Tuesday, December 30, 2014

AJALI YA LORI NYORORO IRINGA, LAFUNGA BARABARA KWA SAA KADHAA

Sehemu ya msururu wa magari yaliyokwama baada ya ajali hiyo kuziba barabara ya Iringa-Njombe
Msururu wa magari yaliyokwama baada ya ajali hiyo kuziba barabara ya Iringa-Njombe
Sehemu ya Lori lililopata ajali
Wafanyakazi wa Lori hilo wakitafakari nini cha kufanya

Edwin Moshi wa Eddy Blog
Watumiaji wa barabara ya Iringa Njombe wamekwama toka jana majira ya saa 10 jioni kufuatia ajali ya lori lililobeba shaba lenye namba za usajili T 261 BCM linalovuta tela lenye namba za usajili T 595 BAS kupata ajali na kufunga barabara na kusababisha magari kushindwa kupita. 
 Mtandao huu umeshuhudia msururu mkubwa wa magari yanayokwenda mikoa ya njombe Ruvuma Mbeya na nchi jirani, pamoja na yanayotoka kwenye mikoa hiyo kwenda Iringa Dodoma, Dare es Salaam na mikoa mingine yakiwa yamekwama kwenye msururu huo.

Ajali hiyo imetokea eneo la Nyororo mkoani Iringa. 
Baadhi ya abiria na madereva wa malori waliokuwa eneo la tukio wamelalamikia ufinyu vya kulitoa lori hilo kuwa ni hafifu hali iliyopelekea wakae hapo muda mrefu(karibia siku moja). 



 Hali hiyo iliondolewa majira ya saa tatu asubuhi baada ya lori hilo kufanikiwa kuondolewa barabarani na kusogezwa pembeni ndipo magari hayo yakaendelea na safari.  

SHEIKH ALI MZEE COMORIAN AZIKWA MAKABURI YA WANGAZIJA, JIJINI DAR

 Rais Mstaafu wa awamu ya pili,Alhaj Ali Hassan Mwinyi (wa tatu kushoto),Waziri Mkuu Mstaafu,Dkt. Salim Ahmed Salim (wa nne kulia),Sheik Mkuu wa Tanzania,Shaaban Simba (wa pili kushoto) na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mussa Salum (wa tatu kulia) wakijumuika pamoja na Waombolezaji wengine kwenye ibada ya Mazishi ya Sheikh Ali Mzee Comorian,katika makaburi ya Wangazija mtaa wa Bibi Titi Mohamed, jijini Dar es salaam mapema jana.
Masheikh wakijadiliana jambo kabla ya Mazishi ya Sheikh Ali Mzee Comorian,katika makaburi ya Wangazija mtaa wa Bibi Titi Mohamed,jijini Dar es salaam mapema jana.
Taratibu ya kuandaa Kaburi la Marehemu Sheikh Ali Mzee Comorian zikiendelea katika makaburi ya Wangazija mtaa wa Bibi Titi Mohamed,jijini Dar es salaam mapema  jana,huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha.
Umati wa Waombolezaji ukiwasili kwenye Makaburi ya Wangazija mtaa wa Bibi Titi Mohamed,jijini Dar es salaam mapema leo,tayari kwa kuhifadhi mwili wa Marehemu Sheikh Ali Mzee Comorian akiefariki Dunia jana.
Sehemu ya Umati wa Waombelezaji ukiwa umebeba Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Sheikh Ali Mzee Comorian ukiwasili kwenye Makaburi ya Wangazija mtaa wa Bibi Titi Mohamed,jijini Dar es salaam mapema jana.
Waombolezaji wakiendelea na shughuli ya Mazishi ya Marehemu Sheikh Ali Mzee Comorian kwenye Makaburi ya Wangazija mtaa wa Bibi Titi Mohamed,jijini Dar es salaam mapema jana.
Baada ya mazishi waumini wa Kiislam walifanya zikri kwenye Kaburi la Marehemu Sheikh Ali Mzee Comorian kwenye Makaburi ya Wangazija mtaa wa Bibi Titi Mohamed,jijini Dar es salaam mapema jana.
(PICHA ZA OTHMAN MICHUZI/EMMANUEL MASSAKA)

DIAMOND PLATNUMZ ATUA RWANDA KWA SHANGWE


Staa wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' akiwa na mfanyabiashara mrembo na muimbaji wa Uganda, Zarinah Hassan 'Zari'  au 'The Boss Lady' baada ya kuwasili Rwanda jana.
Diamond Platnumz (katikati) akiwa kamshika mkono mpenzi wake wa sasa Zarinah Hassan 'Zari'  au 'The Boss Lady baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Rwanda.
Diamond na The Boss Lady wakifanya yao.
Diamond (kulia) akiongea na wanahabari baada ya kuwasili Rwanda.
Wanahabari wakifanya yao.

Monday, December 29, 2014

MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA KATA ZA MBANJA


Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama cha Mapinduzi anayewakilisha Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akiongea na vijana na wananchi mara baada ya kuzindua rasmi shina la wakereketwa Zahanati Kempu lililoko katika Kata ya Rasibura 
Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM anayewakilisha Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akizungumza na viongozi wa Tawi la CCM la
Baadhi ya wajumbe wa Tawi la Chama Cha Mapinduzi Mabano katika Kata ya Mbanja wakifurahia hotuba ya Mjumbe wa NEC Taifa wa Lindi Mjini Mama Salma Kikwete wakati alipotembelea Tawi hilo.
Katibu wa Shina la Wakereketwa Zahanati Kempu Ndugu Hidaya Chivi Ali akikabidhi risala ya wanachama wa Shina hilo kwa Mjumbe wa NEC Taifa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.

