Safari ni safari



Haya ndugu zangu hii safari kweli tutafika namna hii, hapa afadhali wengine wangekuwa hadi juu ya dereva.

Comments

boniphace said…
kaka hapa ni safari za minadani na tunatazama kama jambo la kawaida tu. Ikitokea ajali tunasoma mambo ya Mola. Mola hapendi tufe anataka sisi tutumie akili zetu kujitazama katika maisha.
Simon Kitururu said…
Sidhani hata siku moja watu wanaweza kujiamulia kusafiri hivi. Ni hali halisi inayofanya watu wafikie hatua hii katika usafiri. Chakusikitisha ni kwamba hata ajali ikitokea na wasafiri wote wakafariki, ni jambo la kawaida tu TZ.Baada ya wiki moja ajali husahaulika.Kuna sehemu nyingi tu TZ huu ndio usafiri uaminika. La sivyo inabidi utembee au utumie baiskeli kitu ambacho kinafanya safari iwe ndefu sana.
Ndesanjo Macha said…
Safari kweli ni safari. Ajali inapotokea kama alivyosema ndugu Simon tunasikitika siku mbili tatu, tunasahau badala ya kujiuliza tufanye nini, tutunge sera gani, tupitishe sheria gani ili kuzuia au kupunguza ajali. Lakini katika mazingira ambayo askari wa usalama barabarani ni "watoza kodi" kama alivyokuwa akisema Fela Kuti, tunategemea nini?
MICHUZI BLOG said…
dah! hii kali. wapi hii?
Kaka Michuzi huku ni kilimanjaro jamaa walikuwa wanatoka bush wanakwenda zao town.
Yes Brother Ndesanjo kwa mtindo huu wa askari watoza kodi tutegemee balaa, matata na kila masikitiko.
Makene bila shaka unakumbuka hii kule Musoma ukiwa unaelekea Mkunjirwa sijui na wapi kule si unajua kaka.
Kitururu hapa kweli mambo magumu hakuna anayependa kujiamulia kusafiri hivi ni shida tu kaka.
Jeff Msangi said…
Naomba tuliondoe neno ajali kwenye mazungumzo pindi kitu kama hiki kikitokea.
Duh!Charahani kwa ridhaa yako nitaiweka hii picha kwenye blog yangu ya kizungu..sio kwa nia ya kukimbiza watalii ila kwa nia ya kupata maoni yao.