Monday, November 30, 2015

WANASOKA WANAWAKE ZAIDI YA 400 WASHIRIKI TAMASHA LA LIVE YOUR GOALS

 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akifuatilia kabumbu ya wanawake iliyokua ikiendelea wakati wa tamasha la Live Your Goals kuhamasisha mpira wa miguu wa wanawake lililoandaliwa na FIFA jana jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Karume. Kulia ni Mkurugenzi wa Michezo Bw. Leonard Thadeo, na kushoto ni Mwenyekiti Kamati Soka la Vijana Bw. Ayoub Nyenzi.
 Baadhi ya wanasoka wanawake kutoka katika vilabu mbalimbali vya mpira wa miguu wakisakata kabumbu jana jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Karume wakati wa tamasha la Live Your Goals kuhamasisha mpira wa miguu wa wanawake lililoandaliwa na FIFA.
  Mabalozi walioteuliwa na FIFA kuhamasisha mpira wa miguu wa wanawake nchini wakijitambulisha kwa mgeni rasmi wakati wa tamasha la Live Your Goals lilifanyika jana jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Karume kwa mara ya pili baada ya kufanya tamasha hilo kwa mara ya kwanza Mkoani Geita mnamo mwezi Julai 2015.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (wapili kushoto) akimwangalia mtoto Zaynab Dotto mwenye umri wa miaka 10 anavyocheza na mpira kwa umahiri jana jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Karume. Kulia ni Mratibu wa Michezo ya Vijana wadogo Bw. Raymond Gweba na kushoto ni mama mzazi wa mtoto Zaynabu Bibi. Pili Said.

CCM YAKANUSHA TAARIFA ZA MITANDAONI KWAMBA IMEKUBALI KUMKABIDHI MAALIM SEIF IKULU

Chama cha Mapinduzi CCM kimekanusha Taarifa iliyozagaa katika Mitandao ya Kijamii kwamba Chama hicho kimeridhia aliyekuwa Mgombea wa Urais wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akabidhie nchi kuiongoza kwa miaka mitano. 

Akikanusha Taarifa hiyo mbele ya Waandishi wa Habari Afisini kwake Kisiwandui Naibu Katibu Mkuu wa CCM Vuai Ali Vuai amesema taarifa hiyo ni uzushi uliotungwa ili kuwatia taharuki WanaCCM na Wananchi kwa Ujumla. 

Amesema toka kusambaa kwa Taarifa hiyo Jana amekuwa akipigiwa simu na Watu mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kujua ukweli wa Taarifa hiyo hasa ikizingatiwa kuwa ilidaiwa kusainiwa na Naibu huyo. “Huu ni Uzushi Mkubwa na kwamba unafaa kupuuzwa maana hauna lengo jingine zaidi ya kuwagawa WanaCCM” Alismema Vuai. 

Amesema kilichopo nikwamba CCM inajiandaa kwa ajili ya uchaguzi wa Marejeo kama ambavyo Tume ya Uchaguzi ilitangaza kuufuta Uchaguzi na hivyo kurudiwa upya. Aidha Vuai amesema kuwa tayari wamewasiliana na Wanasheria wao pamoja na wataalamu mbalimbali ili kuwabaini waliohusika kusambaza Taarifa hizo na kuwapeleka katika Vyombo vya Sheria. 

“Tumeshafanya mawasiliano na Wataalam wetu na tukiwabaini Sheria ya Makosa ya mtandao itachukua nafasi yake” Alisema Vuai. 

Katika taarifa hiyo iliyosambaa na kudai kusainiwa na Vuai Ali Vuai ilisema kuwa Chama cha mapinduzi kimeridhia na kukubali kumpa nchi Maalim Seif Sharif kupitia chama chake cha Cuf kuwa ndio rais wa uchaguzi ulopita,na yeye ndio atakayeongoza serikali ya umoja wa kitaifa. 

Taarifa hiyo ilieleza kuwa CCM imekubali kushirikiana na maalim Seif katika kuongoza nchi chini ya serikali ya umoja wa kitaifa na kukubali kutoa makamo wa kwanza wa rais na nusu ya mawaziri. 
Vuai amerejea kauli yake kuwa mazungumzo yanayofanywa na Viongozi wa Kitaifa kwa kushirikiana na Viongozi Rais Wastaafu wa Zanzibar hayawezi kubatilisha maamuzi ya Tume ya kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliopita. 


IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR.

RAIS MAGUFULI AONANA NA MABALOZI WA CHINA NA KOREA KUSINI, PROFESA LIPUMBA IKULU LEO

ba7 
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana  na aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba  Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba. Profesa Lipumba amempongeza Rais kwa kuchaguliwa kwake kwa kishindo na pia ameipongeza hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa wakati wa kufungua Bunge la 11 mjini Dodoma 30, 2015
ba9 
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akifanya mazungumzo na aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba  Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba. Profesa Lipumba amempondeza Rais kwa kuchaguliwa kwake kwa kishindo na pia ameipongeza hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa wakati wa kufungua Bunge la 11 mjini Dodoma 30, 2015
ba10 
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana na aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba  Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba. Profesa Lipumba amempondeza Rais kwa kuchaguliwa kwake kwa kishindo na pia ameipongeza hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa wakati wa kufungua Bunge la 11 mjini Dodoma 30, 2015. 
ba1 
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana  na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015
ba2 
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015
ba4 
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana  na Balozi wa Korea ya Kusini  hapa nchini Mhe. Chung IL Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015. Balozi huyo pia alitumia nafasi hiyo kumuaga Rais kwa kuwa muda wake wa kufanya kazi nchini umemalizika.
ba6 
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na Balozi wa Korea ya Kusini  hapa nchini Mhe. Chung IL Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015. Balozi huyo pia alitumia nafasi hiyo kumuaga Rais kwa kuwa muda wake wa kufanya kazi nchini umemalizika.
PICHA NA IKULU

Sunday, November 29, 2015

Vijana wa Iringa wawezeshwa na Airtel FURSA‏

MSD yakarabati jengo la duka la dawa hospitali ya taifa Muhimbili

Mafundi wakikarabati jengo ambalo Bohari ya Dawa (MSD), itafungua duka la dawa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MSD) Dar es Salaam jana kwa ajili ya kuhudumia wananchi kwa karibu zaidi vikiwemo vifaa tiba. Duka hilo linatarajiwa kufunguliwa kesho kutwa.
Fundi akitoboa ukuta sehemu litakapo fungwa beseni la kunawia katika duka hilo.
Mafundi wakiendelea na ukarabati wa jengo hilo lililopo jirani na wodi ya Kibasila linalotizamana na maegesho ya magari.
Fundi akipaka rangi ndani ya jengo hilo.
Jengo la duka hilo la MSD linavyoonekana kwa nje. Hapa mafundi wakiendelea na kazi ya ukarabati.
 
BOHARI ya Dawa (MSD) imejiimarisha na kuhahikisha inatekeleza kwa wakati agizo la Rais Dk. John Magufuli la kuweka maduka ya dawa katika hospitali za rufaa na kanda nchini.
Katika kutekeleza agizo hilo MSD imeanza kwa kasi kubwa ya kukarabati jengo la duka la dawa katika  Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), ambalo linatarajiwa kufunguliwa kesho.
Mwandishi wa habari hii alishuhudia jana kasi kubwa ya mafundi ujenzi wakikarabati  jengo hilo ambalo awali lilikuwa likitumika kama stoo ya kuhifadhi vitu mbalimbali vya hospitali hiyo.
Akizungumza na vyombo vya habari hivi karibuni kuhusu ufunguzi wa maduka hayo, Mkurugenzi Mkuu wa  MSD, Laureane Bwanakunu alisema  agizo la Rais la kuitaka MSD kuanzisha duka la dawa karibu na hospitali limekuja wakati muafaka kwani  kwenye mpango mkakati wa miaka sita wa MSD tayari ilikuwa na mpango wa kufungua maduka hayo kwa ajili ya kusogeza huduma karibu a wananchi.
Alisema maduka ya MSD ambayo yatafunguliwa kwenye hospitali za rufaa na kanda yatafanya kazi masaa 24 na kuuza dawa na vifaa tiba  chini ya bei ya soko pia yatahudumia watu binafsi na wale waliopo kwenye taratibu za Bima ya afya kote nchini.
“Ili kudhibiti watumishi wasio waaminifu kuiba dawa MSD inafanya kazi za uagizaji, uhifadhi  na usambazaji kwa kutumia mfumo wa mtandao wa E9 na tangu mwaka wa fedha uliopita tumeanza kuziwekea alama ya GOT bidhaa zetu ikiwa ni pamoja na vidonge.” alisema Bwanakunu.  
Alisema vidonge ambavyo tayari vimewekewa nembo ya GOT vipo 45 na wanaendelea kuwapa maelekezo wazabuni ili vyote viwekwe alama hizo..,nembo ya serikali inaonekana kwenye dawa za serikali kama Diclofenac, moxillin, iprofloxacin, Contrimoxale,paracetamol,
na magnesium.
Alisema wanatarajia kuanzisha huduma ya kutoa taarifa kwa njia ya simu pale wananchi watakapoona kuna wizi wa dawa za serikali na kwamba wananchi  wanaelimishwa kutoa taarifa pale wanapoona dawa za serikali mitaani.
Alisema, pamoja na serikali kuanza kupunguza deni lake linalodaiwa na MSD bado inadaiwa Sh.bilioni 53.

