Monday, December 30, 2013

Rais wa Zanzibar Dr Ali Shein Azindua Rasmi Jengo jipya la Kiwanda cha Uchapaji Zanzibar na Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, huko Maruhubi Mjini Unguja


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akifungua pazia kuashiria ufunguzi rasmi wa Jengo jipya la Kiwanda cha Uchapaji Zanzibar na Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, huko Maruhubi Mjini Unguja, ikiwa ni katika shamra shamra za Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar,(kulia) ni Waziri Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed.
  Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Dr. Aboud Sheikh Rajab, akitoa maelezo kwa  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) alipotembelea jengo jipya la kiwanda cha uchapaji, Maruhubi jana,ikiwa ni shamra shamra za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akiuliza suala kwa Mkurugenzi Kanda wa Kampuni ya MFI DOCUMENT SOLUTION LTD, Rama Subramanian,ikiwa ndio wataalam wa mshine za uchapishaji,alipotembela  na kuona zinavyofanyakazi,wakati wa ufunguzi wa jengo jipya la kiwanda hicho,ikiwa ni shamra shamra za Miaka 50 ya Mapinduzi ya  Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Dr. Aboud Sheikh Rajab,kuhusu mashine mpya zilizonunuliwa na idara ya uchapaji,wakati alipotembelea kuangalia mashine kuona utendaji wake kazi,baada ya kufanya  unguzi rasmi,ikiwa ni shamra shamra za Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akipata maelezo kutoka kwa mtaalam wa mashine ya CTP,ambayo inatoa picha kwa kutumia Plat,Mohamed Abass Rajab,(wa tatu kushoto) wakati wa ufunguzi wa jengo jipya la kiwanda cha Uchapaji cha Zanzibar jana,ikiwa ni shamra shamra za Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu-Zanzibar

Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhani ametawazwa kuwa Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar

 Jaji Mkuu Mstaafu, Jaji Augustino Ramadhani akitoa mkate  kwa waumini wa Kanisa la Anglikana  baada ya kupewa Daraja la Ukasisi   katika Kanisa la Anglikana lililopo  Mkunazini mjini Zanziabar jana,pamoja na mambo mengine Jaji Augustino amewahi kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar na Tanzania, Brigedia Jenerali wa JWTZ pia amewahi kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania na Mahakama ya Afrika Mashariki. Picha na Sahim Shao 

UTENDAJI KAZI WA MBUNGE WA LUDEWA-CCM FILIKUNJOMBE WAWAVUTIA WAPIGA KURA WAKE,WAAMUA KUMBEBA MGONGONI

 Mbunge Filikunjombe kati  akipokea  zawadi ya  mbuzi  kutoka kwa  mkazi wa manda huku mkewe Habiba  akishukuru
 Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe akifurahia  baada ya  kupongezwa kwa  kubebwa mgongoni na mpiga kura wake
  Mbunge wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akiwa amebebwa na mpiga kura  wake kama  kumpongeza kwa utendaji wake mzuri
Wananchi  wa kata  ya Manda  Ludewa wakimfuta  jasho  mbunge  wao  Deo Filikunjombe kama  kumpongeza kwa utekelezaji  mzuri wa ahadi  na uwakilishi  uliotukuka bungeni .Picha Zote na Francis Godwin

Tuesday, December 24, 2013

UMEME BEI JUU JANUARI MOSI

Taarifa ya EWURA YA bei mpya za umeme zitakazoanza kutumika Januari, Mosi 2013
Tarehe 11 Oktoba 2013, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) liliwasilisha maombi ya kurekebisha bei ya umeme kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA). TANESCO ilipendekeza kuongeza bei kwa asilimia 67.87 kuanzia tarehe 1 Oktoba 2013, asilimia 12.74 kuanzia tarehe 1 Januari 2014 na asilimia 9.17 kuanzia tarehe 1 Januari 2015.



