Monday, March 02, 2015

TASWIRA YA MKUTANO WA PAMOJA WA VYAMA VINAVYOUNDA UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI UKAWA JIJINI WASHINGTON DC, MAREKANI

Viongozi wa Vyama vya CUF na CHADEMA wakiwa pamoja katika mkutano jijini Washington DC.
Mbunge wa Mji Mkongwe Zanzibar Mh Ismail Jussa akiwa katika mkutano wa Pamoja wa Vyama vinavyounda umoja wa Katiba UKAWA jijini Washington DC.
Viongozi wa CUF na CHADEMA DMV wakiwa na Mgeni rasmi Mh Ismail Jussa.
Kutoka Kushoto ni Mbunge wa Mji Mkongwe Zanzibar Mh Ismail Jussa, wa pili ni Mh Shamis ambaye ni Mwenyekiti wa CUF DMV, wa tatu ni Mwenyekiti wa CHADEMA DMV Kalley Pandukizi na wa nne ni Katibu wa Tawi la CHADEMA DMV Liberatus Mwang’ombe.
 
Katibu wa Tawi la CHADEMA DMV Liberatus Mwang’ombe akiongea katika Mkutano wa pamoja unaunganisha vyama vya CUF na CHADEMA.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA DMV Kalley Pandukizi akiongea kabla ya Kumpisha Mgeni Rasmi Mh Ismail Jussa.
 
Mh Jussa akiwa na Mwenyekiti wa Tawi la CHADEMA DMV Kalley Pandukizi.
Viongozi wa CHADEMA na CUF DMV wakiwa na Mh Jussa katika Picha ya Pamoja kuonyesha Mshikamano wa Vyama vyao.
Kutoka kushoto ni Katibu Mwenezi wa Tawi la CHADEMA DMV Ndugu Hussein Kauzela, katikati ni Mh Ismail Jussa na Kulia ni Katibu wa CHADEMA DMV katika picha ya pamoja kuonyesha mshikamano.
Mwenyekiti wa CUF DMV Ndugu Shamis akiwa na Mwenyekiti wa Baraza la wanawake Ndugu Baybe Mgaza.
Katibu Mwenezi wa CHADEMA DMV Ndugu Hussein Kauzela akiwa na Mweka Hazina wa Tawi la CHADEMA DMV Ndugu Ludigo Mhagama.
Mh Ismail Jussa akiwa na Kada wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Salma Moshi.
Kwa Picha zaidi Bonyeza Read More

WASHINDI WA TIGO KILI HALF MARATHON WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO

