam ilisema kuwa katika kura za urais, CCM itapata kura kidogo zaidi katika Jimbo la Kigoma Vijijini ambako atapata asilimia 28 huku Jimbo la Nkasi akipata asilimia zote 100.

Kwa mujibu wa utafiti huo kwa upande wa wabunge wa Jamhuri ya Muungano, pia asilimia ya watakaochagua mgombea wa CCM imepungua kwa asilimia 1.3, huku ikiongezeka kwa vyama vya upinzani, vikiongozwa na Chadema ambayo imeongezeka kwa asilimia 2.9, CUF 1.5, TLP na NCCR-Mageuzi asilimia 0.8 kila kimoja.

Kwa mujibu ya Dk Bana asilimia 66.7 ya waliohojiwa walisema watamchagua mgombea wa CCM huku asilimia 11.7 wakitaja mgombea wa CUF na asilimia 11.5 wa Chadema huku vyama vingine vikitajwa na idadi ndogo ya wahojiwa katika nafasi hiyo na ile ya urais.

Utafiti huo unaonyesha kuwa TLP katika urais itapata asilimia 0.4 na ubunge asilimia moja wakati NCCR-Mageuzi ikipata 0.3 urais na 1.1 ubunge na UDP iliambulia sifuri.

Kwa mujibu wa Redet matokeo ya utafiti huo kwa nafasi za udiwani katika vyama hivyo yanakaribia kufanana na nafasi za ubunge na uraisi. habari imeandikwa na Exuper Kachenje na Zulfa Msuya: Source :MWANANCHI.

Wednesday, October 06, 2010

RAIS JAKAYA AMTEUA PROFESA WANGWE KUWA MWENYEKITI WA BODI



Benjamin Sawe

Maelezo

Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dk.Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Profesa Samwel Wangwe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Elimu Kibaha.
Taarifa iliyotumwa Kwa vyombo vya habari kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu na Serikali za Mitaa Bibi Maimuna Tarishi imesema Profesa Wangwe ameteuliwa kutokana na Sheria aliyopewa Rais Kikwete katika Sheria ya Mashirika ya umma namba 17 ya mwaka 1969.
Sambamba na uteuzi wa Profesa Wangwe,Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda pia amewateua Wakurugenzi wa Bodi ya Shirika la Elimu Kibaha.
Kutokana na Mamlaka aliyopewa Waziri Mkuu katika Sheria ya Umma namba 17 ya mwaka 1969 wakurugenzi wa bodi walioteuliwa ni pamoja na Bibi Fatma Kiongosya ambaye ni Mwakilishi wa Wizara ya Afya na Uchumi,Dr Magreth Mhando,Mwakilishi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Wengine ni Bibi Salock Musese kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Bwana Apenda William Mrinji,kutoka Wizara ya Kilimo,Chakula na Ushirika na Bibi Halima Kihemba ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kibaha.
Uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi pamoja na Wakurugenzi hao umeanza rasmi tarehe 1/9/2010 na itamaliza muda wake tarehe 31/08/2013

Tuesday, October 05, 2010

Siku wa waalimu duniani


Mwanafunzi wa shule ya msingi Samora mjini Songea mkoani Ruvuma akimkaribisha Rais Dk Jakaya Kikwete kwa saluti maalumu muda mfupi kabla ya Rais Kikwete kufungua rasmi jingo la Chama Cha waalimu mkoa wa Ruvuma leo asubuhi(picha na Freddy Maro)

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia baadhi ya watoto waliomlaki muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa songea ambapo alikuwa mgeni rasmi katika maadhimnisho ya sherehe ya siku ya mwalimu duniani.(Picha na Freddy Maro)

Serengeti yazindua kampeni ya saidia taifa stars ishinde leo jijini dar



Mgeni rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Muhammed Seif Khatib akibandika stika kwenye ramani ya Tanzania kuashiria kuwa kampeni kubwa ya kuhamasisha watanzania waweze kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu ya taifa katika mchezo wake muhimu dhidi ya timu ya timu ya Taifa ya Morocco hapo jumamosi,Oktoba 9 2010 imezinduliwa rasmi.kati ni Meneja Mkuu wa Uhusiano, mawasiliano na Jamii kutoka kampuni ya bia ya Serengeti Dada Teddy na Rais wa TFF, Leodga Tenga wakishuhudia tukio hilo mchana huu.

Sunday, October 03, 2010

Balozi Maajar akabidhi hati ya utambulisho kwa Obama


Balozi wa Tanzania nchini Marekani,Mwanaid Maajar akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Marekani, Barack Obama mara baada ya kupokea hati ya utambulisho wa Balozi wetu huyo nchini humo.

Friday, October 01, 2010

Dk Slaa afunika Songea


Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Songea na vitongoji vyake, wakati wa mkutano wake wa kampeni, kwenye Uwanja wa Majengo jana. (Picha na Joseph Senga)

Jk afunika Tabora


JK akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Igunga,Rostam Aziz katika uwanja wa SabaSaba mjini Igunga mchana huu.

Umati mkubwa ulijitokeza uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora kumsikiliza JK

MRADI WA TACTIC KUPUNGUZA MSONGAMANO WA MAGARI JIJINI MWANZA

  * Sekta ya uvuvi nayo yaguswa. Mwanza.  Ujenzi wa Barabara ya Buhongwa-Igoma yenye urefu wa Km 14 kwa kiwango cha lami inayojengwa katik...