Meneja mstaafu wa NHC, Mkoa wa Kilimanjaro Shehe Salum Kombo akifurahia zawadi ya gitaa aliliopewa katika sherehe ya kumuaga rasmi iliyofanyika ijumaa iliyopita mjini Moshi.
Kaimu Meneja NHC Mkoa wa Kilimanjaro Stanley Msofe akitoa neno katika sherehe ya kuwaaga wastaafu ndh Shehe Kombo na Margareth Kimario. Watumishi hawa walistaafu utumishi mwezi June na Julai mwaka huu.Kaimu Meneja wa NHC, Mkoa Kilimanjaro Stanely Msoffe akikabidhi zawadi ya Gitaa kwa Meneja mstaafu wa mkoa wa Kilimanjaro Shehe Salum Kombo.
Mhasibu wa mkoa Hellen Mosha akiserebuka na Meneja mstaafu Shehe Salum Kombo katika sherehe ya kuwaaga wastaafu iliyofanyika ktk ukumbi wa ofisi ya mkoa Kilimanjaro.
Kaimu Meneja wa Mkoa wa Kilimanjaro Stanely Msoffe akijiandaa kufungua shampen. Kulia kwake ni Fredrick Stephen Shoo ambae ni mume wa mstaafu Margareth Kimario na pia mtumishi wa NHC Arusha.Mstaafu Margareth Kimario akisindikizws na wafanyakazi wa Mkoa Kilimanjaro kwenda kupokea zawadi yake. Mama Shoo alipewa zawadi ya vyombo vya nyumbani na vitenge.
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa Kilimanjaro wakishiriki katika tukio hilo.
Baadhi ya watumishi wa Shirika la Nyumba la Taifa wakifurahia tukio la kuwaaga wastaafu. Tukio hili lilifanyika ktk ukumbi ulioko ofisi za mkoa.
Meneja mstaafu wa NHC Mkoa wa Kilimanjaro Shehe Salum Kombo akifurahia zawadi ya gitaa aliliopewa katika sherehe ya kumuaga rasmi iliyofanyika ijumaa iliyopita mjini Moshi.
Comments