Wednesday, August 02, 2017

Vitu ambavyo hauruhusiwi kusafiri navyo kwenye ndege


Na Jumia Travel Tanzania

Kama umeshawahi kusafiri kwa ndege naamini utakuwa unafahamu ni kitu gani cha kubeba kwenye begi lako na kipi sio. Endapo haujawahi au unatarajia kufanya hivyo kwa siku za hivi karibuni basi usafiri huo una masharti na taratibu zake ambazo ni lazima zifuatwe vinginevyo hautoweza kuutumia.

Tofauti na usafiri wa kawaida kama vile mabasi ambayo watanzania wengi tunayatumia ambapo ni mara chache kukuta kunakuwa na upekuzi mkali wa abiria mbali na tiketi zao, Jumia Travel ingependa kukufahamisha kwamba kusafiri kwa kutumia ndege kuna masharti na taratibu ambazo kila abiria ni lazima azifuate na kuzizingatia ndipo aruhusiwe kuingia ndani.  

Vifaa vyenye ncha kali.Hairuhusiwi kabisa kubeba vitu vyenye ncha kali kama vile kisu, wembe, mkasi, bisibisi au panga kwenye begi lako la kusafiria labda iwe kwenye mzigo tofauti ambao utapekuliwa na kupewa kibali. Kwa ufupi kama unadhani utahitajika kuvibeba ni vema kuviweka kwenye mzigo tofauti ili vifanyiwe upekuzi ndipo uruhusiwe. Tofauti na hapo ili kuepuka usumbufu au kuchelewa safari yako basi unashauriwa kuwasiliana mapema na shirika la ndege utakalosafiri nalo kwa msaada zaidi.      

Silaha za moto. Hakuna silaha inayoruhusiwa kubebwa kwenye begi lako la kusafiria kwa sababu za usalama wako na abiria wengine kwenye ndege. Ingawa taratibu hutofautiana baina ya nchi au mashirika ya ndege lakini asilimia kubwa vitu hivyo huwa haviruhisiwi kabisa labda kuwa na sababu na kibali maalumu.   

Vitu vinavyoweza kulipuka.Kuna baadhi ya bidhaa tunazitumia ambazo ndani yake zina kemikali ambazo hulipuka kwa urahisi bila ya kujua. Kwa mfano, takribani marashi yote ya kujipulizia mwilini (body spray) au vibiriti vya gesi huwa na kemikali ambazo zinaweza kulipuka kwa urahisi na ndiyo maana huwekwa alama ya moto (inflamable). Hivyo basi ni vema kulijua hilo ili unaposafiri usibebe maana utaishia kwenda kuyaacha mahala pa ukaguzi kabla ya kupanda ndege.

Vifaa vya michezo. Kuna baadhi ya vifaa vya michezo vinachukuliwa kama silaha. Kwa mfano, vifaa vya kuchezea gofu, tenesi, mpira wa magongo, upinde na mkuki na kadhalika. Kwa mfano, timu nyingi za michezo mbalimbali zinaposafiri vifaa hivi huwekwa kwenye mizigo tofauti na ile ya wachezaji kwa ajili ya ukaguzi ili kuepusha usumbufu.

Vifaa vya kazi. Inawezekana ukawa ni fundi mzuri na una wateja takribani kila kona ya nchi hivyo ukahitajika kusafiri kwenda kufanya kazi. Itakuwa ni jambo la busara ukafahamu mapema kwamba kusafiri kwenye begi lako na vifaa vyako vya kazi kama vile nyundo, msumeno, patasi au bisibisi itakuwa ngumu. Utaweza kufanya hivyo pale tu utakapovifungasha kwenye mzigo wake tofauti ili ukaguliwe kwa ajili ya usalama wako.   

Dawa za binadamu. Kuna wakati unaweza ukawa na matatizo ya kiafya lakini ukahitajika kusafiri hivyo ni vema kujua pia kuna taratibu za kusafiri na dawa zako za matibabu. Iwe unasafiri ndani au nje ya nchi vitu muhimu vya kuzingatia ni pamoja na barua au maelezo ya daktari kuhusu ugonjwa wako pamoja na dawa alizopendekeza kuzitumia na kubeba. Kwa hiyo ili kuepuka kuzuiwa kusafiri na dawa wakati mwingine itakuwa vizuri hata ukawasiliana na shirika la ndege utalosafiri nalo ili ujue taratibu zao zikoje.

Vimiminika. Unaweza ukashangaa kwanini hautoruhusiwa kusafiri na maji yako ya kunywa ambayo umeyabeba kwenye begi lako. Ingawa sheria hutofautiana kwa baadhi ya nchi ambazo huruhusu kiwango fulani kwa hapa Tanzania hali ni tofauti. kwenye kundi hili maziwa ya chupa na madawa hayaingii kwenye kundi hili ingawa ni lazima yaambatinishwe na maelezo au kibali maalum.     