HIVI NDIVYO ALIVYOPOKELEWA DIAMOND NA KUNDI LAKE NCHINI BURUNDI..

116

1 
2 3 4 5 6 7 1515782_813759588680773_361530474_n 10843796_1600128320221330_1387340386_n  10864869_1532023193734930_727265778_n 10864970_1592259054322814_1268864582_n 10890552_323662227824937_934916415_n 10891006_431393020343188_1378749524_n

NYALANDU ATANGAZA RASMI KUWANIA URAIS 2015

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo Nyalandu alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota kwenye Mkutano wa jimbo uliofanyika kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo, jimboni humo (Picha na Bashir Nkoromo)
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo Nyalandu alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota kwenye Mkutano wa jimbo uliofanyika  kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo, jimboni humo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo Nyalandu alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota kwenye Mkutano wa jimbo uliofanyika kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo, jimboni humo
 Mwimbaji wa muziki wa Injili, Frola Nkone akiimba kutumbuiza wakati wa mkutano huo
Mwanamuziki wa muizki wa Injili, Rose Mhando akiimba kutumbuiza wananchi katika mkutano huo wa Nyalandu
Wasanii wa kikundi cha Makomandoo cha mjini Singida wakitumuiza wakati wa mkutano huo
Wadau wakifurahia burudani wakati wa mkutano huo wa Nyalandu

 Steve Nyerere ambaye ni Msanii na Kamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM, akizungumza kabla ya kumwaga vimbwanga vyake vya kuingiza sauti za viongozi mbalimbali wakati wa mkutano huo wa Nyalandu.
KABLA YA MKUTANO
Nyalandu na Mkewe Faraja Kota wakiingia kwenye Kanisa la KKKT  Usharika wa Ilongelo kwa ajili ya ibada maalum. Pamona nao ni watoto wao Sera na Christopher kabla ya kwenda Uwanjani kutangaza azma yake ya kuwania Urais 2015
Nyalandu na Faraja Kota wakiwa na watoto wao Sera na Christopher katika kanisa hilo 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro  Nyalandu akitoa neno la shukrani baada ya ibada maalum katika katisa la KKKT Usharika wa Ilongelo jimboni humo.
Mwimbaji wa nyimbo za Injili lkatika Kanisa la KKKT Usharika wa Ilongelo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu akizungumza na viongozi wa shule ya Kiislam ambayo huhudumia watoto wa dini zote katika kata ya Ilongelo, shule hiyo ina watoto 74.
Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akisalimia waumini kwenye Kanisa la FPCT  katika jimbo la Ilongelo alipofika kwa ajili ya ibada maalum
Waumini wakiwa katika kanisa la FPCT wakati wa ibada maalum aliyohudhuria Nyalandu jana
Nyalandu na Mkewe wakitoka katika Kanisa la FPCT baada ya kuhudhuria ibada maalum jana asubuhi. Na Bashir Nkoromo, Singida
Mbunge wa Singida Kaskazini, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ametangaza rasmi kuwania Urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu mwakani.
Amesema amechukua uamuzi huo baada ya kuona kwamba anao uwezo wa kuiongoza Tanzania, katika harakati za kuwafikisha kwenye maendeleo endelevu wanayotaka Watanzania.
Amesema, yuko tayari kushindanishwa na Watanzania wengine watakaoona kuwa wanafaa kuwa Rais, lakini akisema kwanza kila atakayejitokeza itabidi kazi zake zipimwe kwa moto na endapo zitayeyuka hafai.
Nyalandu ambaye alitangaza uamuzi huo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo jimbo la Singida Kaskazini, alisema, yeye anaingia kwenye kinyang'anyiro akiwa kifua mbele kutokana na kuamini kwamba amekwishafanyakazi zilizotukuka.
"Kazi zangu nilizofanya zinajulikana na ninaziamini kwamba ni nzuri, hivyo yeyote atakayetaka urais apimanishwe na mimi kwa kupimwa kazi zetu kwa moto", alisema Nyalandu
Itakapofika siku ya siku, nitaenda Dodoma nikisindikizwa na wana Singida Mashariki, na wengine wengi kutoka pembe zote za Tanzania, kwenda Dodoma kuchukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea Urais kwa tiketi ya CCM", alisema.
Mkutano huo wa jimbo ambao ulipambwa na shamrashamra mbalimbali zikiwemo za wasanii wakiwemo kina Rose Mhando, ulifurika maelfu ya wananchi waliohamasika kumsikiliza Nyalandu.
HABARI KATIKA PICHA, NYALANDU AKITANGAZA KUWANIA URAIS JANA.

SERIKALI YARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA KITUO CHA KISASA CHA UTALII KUSINI, KUKAMILIKA DESEMBA

  Na Mashaka Mhando, Iringa UJENZI wa kituo cha kisasa cha utalii mkoani Iringa, kinachotarajiwa kuwa mkombozi na kiungo muhimu cha kukuza u...