Vilevile TANESCO waliomba kuidhinishwa kwa kanuni ya kurekebisha bei ya umeme kulingana na mabadiliko ya bei za mafuta, mfumuko wa bei na mabadiliko ya thamani ya shilingi ya kitanzania. Aidha, TANESCO iliomba kuidhinishwa viwango vya gharama za kuunganisha umeme vinavyozingatia ruzuku inaliyotolewa na Serikali, na kuidhinishwa tozo mbalimbali kwa huduma zitolewazo na TANESCO.

Kwa mujibu wa TANESCO, kupitishwa kwa maombi haya kutaliwezesha Shirika (a) kupata fedha za uendeshaji na uwekezaji wa miundombinu, (b) kulifanya Shirika liweze kukopesheka na hivyo kuwezesha kupata mikopo yenye masharti nafuu, (c) kuliwezesha Shirika kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya umeme kwenye Gridi ya Taifa, na (d) kuongeza uwezo wa
kufanya matengenezo ya mara kwa mara ya miundombinu iliyopo ili kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa huduma za umeme wa uhakika kwa wateja.

Itakumbukwa kwamba bei za umeme zinazotumika hivi sasa ziliidhinishwa mwezi Januari 2012. Bei hizo zilipanda kwa asilimia 40.29 ikilinganishwa na maombi ya TANESCO ambapo ilipendekeza bei zipande kwa wastani wa asilimia 155. Sababu ilikuwa ni kuongezeka kwa gharama za uendeshaji kulikosababishwa na hali ya ukame katika maeneo yanayotiririsha maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme, toka mwaka 2011.

Hali hiyo ilipelekea TANESCO kulazimika kununua umeme kwa gharama kutoka kwa wazalishaji wa dharura (Emergency Power Producers). Hali ya maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme bado sio nzuri na hivyo TANESCO itaendelea kununua umeme kutoka kwa wazalishaji wa dharura (Emergency Power Producers).

USHIRIKISHWAJI WA WADAU

Kulingana na Kifungu Na. 19(2) (h) cha Sheria ya EWURA, Mamlaka ilifanya Taftishi ili kupata maoni juu ya ombi la kurekebisha bei za umeme. Ukusanyaji wa maoni ulihusisha pia mikutano minne (4) iliyofanyika Iringa na Shinyanga tarehe 15 Novemba 2013, Bagamoyo tarehe 20 Novemba na kuhitimishwa Dar es Salaam tarehe 22 Novemba 2013. Aidha, tarehe 6 Desemba 2013, EWURA iliitisha mkutano wa mwisho wa wadau wakiwemo wawakilishi kutoka Wizara ya Nishati na Madini(MEM), TANESCO, Shirika la Umeme la Zanzibar (ZECO), Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania, Baraza la Watumiaji na Baraza la Ushauri la Serikali, Umoja wa Wazalishaji wa Saruji wa Afrika Mashariki, na kiwanda cha ALAF. Katika mkutano huo EWURA iliwasilisha mwelekeo wa maamuzi kuhusu maombi ya TANESCO na namna zilivyokokotolewa. Wadau walipewa fursa ya kutoa maoni yao kuhusu mwelekeo wa bei na maoni yao yamezingatiwa katika kufikia maamuzi ya mwisho.

UCHAMBUZI NA UAMUZI

Kwa kufuata sheria na kanuni zinazoelekeza kuhusu uchambuzi wa bei ya umeme, EWURA ilifanya uchambuzi wa kifedha na kiufundi ili kubaini uwezo wa TANESCO katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku. Uchambuzi uliangalia utendaji wa Shirika la TANESCO katika miaka iliyopita na pia iliangalia majukumu yanayoikabili TANESCO katika miaka mitatu ijayo. EWURA imebaini kwamba hali ya kifedha ya Shirika la Umeme sio nzuri. Shirika limeendelea kupata hasara, ambayo iliongezeka kutoka shilingi bilioni 47.3 katika mwaka 2010 na kufikia shilingi bilioni 223.4 mwishoni mwa mwaka 2012. Pamoja na mapungufu ya kiufanisi, sababu kubwa ya ongezeko la hasara ni kuongezeka kwa gharama za uzalishaji wa umeme ambao TANESCO inanunua kutoka kwa wazalishaji binafsi. Hali hii imelifanya shirika kushindwa kulipa madeni yake ya muda mfupi na ya muda mrefu, ambayo yamelibikizwa na kufikia TZS 456.8 bilioni tarehe 22 Novemba 2013, hali ambayo inatishia uendelevu wa huduma ya umeme hapa nchini.