Bangi. Nadhani hili linaeleweka miongoni mwa watu wengi kwamba Tanzania kilevi hicho ni marufuku kukitumia kwa hiyo kukutwa nacho tu ni uvunjaji wa sheria. Kuna baadhi ya nchi zinaruhusu aina ya kilevi hicho kana kwamba mpaka madaktari hutoa vibali kabisa kwa wagonjwa wao kutumia. Ila kwa nchi ya Tanzania bangi ni marufuku na ukikutwa nayo utachukuliwa hatua za kisheria.

Kwa kawaida mtu wa kawaida anaposafiri kwa kutumia ndege kunakuwa hakuna vitu vingi vya kuhofia kwani ni mara chache vitu hivyo huhitajika kubebwa. Mbali na hapo utajitafutia matatizo au kuhatarisha usalama wa abiria wenzako. Jumia Travel imeona ni vema kukutahadhirisha kwamba kutokana na kuongezeka kwa matukio ya kutishia usalama kupitia usafiri huo, hatua kali zimekuwa zikichukuliwa na nchi mbalimbali duniani.

RAIS DKT MAGUFULI AWAPANDISHA NA KUWATEUA MAAFISA WAWILI WA ZIMAMOTO KUWA MAKAMISHNA

MTANDAO WA ELIMU TANZANIA, (TenMet), WAKUTANA NA BLOGGERS JIJINI DARES SALAAM


Afisa Programu wa Mtandao wa Elimu Tanzania, (TenMet), Bi. Alistidia Kamugisha, akizungumza wakati wa kikao cha kujenga ushirikiano baina ya taasisi hiyo na Bloggers kilichofanyika makao makuu ya TenMet, Sinza jijini Dar es Salaam, leo Agosti 2, 2017.
Meneja Programu wa TenMet, Bw.Nicodemus Shauri Eatlawe, (katikati), akifafanua jambo wakati wa kikao hicho. Kulia ni Bi. Alistidia Kamugisha, na Afisa Programu wa taasisi hiyo, Bw. David Sizya.
 Mmoja wa washiriki wa kikao hicho, akitoa maoni yake.
 Afisa wa TenMet, Bw. Dominic Dogani, akitoa ufafanuaiz wa masuala mbalimbali yatakayojadiliwa kwenye kikao hicho.
 Majadiliano yakiendelea.

 Mmoja wa washiriki wa kikao akitoa maoni yake.
 Baadhi ya washiriki wa kikao hicho wakinakili yaliyokuwa yakijadiliwa kupitia vitendea kazi vyao.
 Mwenyekiti wa Mtandao wa Bloggers Tanzania, (TBN), Bw. Joachim Mushi, akiwa makini na yaliyokuwa yakijadiliwa.
 Mmiliki wa blog ya Jiachie, Bw. Ahmad Michuzi (kulia) akifuatilia mjadala. Kushoto ni Bw. Mushi.
 Bi. Kamugisha akiweka sawa vitabu vyenye taarifa za TenMet.
 Bw. Sizya, (kulia), akimpatia nakala ya vitabu vya TenMet mwandishi wa Mo Blog, Bw. Rabif Humwe.
Picha ya pamoja.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said.
BINADAMU ili aweze kuyakabili mazingira yake, moja ya nyenzo muhimu ni elimu, na kwa kutambua umuhimu wa elimu, wadau mbalimbali wamekuwa wakifanya juhudi kubwa katika kusaidiana na serikali ili kufikia lengo la kuwapatia elimu Wananchi wa Tanzania.
Mtandao wa Elimu Tanzania, kwa kifupi TenMet, ni moja ya taasisi zinazifanywa juhudi kub wa katika kuhakikisha malengo yaliyotajwa hapo juu yanafikiwa.
TenMet ambayo iliasisiwa miaka 18 iliyopita ikiunganisha taasisi nyingine 39 wakati huo, kwa sasa mtandao huo umepanuka na kufikia jumla ya taasisi 181 zilizojikita katika swala la kuhakikisha watanzania wanapatiwa haki yao ya elimu, lakini sio tu kupatiwa elimu bali pia elimu iliyo bora.
Ili kufikisha ujumbe kwa wahusika (jamii) TenMet hufikisha ujumbe kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na makongamano, semina na vyombo vya habari vikiwemo vile vya kisasa (social media kama vile Blogs).
Agosti 2, 2017, Maafisa wa TenMet waliwaalika bloggers ili kuangalia namna gani wanavyoweza kushirikiana katika kutekeleza malengo yaliyoanishwa hapo juu ya kusambaza taarifa mbalimbali zinazohusu masuala ya elimu.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Meneja Programu wa TenMet, Bw.Nicodemus Shauri Eatlawe, alisema, lengo la mkutano huo ni kuimarisha ushirikiano wa kikazi baina ya taasisi yake na vyombo vya habari vya kimtandao kwani anaamini taarifa zitawafikia wadau wengi zaidi.

