Mabilioni ya JK hayakupaswa kwenda benki

HAPANA shaka walalahoi wenzangu mtakuwa katika majonzi makubwa hasa baada ya kubaini kuwa kile mlichoahidiwa, ni dhahiri kuwa ni ndoto ya mchana na katu haiwezi kuwakomboa hata iweje.

Nadhani mnakumbuka kwamba Serikali ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ile ya Awamu ya Nne hivi karibuni ilitoa matumaini mapya kwa kutoa ahadi ya kugawa Sh21 bilioni katika mikoa yote nchini.

Tulipotajiwa tarakimu, hakika wengine tulifurahia sana tukajua kwamba angalau tunaweza kuambulia vijisenti na hivyo angalau kutusukuma kututoa tulipo hadi katika hatua nyingine.Soma zaidi kwa kubonya hapa

Comments

Unknown said…
Sasa mzee wa mishitu kama fedha hazitakua managed na watu wenye uwezo na uzoefu kama mabenki si hela zote hizo zitapotea? Hizo fedha ni mkopo na mkopo wowote ili uweze kufanikiwa lazima usimamiwe vizuri na wataalam.
MTANZANIA. said…
Duh! Inasikitisha na inauma sana. Inahitaji usimamizi wa hali ya juu ili mikopo iwafikie walengwa. Karibu kwenye blog yangu mzee wa Mshitu.
Habari Hub said…
Mtanzania nitafika nyumbani kwako kukutembelea hakuna shida.
Stephen naelewa sana kwamba unahitajika usimamizi ila ninachosema fedha hizi hazitatusaidia masikini ng'o