Mamlaka imetumia Kanuni ya Ukokotoaji wa Bei kama ilivyopendekezwa na AF-MERCADOS wakati wa kukokotoa mahitaji ya mapato ya TANESCO. Kanuni hiyo inawezesha kukokotoa bei zinazolandana na gharama halisi kwenye mfumo wa umeme na kuzigawa kwenye makundi ya watumiaji umeme, kadiri kila kundi linavyosababisha gharama kwenye mfumo wa umeme kwa mujibu wa mahitaji ya Sheria ya Umeme ya 2008 Kifungu cha 23(2)(f).

EWURA imejiridhisha kwamba, ufumbuzi wa matatizo ya kifedha ya TANESCO, unahitaji njia/mikakati miwili itekelezwe kwa pamoja:
kuongeza bei ya umeme ili kufikia bei inayokidhi gharama halisi (Cost Reflective Tariff); na
TANESCO kupata mkopo wa gharama nafuu ama ruzuku kutoka Serikalini ili kulipa limbikizo la madeni ya Shirika.

Bodi ya Wakurugenzi wa EWURA, katika kikao chake cha tarehe 10 Desemba 2013 pamoja na mambo mengine, ilitoa maamuzi ya ongezeko la bei za umeme kwa viwango mbalimbali kwa makundi mbalimbali ya wateja, kama ifuatavyo:

Kundi D1: Hili ni kundi la wateja wadogo wa majumbani, hasa vijijini, ambao hutumia wastani usiozidi wa Uniti 75 kwa mwezi. EWURA imeongeza wigo wa mahitaji ya umeme na kufikia uniti 75 kwa mwezi, lengo likiwa ni kuongeza idadi ya wateja wa TANESCO wanaoweza kulipa kidogo kwa matumizi ya umeme kwa kiwango hicho, na pia kuwahamasisha kutumie zaidi umeme. Awali kundi hili lilikuwa linatunia wastani wa matumizi ya uniti 50 kwa mwezi. Bei mpya ni shilingi 100 kwa uniti moja, kutoka shilingi 60 za sasa, sawa na ongezeko la shilingi 40.

Kundi T1: Hili ni kundi la watumiaji wakubwa wa umeme majumbani, biashara ndogondogo, mashine za kukoboa na kusaga nafaka, taa za barabarani, mabango n.k. Bei iliyoidhinishwa ni shilingi 306 kwa uniti moja, ikiwa ni ongezeko la Shilingi 85 ya bei ya sasa. TANESCO ilipendekeza ongezeko la shilingi 131.

Kundi T2: Hili ni kundi la watumiaji umeme wa kawaida ambao hupimwa katika msongo wa volti 400, na ambao matumizi yao ya wastani kwa mwezi ni zaidi ya uniti 7,500 wateja wafanyabiashara kubwa, viwanda vya kati. Bei ya nishati iliyoridhiwa ni shilingi 205 kwa uniti moja, sawa na ongezeko la shilingi 73 ya bei ya sasa. TANESCO walipendekeza ongezeko la shilingi 145 ya bei ya sasa.

Kundi T3-MV: Hili ni kundi la wateja wakubwa kama viwanda vikubwa waliounganishwa katika msongo wa kati (Medium Voltage). EWURA imeidhinisha bei ya nishati kwa kiwango cha shilingi 166 kwa uniti moja, sawa na ongezeko la shilingi 45 ya bei ya sasa. TANESCO walipendekeza ongezeko la shilingi 148 kwa uniti moja.