“Lakini pia tunaamini ushirikiano huu utatusaidia katika kuibua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu nchini, kwa kuhabarisha umma, hivyo tunayo furaha kubwa kukutana nanyi leo hii.”Alifafanua.
Kwa upande wake, Afisa Programu wa TenMet, Bi. Alistidia Kamugisha, amefafanua kuwa, TenMet kama ambavyo malengo yake yalivyoainishwa, imekuwa ikifanya tafiti mbalimbali kuhusu elimu hapa nchini, lakini pia kwa kushirikiana na taassi nyingine za kimataifa ikiwa ni pamoja na kuratibu mikutano, maonesho na semina kuhusu masuala ya elimu.

Tuesday, August 01, 2017

MASAUNI AWATAKA WANAFUNZI VYUO VIKUU NCHINI KUONGEZA KASI YA UBUNIFU, AFUNGUA MAONYESHO YA SAYANSI CHUO CHA ST. JOSEPH DAR


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akikata utepe kuashiria kufungua Maonyesho Makubwa ya Sayansi na Teknolijia yaliyoandaliwa na wanafunzi wanaosoma fani ya uhandisi Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph, jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho, Dk. Prakabahran Anath. Masauni baada ya kuangalia kazi za ubunifu mbalimbali uliofanywa na wanafunzi hao, aliwataka wanafunzi hao kuongeza kasi zaidi ya kuongeza ubunifu kutokana na taaluma wanayoipata chuoni hapo.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa suti) akimsikiliza Mwanafunzi wa mwaka wanne fani ya uhandisi Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph cha jijini Dar es Salaam, Tumaini Lutufyo (kushoto) wakati alipokuwa anatoa maelezo ya gari la kuzima moto ambalo linatumia gesi lililotengenezwa na wanafunzi wa chuo hicho. Masauni alifungua Maonyesho ya Sayansi na Teknolojia chuoni hao ambapo aliangalia kazi mbalimbali za ubunifu uliofanywa na wanafunzi hao, pia aliwataka wanafunzi hao kuongeza kasi zaidi ya kuongeza ubunifu kutokana na taaluma wanayoipata chuoni hapo 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiliendesha gari linalotumia umeme wa jua lililotengenezwa na wanafunzi wa fani ya uhandisi Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph cha jijini Dar es Salaam. Masauni alifungua Maonyesho ya Sayansi na Teknolojia chuoni hao ambapo aliangalia kazi mbalimbali za ubunifu uliofanywa na wanafunzi hao, pia aliwataka wanafunzi hao kuongeza kasi zaidi ya kuongeza ubunifu kutokana na taaluma wanayoipata chuoni hapo .
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph cha jijini Dar es Salaam, mara baada ya kufungua Maonyesho ya siku mbili ya Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na Chuo hicho kwa lengo l kuonyesha ubunifu mbalimbali wa wanafunzi hao. Masauni baada ya kuangalia kazi za ubunifu mbalimbali uliofanywa na wanafunzi hao, aliwataka wanafunzi hao kuongeza kasi zaidi ya kuongeza ubunifu kutokana na taaluma wanayoipata chuoni hapo. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph cha jijini Dar es Salaam, Dk. Prakabahran Anath alipokua anatoa historia ya chuo hicho kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri huyo kufungua Maonyesho Makubwa ya Sayansi na Teknolijia yaliyoandaliwa na wanafunzi wanaosoma fani ya uhandisi chuoni hapo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKAGUA MIRADI WILAYA YA MBEYA MJINI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Methadone Clinic ambao ni maalum kwa kuwahudumia na kuwapa ushauri nasaha waathirika wa madawa ya kulevya kwenye . hospitali ya Rufaa ya Mbeya Julai 31, 2017. Kushoto ni Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_7118
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa  Salim Jessa  (wanne kushoto) ambaye ni  Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Malumalu kilichopo Iyunga jijini Mbeya  wakati alipoembelea kiwanda hichi Julai 31, 2017.  Watatu kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_7147
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa  Salim Jessa  (kulia) ambaye ni  Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Malumalu kilichopo Iyunga jijini Mbeya  wakati alipoembelea kiwanda hicho Julai 31, 2017. Kushoto kwake ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_7255
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipokea maua kutoka kwa mtoto , Felista (4) wa Shule ya Wenye Ulemavu ya Child Support Tanzania ya jijini Mbeya baada ya kuwasili kwenye kiwanda cha vinywaji baridi cha SBS – PEPSI kilichopo eneo la Iyunga jijini Mbeya Julai 31, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_7266
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na watoto wa Shule Wenye Ulemavu ya Child Support Tanzania ya jijini Mbeya baada ya kuwasili kwenye kiwanda cha vinywaji baridi cha SBS- Pepsi kilichopo Iyunga jijini Mbeya Julai 31, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_7364
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha vinywaji baridi  cha SBS- Pepsi kilichopo eneo la Iyunga jijini Mbeya, Julai 31, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_7413
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wakazi wa Mbeya baada ya kuwasili kwenye Viwanja vya  Ruanda Nzove jijini humo kuhutubia mkutano wa hadhara, Julai 31, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_7422
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta jambo na Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_7441
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Viwanja vya  Ruanda Nzove jijini Mbeya Julai 31, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MANISPAA YA KINONDONI YAKABIDHIWA SHULE YA SEKONDARI MAENDELEO


Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Benjamin Sitta akizungumza na watumishi  wa serikali na wanafunzi mapema jana katika hafla ya kupokea msaada wa shule ya sekondari ya Maendeleo yenye thamani ya sh milioni 800 iliyojengwa na kampuni ya magari ya (KIA) ya Korea Kusini na Good Neighbors jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Good Neighbour ambao ndio wadhamini wa shule hiyo, Namun Heo akizungunza na watumishi wa serikali katika hafla ya kukabidhi majengo ya shule ya sekondari ya Maendeleo yenye thamani ya sh milioni 800 iliyojengwa na kampuni ya magari ya (KIA) ya Korea Kusini na Good Neighbors, jijini Dar es Salaam. 
Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Benjamin Sitta (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Good Neighbour,Namun Heo (kulia) wakisani hati ya makabidhiano ya shule ya sekondari ya Maendeleo iliyojengwa na kampuni ya magari ya (KIA) ya Korea Kusini na Good Neighbors,mapema jana jijini Dar es Salaam.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta (wa kwanza kushoto) akiwa ameambata na watumishi wa serikali wakikagua moja ya majengo ya shule hiyo. 

Muonekano wa shule ya sekondari ya Maendeleo yenye thamani ya sh milioni 800 iliyojengwa na kampuni ya magari ya (KIA) ya Korea Kusini na Good Neighbors jana jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii.

JAFO APONGEZA MSHIKAMANO WA VIONGOZI NA WATENDAJI RORYA

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikata utepe na kuweka jiwe la msingi katika shule ya sekondari Nyamtinga wilayani Rorya. 
Baadhi ya vyumba vya madarasa vilivyokaguliwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo. 
Mbunge wa Vitimaalum Agnes Marwa akizungumza na wananchi wakati wa ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo. 
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa Rorya na kuwapongeza kwa ujenzi wa madarasa na mabweni. 

……………………………………………………………….. 
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo amewapongeza viongozi na watendaji wa wilaya na halmashauri ya wilaya ya Rorya kwa mahusiano mazuri waliyonayo katika kuwaletea wananchi maendeleo. 
Jafo alitoa sifa hizo alipokuwa wilayani humo kwa ziara ya kikazi ya kukagua miradi na kuongea na watumishi .

Katika ziara hiyo, Jafo alifanikiwa kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa, mabweni, maabara, na vyoo kwa sekondari ya Nyamtinga na Nyamunga ambapo majengo hayo yamebainika kujengwa kwa ubora wa kuridhisha. 

Ujenzi wa miundombinu hiyo imegharimu zaidi ya sh.milioni 500 kutoka serikali kuu kwa lengo la kuboresha elimu hapa nchini
Kwa upande wake,Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara, Agness Marwa amempongeza Naibu Waziri huyo kwa kufika wilayani Rorya na kwamba amekuwa Waziri pekee aliyefanikiwa kutembelea wilayani humo katika kipindi hiki cha serikali ya awamu ya tano. 

Mbunge huyo ameishukuru serikali kwa upendo wake wa kuisaidia wilaya hiyo miradi ya maendeleo. Naibu Waziri Jafo leo amekamilisha ziara yake ya kikazi ya siku sita ya kukagua miradi ya maendeleo na kuongea na watumishi kwa mkoa wa Kagera na Mara na anaendelea na ziara yake katika mikoa mingine.

TAWIRI YASHIRIKI MKUTANO WA KIMKAKATI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

Mkurugenzi Mkuu TAWIRI Dkt. Eblate Mjingo ni miongoni mwa Wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii wanaoshiriki  mkuta...