TI1Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidaz Gama (kushoto), akimkabidhi hundi ya sh. Milioni 2, mshindi wa kwanza wa mashindano ya Tigo Kili Half Marathon Ismail Juma baada ya kushinda katika mashindano hayo yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ushirika Mkoani Moshi, katikati ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano pamoja na Mwenyekiti wa Chama Cha Mchezo wa Riadha Mkoa wa Kilimanjaro (KAA) Liston Metacha.
TI2Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidaz Gama (kulia) akifurahia jambo na Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano wakati wa mashindano ya Tigo Kili Half Marathon, yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ushirika Mjini Moshi.
TI3Washindi wa kwanza mpaka wa tatu wa mashindano ya Tigo Kili Half Marathon, kwa upande wa wanaume, wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Leonidaz Gama (kushoto), kulia ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano, akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Tanzania (RT) William Kalage pamoja na na Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Kilimanjaro (KAA) Liston Metacha.
TI4Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano (wa pili kushoto) akisoma risala katika mashindano ya fainali ya mashindano ya Tigo Kili Half Marathon, iliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ushirika Mjini Moshi, wa kwanza kushoto ni Ofisa Mawasiliano wa Tigo John Wanyancha, akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidaz Gama pamoja na Makamu Mwenyekiti wa RT William Kalage na Mwenyekiti wa KAA Liston Metacha.
TI5Mkurugenzi wa Kampuni ya simu ya Tigo Diego Gutierez (kushoto) akizungumza na Kaimu wake Cecile Tiano (katikati) pamoja Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini David Charles kabla ya kuanza kwa mashindano ya Tigo Kili Half Marathon yaliyofanyika juzi Mkoani Moshi.
TI01Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano (wa pili) kushoto, akiwa katika picha na baadhi ya viongozi wa kampuni hiyo kabla ya kuanza kwa mashindano ya Tigo Kili Half Marathon iliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ushirika Mjini Moshi.
TI02Washindi wa mashindano ya Tigo Kili Marathon, kwa upande wa Wanawake, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo, katika mashindano hayo yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo cha Ushirika Mjini Moshi.
TI03Washindi wa mashindano ya Tigo Kili Marathon, kwa upande wa Wanawake, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo, katika mashindano hayo yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo cha Ushirika Mjini Moshi.
TI04Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidaz Gama (kushoto), akimkabidhi hundi ya sh. 500,000 mshindi wa tatu Vicoty Chepkemei, baada ya kuibuka mshindi katika mashindano ya Tigo Kili Half Marathon kwa upande wa wanawake katika mashindano hayo yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ushirika Mjini Moshi, wa pili katikati ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Kilimanjaro (KAA) Liston Metacha na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Tanzania (RT) William Kalage.
TI05Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidaz Gama (kushoto), akimkabidhi hundi ya sh. Milioni 1 mshindi wa pili wa mashindano Tigo Kili Half Marathon, Eunice Echumba, katika mashindano hayo yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ushirika Mjini Moshi, wa pili katikati ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Kilimanjaro (KAA) Liston Metacha na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Tanzania (RT) William Kalage.
TI06Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidaz Gama (kushoto), akimkabidhi hundi ya sh.500,000 mshindi wa tatu Theophil Joseph, baada ya kuibuka mshindi katika mashindano ya Tigo Kili Half Marathon kwa upande wa Wanaume, katika mashindano hayo yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ushirika Mjini Moshi, wa pili katikati ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Kilimanjaro (KAA) Liston Metacha.

WAZIRI MKUU AENDELEA NA ZIARA MBOZI MKOA WA MBEYA

1Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wauguzi na madaktari ya hospitali ya mkoa wa Mbeya wakati alipofika hospitalini hapo kuwaona majeruhi wa ajali ya askari wa kutuliza ghasia iliyotokea  Februari 28, 2015 kati ya Mbeyana Chuna.
(Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)
2Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimfariji WP Cecilia  Mussa mmoja wa askari waliojeruhiwa akatika ajali ya gari iliyotokea katika  kijiji cha Chang’ombe  katika barabara ya barabara ya Mbeya Chunya Machi 1, 2015. Majeruhi hao wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Mbeya na hali zao ni nzuri.
4Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu  Pinda akimfariji WP Mwazanije Hassan  mmoja wa askari waliojeruhiwa akatika ajali ya gari iliyotokeakwenye kijiji cha Chang’ombe  katika barabara ya Mbeya Chunya Machi 1, 2015. Majeruhi hao wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Mbeya na hali zao ni nzuri.
6Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wananchi wa Vwawa , Mbozi akiwa katika ziara ya mkoa wa mbeaya Machi 1, 2015
789Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakitazama ngoma ya kabila la Wanyiha  wakati walipotembelea kiwanda cha kusindika kahawa cha CMS kilichopo Mbozi wakiwa katika ziara ya mkoa wa Mbeya Machi 1, 2015
10Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisikiliza maelezo kuhusu utafiti wa zao la kahawa kutoka kwa  Mtafiti Charles Mwingira wakati alipotembelea kituo cha utafiti wa kahawa cha Mbimba , Mbozi machi 1, 2015.
11Waziri Mkuu, Mizengo  Pinda akikagua shamba la mfano la kahawa fupi wakati alipotembelea kituo cha utafiti wa zao la kahawa akiwa katika ziara ya mkoa wa Mbeya Machi 1, 2015
13

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua maabara ya Shule ya Sekondari ya Vwawa akiwa kayioka ziara ya mkoa wa Mbeya Machi 1, 2015. Kushoto ni Mkuu  wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro.
15Waziri Mkuu, Mizengo Pindaq akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Vwawa  baada ya kufungua  maabara zao akiwa katika ziara ya mkoa wa Mbeya Machi 1, 2015
17Waziri Mkuu, Mizengo Pinda namkewe Tunu wakikagua sehemu ya shehena ya mahindi iliyohifadhiwa nje ya maghala ya NFRA, Vwawa, Mbozi Machi 1, 2015