Kundi T3-HV: Hili ni kundi la wateja wakubwa waliounganishwa katika msongo wa juu (High Voltage – Voti 66,000 na zaidi) ikiwa ni pamoja na ZECO, Bulyanhulu, na Twiga Cement. Bei iliyoidhinishwa ni shilingi 159 kwa uniti moja, sawa na ongezeko la shilingi 53 la bei ya sasa. TANESCO waliomba ongezeko la shilingi 80 kwa uniti moja.

Bei ya umeme itakuwa inarekebishwa kila baada ya miezi mitatu kulingana na mabadiliko ya kiwango na bei za mafuta; mfumuko wa bei, mabadiliko ya thamani ya fedha, na upatikanaji wa ruzuku toka Serikalini.

Vilevile, TANESCO inatakiwa kutekeleza miradi ya uwekezaji iliyoainishwa kwa kutumia fedha zitakazokusanywa kutokana na bei zilizoidhinishwa. EWURA inaweza kurekebisha bei ya umeme ya TANESCO kila mwisho wa mwaka 2014 na/au mwaka 2015 endapo TANESCO itashindwa kutekeleza miradi iliyotajwa katika Jedwali husika. Marekebisho hayo yatatokana na makadirio ya gharama za miradi ambayo haikutekelezwa.

Kutokana na matazamio ya kuwa na mabadiliko makubwa katika uzalishaji wa umeme (generation mix) katika mwaka 2015 na kuendelea, kutokana na matarajio ya kuongezeka kwa kwa upatikanaji wa gesi asilia, EWURA itafanya utafiti kubaini gharama halisi (Cost of Service Study) ya huduma ya umeme kwa wakati huo. Hivyo, bei zilizoidhinishwa zitatumika mpaka mwaka 2016, kama utafiti unaotazamiwa kufanywa hautakamilika kabla ya mwisho wa mwaka 2015.

EWURA ililinganisha bei za umeme kwa kila Uniti, katika nchi za Afrika ya Mashariki, na kuona kuwa bado bei za umeme za Tanzania zipo chini ukilinganisha na bei za katika nchi jirani kama inavyoonyeshwa hapa chini, kwa makundi mbalimbali ya watumiaji umeme.

Pamoja na maamuzi hayo, Bodi ya Wakurugenzi wa EWURA, pia iliagiza TANESCO kutekeleza yafuatayo:

    kuzalisha umeme kwa kutumia mitambo yenye gharama nafuu ("least cost merit order") na kuwasilisha ripoti kwa Mamlaka katika kila mwezi ikionyesha uzalishaji halisi na mpango wa uzalishaji kama ilivyoidhinishwa na EWURA;

    kuhakikisha kuwa zabuni za miradi ya uzalishaji umeme zinatolewa kulingana na mahitaji kama ilivyoidhinishwa kwenye Mpango wa Umeme wa Taifa (Power System Master Plan). Miradi yote mipya lazima ipatikane kwa njia ya ushindani kwa kufuata Sheria ya Umeme, "Public Private Partnership Act", Sheria ya Manunuzi ya Umma na Kanuni husika;

    kuwasilisha ripoti kila baada ya miezi mitatu kuhusu viashiria vya takwimu za ubora na uhakika wa umeme (supply and reliability) katika misongo ya 11kV, 33 kV, 66 kV, 132 kV, na 220 kV kwa kila mkoa kwa ajili ya uhakiki. Takwimu husika zinatakiwa kuonyesha jumla ya masaa mteja aliyokosa umeme kwa kila njia ya umeme ("feeder"), kukosekana kwa umeme kulikopangwa (planned outages), na ambao haukupangwa (unplanned outages), idadi ya matukio ya kukosa umeme katika kila "feeder", idadi ya wateja wanaohudumiwa na kila "feeder", idadi ya wateja walioathirika na katizo la umeme katika kila "feeder" na kiasi cha umeme kilichokosekana kutokana na katizo hilo (total unserved energy in kWh);

