Hivi tunachohitaji ni sifa tu kuitwa graduates au?

HAIWEZEKANI kupuuza jitihada zote za serikali inazofanya kuwezesha kuanzishwa kwa chuo kikuu kipya kitakachowezesha kuchukua wanachuo 40,000 huko Dodoma.

Haiwezekani pia kusema kuwa eti serikali haikufanya jambo la maana kuweza kufikia uamuzi huu mzito ilhali sekta ya elimu ya juu imekuwa ikididimia.

Pia haiwezekani kupuuza jitihada zingine zozote za kujaribu kuonyesha nia njema japo kwa kauli tu kuanzisha vyuo vikuu vingi kadri inavyowezekana.

Lakini inawezekana kuhoji na vile vile kuwa na mashaka mengi hasa kama uamuzi huu unakuja wakati kile tulicho nacho kinatushinda na tena kinakaribia kutushinda kabisa.
Unaweza kusoma zaidi kwa kubonya hapa

Comments

MTANZANIA. said…
Cherehani!
Binafsi sipendi taifa liwe na wahatimu kwa jina tu bali uwezo wa kufikiri na kutenda kwa ajili ya mustakabali wa taifa letu.

Suala la muhadhiri mmoja kufunza UDSM, MKWAWA na tena CHANG'OMBE ndio haswa linanichanganya. Hivi kweli huyu Dr/Prof ataifanya kazi yake kiufasaha? Hivi atapata muda wa kutosha kuzipitia kazi za wanafunzi wake? Hivi atapata muda wa kutosha kuonana na wanafunzi wake?

Nimeipenda mada yako kwani inatoa changamoto.
Ndesanjo Macha said…
Zamani tulikuwa tukisema kuwa elimu ni ufunguo wa maisha. Sidhani kama tunaweza kutumia kauli hii tena iwapo unakuwa na mfumo wa elimu (ujinga?) ambapo mhadhiri anafundisha UDSM, Mkwana, na Chang'ombe. Halafu bado anakuwa na kazi wanazoziita "consultancy" halafu anakuwa pia na NGO.
Anonymous said…
Hey very nice blog!

Also visit my web-site ... mobile website