Sunday, March 01, 2015

RAIS KIKWETE AIFARIJI FAMILIA YA MAREHEMU JOHN KOMBA LEO



Rais Jakaya Mrisho kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda yeye Mama Salma Kikwete kutoa pole na kuifariji familia ya Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Marehemu Kepteni John Komba aliyefariki dunia jana nyumbani kwa marehemu Mbezi kwa Komba jijini Dar es salaam leo March 1, 2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo walipokwenda yeye na Rais Kikwete kutoa pole na kuifariji familia ya Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Marehemu Kepteni John Komba aliyefariki dunia jana nyumbani kwa marehemu Mbezi kwa Komba jijini Dar es salaam leo March 1, 2015. 
Rais Jakaya Mrisho kikwete na mkewe Mama Salma kikwete wakimfariji familia ya Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Marehemu Kepteni John Komba aliyefariki dunia jana nyumbani kwa marehemu Mbezi kwa Komba jijini Dar es salaam leo March 1, 2015. 
Rais Jakaya Mrisho kikwete na mkewe Mama Salma kikwete wakiwafariji wasanii wa Tanzania One Theatre kufuatia kifo cha kiongozi wao, Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Marehemu Kepteni John Komba aliyefariki dunia jana nyumbani kwa marehemu Mbezi kwa Komba jijini Dar es salaam leo March 1, 2015.PICHA NA IKULU

RED BRIGADE WA CHADEMA, WALA KIAPO MBELE YA MBOWE, MWANZA


Vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, almaarufu kama RED BRIGADE, wakila kiapo cha utii, mbele ya Mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe, jijini Mwanza jana Jumamosi Februari 28, 2-015. Kiapo hicho kinafuatia kkamilika kwa mafunzo ya kiulinzi na usalama kwa vijana hao, ambapo nchi inaelekea kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu 2015.

Vijana hao wakila kiapo mbele ya Mbowe, (kulia).
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Wilfred Rwakatare (kulia), kiasoma taarifa ya mafunzo ya vijana wa chama hicho 'Red Brigedi' huku mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe (kushoto) akisikiliza kwa makini.

Vijana hao wakitoa heshima mbele ya Mwenyekiti wao Mbowe.PICHA KWA HISANI YA KIVIS BLOG

VIONGOZI MBALI MBALI WAHANI MSIBA WA KOMBA













Kapteni Komba afariki, aacha mjane na watoto 11

Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mkurugenzi wa Kikundi cha Tanzania One Theatre (TOT) Kapteni John Komba amefariki dunia jana alipokuwa akipelekwa katika hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam baada ya kuzidiwa.
Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na Hospitali ya TMJ, ofisi ya Bunge na Chama Cha Mapinduzi na kwamba kwa sasa taratibu za maziko yake zinaendelea kufanywa .
Aidha taarifa za hivi punde kutoka nyumbani kwake maeneo ya Mbezi Beach Tangi Bovu zinaeleza kuwa maelfu ya watu kutoka katika kada mbalimbali wanaendelea kumiminika nyumbani kwa marehemu ili kutoa faraja kwa familia kwani marehemu ameacha mjane mmoja na watoto kumi na moja.
Akizungumza na tovuti hii mmoja wa madaktari aliyempokea wakati anafikishwa hospitali ya TMJ, Dk Elisha Ishan amesema Komba alifikishwa hospitalini hapo saa 10 jioni jana akiwa mahututi .
"Nilimpokea nilianza moja kwa moja kumpima shinikizo la damu na vipimo vingine lakini tayari vilikuwa havifanyi kazi na hapo ndipo tukathibitisha kuwa ndugu yetu ameaga dunia," alisema Dk Ishan
Pamoja na hayo Dk Ishan amekwepa kutaja moja kwa moja chanzo cha kifo cha mareheme, hata hivyo amesea Kapteni Komba alikuwa na tatizo la shinikizo la damu na kwamba siku za karibuni alifika hospitalini hapo kwenye kiliniki yake ya shinikizo la damu.

MAKATIBU WAKUU WAKAGUA AICC MAANDALIZI YA MWISHO MKUTANO WA IPU, ARUSHA

Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali pamoja na Kamati ya Wataalamu ya Maandalizi ya Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), wamefan...