    kuwasilisha kwa Mamlaka, katika kipindi cha miezi mitatu baada kuanza kwa Agizo hilo la Mamlaka, mpango wa utekelezaji wa "Demand Side Management Programme" ili uidhinishwe;

    kupunguza kiwango cha upotevu wa umeme (technical and non-technical losses) katika mtandao wa usambazaji kutoka asilimia 19 ya mwaka 2012 hadi asilimia 15.1 ifikapo mwisho wa mwaka 2015;

    kubuni mikakati ya kupambana wizi wa umeme utokanao na uunganishaji umeme usio halali, na kuondoa ucheleweshaji usio wa lazima katika kutunganisha wateja wapya;

    kuhamisha wateja walio katika kundi la D1 kwenda T1 endapo matumizi yao ya mwezi yatazidi uniti 75 kwa miezi mitatu mfululizo;

    kuwasilisha kwa Mamlaka, kabla au tarehe 31 Machi, 2014, Mpango wa kuwawekea wateja wake mita za LUKU na AMR ili kupunguza wateja wanaotumia mita za zamani (conventional meters);

    kuwasilisha kwa Mamlaka, kila baada ya miezi mitatu, taarifa/ripoti ya ukusanyaji wa madeni kutoka kwa wateja wake ili kuongeza mapato ya Shirika;

    kutoa elimu kwa wateja wake kuhusu haki na wajibu wa wateja kwa mujibu wa Mkataba wa Huduma kwa Wateja na kushughulikia kero za wateja kama inavyoelekezwa katika Mkataba husika na Kanuni za Umeme;

    kuwasilisha kwa Mamlaka, maombi ya marekebisho ya bei yatokanayo na mabadiliko ya bei za mafuta, mfumuko wa bei na ubadilikaji wa thamani ya fedha; Ukokotoaji wa marekebisho hayo utakuwa kama ulivyoainishwa katika Kanuni za Kupanga Bei za Umeme za mwaka 2013 (Electricity (Tariff Setting) Rules, 2013);

    kuendelea kutoa taarifa kwa Mamlaka kuhusu hali ya kifedha na kiundeshaji. Taarifa hizi zitatumiwa na Mamlaka katika kutathmini utendaji wa TANESCO ikilinganishwa na mashirika mengine ya umeme katika nchi jirani ili kuboresha utendaji wake. Tathmini hii pia itatumiwa na Mamlaka katika kubaini uhalali wa maombi ya baadae ya kurekebisha bei;

    kuwasilisha kwa Mamlaka, kabla au tarehe 31 Machi 2014, mpango wa utekelezaji wa kila sharti katika Agizo la EWURA.

Bei mpya za umeme zitaanza kutumika tarehe 1 Januari 2014. Ni matarajio ya EWURA kwamba TANESCO watatumia fursa hii kutoa huduma bora zaidi za umeme na kuhakikisha kuwa wanashughulikia malalamiko ya wateja kila yanapojitokeza ili kurejesha imani kwa Shirika la Umeme la TANESCO.