BOMOBOMOA SALASALA ILI KUPISHA UJENZI WA BOMBA LA MAJI -RUVU CHINI


 Kazi ya kubomoa baadhi ya nyumba ikiendelea mwishoni mwa wiki eneo la Salasala jijii Dar es salaam ili kupisha ujenzi wa bomba la maji kutoka Ruvu Chini.
  Tingatinga likisukuma na kung’oa miti na jengo eneo Salasala iliyo  ndani ya hifadhi ya bomba la maji kutoka Ruvu Chini hadi jijini Dar es salaam jijii Dar es salaam.
  likisukuma na kung’oa mnazi eneo Salasala ambao upo ndani ya hifadhi ya bomba la maji kutoka Ruvu Chini hadi jijini Dar es salaam jijii Dar es salaam.
  Tingatinga likisukuma na kung’oa mnazi eneo Salasala ambao upo ndani ya hifadhi ya bomba la maji kutoka Ruvu Chini hadi jijini Dar es salaam jijii Dar es salaam.

Mafundi wakiendelea kubomoa nyumba iliyopo eneo la Salasala kwa hiyari ya mmiliki wa nyumba hiyo ili kupisha ujenzi wa bomba la maji kutoka Ruvu Chini. (Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO).
Tingatinga likishushwa tayari kwa kazi ya bomobomoa eneo la Salasala jijii Dar es salaam ili kupisha ujenzi wa bomba la maji kutoka Ruvu Chini hadi jijini Dar es salaam.


  Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Zoezi la kubomoa nyumba na majengo yaliyoingia ndani ya ya hifadhi ya miundombinu ya bomba la maji kutoka Ruvu Chini limeendelea mwishoni mwa wiki ili kuhakikiha kunakuwepo usalama wa bomba hilo na kuwapatia wakazi wa jiji la Dar es salaam na maeneo ya mkoa wa Pwani uhakika wa maji ifikapo Februari, 2016.  

Bomo bomoa hiyo ya mwishoni mwa wiki ilihusisha maeneo ya Salasala ambapo baadhi ya nyumba, karakana na uzio vyote viljengwa ndani ya hifadhi ya miundombinu hiyo ya maji.

Akizungumzia ubomoaji huo, Mkurugenzi wa Usimamizi na Ufundi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), Romanus Mwang'ingo alisema kuwa ni wajibu wa wakazi wa maeneo hayo kuvunja sehemu za makazi yao yaliyoingia ndani ya hifadhi ya mradi kwa hiyari ama nyumba hizo kuvunjwa baada ya kukaidi agizo la kubomoa ili kupisha ujenzi wa bomba la maji kutoka Ruvu Chini hadi jijini Dar es salaam.

“Umbali sahihi unaopaswa wakazi hao kujenga makazi yao kutoka lilipo bomba la maji ni mita 15 kila upande ambapo hatua hiyo inapelekea kuwa jumla ya mita 30 ya umbali unaotakiwa ili kuhakikisha kunakuwepo na usalama na kuruhusu matengenezo mengine tofauti na hali ya awali ambayo huwezi hata kufanya kazi maana bomba limepita ndani ya uzio na makazi ya watu ambayo ni hatari kwa usalama wa maisha yao na mali zao” alisema Mwang'ingo.