RAIS DKT.KIKWETE ATOA ZAWADI YA KRISMASI

kurasiniKaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Beatrice Fungamo (katikati) akimkabidhi Mwakilishi wa Makao ya Watoto Kurasini wilayani Temeke Bibi  Beatrice Mgumiro mbuzi tatu(3), kilo 150 za mchele na lita ishirini za mafuta ya kupikia  ikiwa ni zawadi ya Krismas zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Zawadi hizo ambazo ni mbuzi, mchele na mafuta zilitolewa jana na Rais Kikwete ili kuwakumbuka watoto walio katika makundi maalum ili nao washerekehe sikukuu.mahabusuKaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Beatrice Fungamo (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Kituo cha Mahabusu ya Watoto Ramadhani Yahaya (kulia)  mbuzi mbili (2), kilo 100 za mchele na lita ishirini za mafuta ya kupikia  ikiwa zawadi ya Krismas zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Zawadi hizo ambazo ni mbuzi, mchele na mafuta zilitolewa jana na Rais Kikwete ili kuwakumbuka watoto walio katika makundi maalum ili nao washerekehe sikukuu.msimbazi watotoKaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Beatrice Fungamo (kushoto) akimkabidhi  Msaidizi wa Mkuu wa Kituo cha Watoto Yatima Msimbazi  Sister Maria Silvana  (kulia) mbuzi tatu(3), kilo 100 za mchele na lita ishirini za mafuta ya kupikia  ikiwa zawadi ya Krismas zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Zawadi hizo ambazo ni mbuzi, mchele na mafuta zilitolewa jana na Rais Kikwete ili kuwakumbuka watoto walio katika makundi maalum ili nao washerekehe sikukuu.vosaKaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Beatrice Fungamo (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi WA  Kituo cha Vosa  Mission Hochimin Mugarura (kulia)  mbuzi mbili(2), kilo 100 za mchele na lita ishirini za mafuta ya kupikia  ikiwa zawadi ya Krismas zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Zawadi hizo ambazo ni mbuzi, mchele na mafuta zilitolewa jana na Rais Kikwete ili kuwakumbuka watoto walio katika makundi maalum ili nao washerekehe sikukuu.
Picha na MAELEZO_ Dar es salaam

MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA( TCAA) WATOA MSAADA WA VYAKULA MBALIMBALI KWA WATOTO YATIMA WANAOLELEA KATIKA KITUO CHA NEW LIFE ORPHANS HOME CHA KIGOGO JIJINI DAR ES SALAAM

Afisa habari wa Mamlaka ya  Usafiri wa Anga  Tanzania (TCAA) Ally Changwila  akiwakabidhi  msaada wa madaftari Rahma Seif na Yusra Yahaya  ambao ni watoto wanaolelewa katika kituo cha yatima cha New Life Orphans Home kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam. Vyakula mbalimbali vilitolewa ikiwemo mchele na Maharage.

Afisa habari wa Mamlaka ya  Usafiri wa Anga  Tanzania (TCAA) Ally Changwila  (kushoto) akiwa na wafanyakazi wenza katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto…
Afisa habari wa Mamlaka ya  Usafiri wa Anga  Tanzania (TCAA) Ally Changwila  akiwakabidhi  msaada wa madaftari Rahma Seif na Yusra Yahaya  ambao ni watoto wanaolelewa katika kituo cha yatima cha New Life Orphans Home kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam. Vyakula mbalimbali vilitolewa ikiwemo mchele na Maharage.
Afisa habari wa Mamlaka ya  Usafiri wa Anga  Tanzania (TCAA) Ally Changwila  (kushoto) akiwa na wafanyakazi wenza katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto yatima wanaolelewa katika kituo  cha New Life Orphans Home kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam. Baada ya kuwa kabidhi msaada wa vyakula mbalimbali yakiwemo mafuta ya kupikia , mchele na sukari.
Afisa habari wa Mamlaka ya  Usafiri wa Anga  Tanzania (TCAA) Ally Changwila  akiwakabidhi  msaada wa mafuta ya kula Mohamed Achume ambaye ni miongoni mwa  watoto wanaolelewa katika kituo cha yatima cha New Life Orphans Home kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam. Vyakula mbalimbali vilitolewa ikiwemo mchele na Maharage.
Mohamed Achume anayelelewa katika kituo cha kule yatima cha New Life Orphans Home kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam akikabidhiwa  msaada  wa gunia la mchele na  Afisa habari wa Mamlaka ya  Usafiri wa Anga  Tanzania (TCAA) Ally Changwila (kushoto) ikiwa ni sehemu ya vyakula mbalimbali vilivyotolewa na mamlaka hiyo kwa ajiri ya watoto hao kusherehekea sikukuu ya krismasi.

Monday, December 23, 2013

YANGA YAMTEMA RASMI BRANDTS, BIN KLEB AWEKA MAMBO HADHARANI LEO JANGWANI!!

binklebkatabaro (1)Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Abdallah Bin Kleb (katikati) akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga, kushoto ni Musa Katabaro na kulia Afisa Habari Baraka Kiziuguto. Picha kwa Hisani ya Young Africans Official Website
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Dar es salaam
Tel: 0712461976 au 0764302956
KIMENUKA jangwani!. Siku mbili tu baada ya Yanga kupata kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Simba SC katika mechi ya Nani Mtani Jembe, uongozi wa klabu hiyo umetangaza kuachana na kocha wake, Mholanzi, Ernie Brandts.
Mwenyekiti  wa Kamati ya Mashindano wa klabu ya Yanga Abdallah Bin Kleb amesema Uongozi umempatia taarifa (Notice) ya siku  thelathini (30) , Brandts juu ya kusitisha mkataba wake kuanzia jana Disemba 22 mwaka huu.
Bin Kleb amesema maamuzi hayo yanafuatia muenendo wa matokeo mabaya katika michezo iliyopita ya Ligi Kuu, kirafiki na bonanza la Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba SC mwishoni mwa wiki.
“Hatua ya Yanga kusitisha mkataba  na Brandts isichukuliwe kama chuki bali ni moja ya sehemu ya kuhakikisha tunaboresha benchi la ufundi ili tuweze kupata matokeo mazuri katika Mashindano yanayotukabili”. Alisema Bin Kleb.
 Bin kleb aliongeza kuwa Ukitazama uwezo wa mchezaji mmoja mmoja wa Yanga SC na wapinzani wao Simba Sc, na soka walilocheza kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe  ni dhahiri kocha amefikia mwisho kimbinu na hana njia mbadala.
“Yanga imekua ikicheza chini ya kiwango katika michezo ya Ligi Kuu hali iliyoplekea kupata ushindi kwa tabu na wakati mwingine timu kupoteza pointi”. Alisema Bin Kleb.
 Mwenyekiti huyo alisema kuwa Kufuatia kupewa taarifa ya siku 30, Brandts ataamua mwenyewe kama ataendelea kusimamia mazoezi ya timu au kuondoka moja kwa moja kabla ya muda huo ukiwa haujakamilika. 
Bin kleb aliongeza kuwa Ikiwa Brandts ataondoka mapema timu itaendelea na mazoezi kama kawaida  kila siku asubuhi katika uwanja wa bora kijitonyama kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na mashindano ya kimataifa chini ya kocha msaidizi Fred Felix “Minziro”.
 “Ili kuhakikisha timuYanga  inafanya vizuri katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya kimataifa uongozi unakamilisha maandalizi ya safari ya kambi nje ya nchi na taratibu zote zitakapokamilika tutawajulisha”. Alisema Bin Kleb.
BRANDTSErnie Brandts amepewa `Notice` ya kusitishwa kwa mkataba wake.
Aidha uongozi upo katika mchakato wa kumapata mrithi wa Brandts ambaye ataungana na timu kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili na Mashindano ya klabu Bingwa Afrika.
 “Tunawaomba wanachama, wapenzi na washabiki wa Yanga wasivunjike moyo kufuatia matokeo ya bonanza mwishoni mwa wiki, uongozi unajipanga kuhakikisha timu inaimarika kwenye benchi la ufundi na kurudisha furaha katika mzunguko wa pili wa VPL”. Alisema Bin Kleb.
Katika hatua nyingine , Bin Kleb amethibitisha ushiriki wa Yanga katika Kombe la Mapinduzi Januari mwakani visiwani Zanzibar.
Mwaka huu Yanga haikushiriki kombe la mapinduzi kufuatia kuwa na ziara nchini Uturuki ambako iliweka kambi ya wiki mbili.

Waziri Mkuu azindua boti mbili za doria na uokozi

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba ametoa siku 14 kwa wizara na taasisi zinazohusika na Kituo cha Kitaifa cha pamoja cha Oparesheni zipeleke w...