Vile vile Mwang’ingo alizitaja changamoto zilizochangia kuchelewesha kukamilika kwa mradi huo kwa wakati ni kuwepo kwa kesi zilizofunguliwa na wananchi kuzuia ufanisi wa kazi hiyo ambapo kulikuwa na kesi 17 katika mahakama mbalimbali katika maeneo hayo ikiwemo mahakama ya ardhi. 

Kwa mujibu wa Mwang’ingo hadi sasa DAWASA imeshinda kesi 13 na kupewa haki ya kutumia njia hiyo kukamilisha upanuzi wa mradi na zimebaki kesi nne ambazo bado zipo mahamani na zimefikia hatua mbalimbali kulingana na taratibu za kimahakama.

Kwa upande wake mkazi wa Salasala Mhandisi Josephat Nakapange ambaye sehemu ya nyumba yake pamoja na uzio vipo ndani ya hifadhi hiyo ya bomba la maji kutoka Ruvu Chini hadi Dar es salaam alisema kuwa yeye hana tatizo wala ugomvi na mradi huo, wamepokea maelekezo na wanayafanyia kazi.
“Hivi sasa ninavyoongea mafundi wapo kwenye eneo langu wanaendelea na zoezi la kutoa mabati na baadaye kuvunja kuta zilizo ndani ya umbali unaotakiwa kuachwa wazi kwa ajili ya mradi wa bomba la maji” alisema Josephat.

Aidha, Josephat aliongeza kuwa ni vema ziwekwe alama katika maeneo yote yanayotakiwa kuachwa wazi ambayo yapo ndani ya hifadhi ya mradi ili kuepusha usumbufu na gharama zisizo za lazima kwa wakazi ulipopita mradi huo.
Maeneo yaliyohusishwa na ubomoaji huo mwishoni mwa wiki ni pamoja na Bunju, Bondeni, Boko, Tegeta, Mbezi Intacheki, na Mbezi Tangibovu ili kuruhusu kukamilisha ujenzi wa bomba hilo la maji kutoka Ruvu Chini ha jijini Dar es salaam.

Saturday, November 28, 2015

NEWS ALERT: WATUMISHI WENGINE WATATU WASIMAMISHWA KAZI TRA

SERIKALI imewasimamisha kazi watumishi watatu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao jana iliamriwa kwamba watahamishiwa mikoani.

Watumishi hao ni Bw. Anangisye Mtafya, Bw. Nsajigwa Mwandengele na Bw. Robert Nyoni.

Uamuzi huo umetolewa leo (Jumamosi, Novemba 28, 2015), na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa ili kupisha uchunguzi zaidi wa tuhuma zinazowakabili. Kama ilivyo kwa wenzao sita waliosimamishwa kazi jana (akiwemo aliyekuwa Kamishna Mkuu), nao pia hawaruhusiwi kusafiri kwenda nje ya nchi hadi uchunguzi utakapokamilika.
 “Kazi ya kuwachunguza ilianza jana ileile na sasa, tumeona hawa watu wanapaswa kuwa nje ya utumishi ili kupisha uchunguzi ufanyike kwa uhuru zaidi,” alisema Waziri Mkuu.
Pia Waziri Mkuu amemuagiza Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, Dkt. Philip Mpango atekeleze maagizo hayo kwa kuwaandikia barua watumishi hao.

Jana mchana, Waziri Mkuu alifanya ziara ya kushtukiza kwenye bandari ya Dar es Salaam akiwa na nia ya  kukagua namna shughuli zinavyoendelea kwenye bandari hiyo hasa kwenye maeneo ya kupokelea mizigo kutoka nje ya nchi.
Katika kikao kilichofanyika bandarini hapo na kuhudhuriwa na baadhi ya viongozi wa Serikali, Waziri Mkuu aliamua kuwasimamisha kazi maafisa watano na TRA kutokana na ‘upotevu’ wa makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 80/-.
Waziri Mkuu alisema upotevu huo unasababishwa na mchezo unaofanyika baina ya wafanyabiashara na watumishi wa TRA ambao wanaruhusu makontena kupita bila kulipiwa ushuru na hivyo kuikosesha Serikali mapato

MAKATIBU WAKUU WAKAGUA AICC MAANDALIZI YA MWISHO MKUTANO WA IPU, ARUSHA

Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali pamoja na Kamati ya Wataalamu ya Maandalizi ya Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), wamefan...