Monday, January 06, 2014

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda Aupokea mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dr. William Mgimwa uwanja wa ndege wa Nduli Iringa

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akishuhudia wakati mwili wa  aliyekuwa  Waziri wa Fedha, Dr. William Mgimwa wakati ulipowasili kwenye uwanja wa ndege  wa Nduli Iringa Desemba 5,2014 kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika  Desemba 6, 2014 kijijini  Magunga.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpa pole Jane Kakingo Mgimwa, mjane wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dr. William Mgimwa baada ya mwili wa marehemu kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Nduli Iringa  Desemba 5, 2014 kwa ajili ya mazishi  yanayotarajiwa kufanyika kijijini Magunga Desemba  6, 2014. 
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwafariji  wanafamilia wa aliyekuwa Waziri  wa Fedha, Dr. William Mgimwa baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu  katika kijiji cha  Magungua, Iringa kuwapa pole na kukagua maandalizi ya mazishi Desemba 5, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na  Bibi Jane Katingo, Mama Mzazi wa Aliekuwa Waziri wa Fedha, Dr. William Mgimwa wakati  alipokwenda  nyumbani kwa marehemu huyo katika kijiji cha Magunga, Iringa  kutoa pole na kuangalia maandalizi a mazishi  Januari 5, 2014
 Waziri mkuu, Mizengo  Pinda  akizungumza na   jamaa wa karibu wa aliyekuwa waziri wa Fedha, Dr. WilliamMgimwa baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu katika kijiiji cha Magunga, Iringa kuwapa pole wafiwa  na kukagua maadalizi ya  mazishi Desemba 5, 2014.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Friday, January 03, 2014

MHE ZITTO KABWE AIBWAGA CHADEMA KATIKA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA

 

Zitto Kabwe akiingia mahakama Kuu Dar es Salaam.  
 Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe (kulia) akitoka katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam jana, ambapo aliwasilisha ombi la pingamizi la yeye kutojadiliwa kwenye kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kinachotarajia kufanyika leo, hadi rufaa yake ya kupinga kuenguliwa wadhifa huo kwenye Baraza Kuu la chama hicho. Kushoto ni Wakili wa Zitto, Albert Msando. Mahakama Kuu imekubaliana na Zitto Kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kinachotarajiwa kufanyika kesho kutomjadili kwa namna yoyote.PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG  
Wanasheria wa Chadema, Tundu Lisu (kushoto) na Peter Kibatala waliofika

 kupinga hoja hiyo mahakamani. 
Tundu Lisu na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wakijadiliana jambo wakati wakisubiri uamuzi wa mahakama 
Zitto ana wakili wake Msando wakiwasiliana na marafiki zao walipokuwa wakisubili uamuzi wa mahakama, ambapo Zitto aliibuka dedea kwa pingamizi lake kukubaliwa hivyo kikao cha Kamati Kuu kinachofanyika kesho kukatazwa 

WANAKWAYA ARUSHA WALIPULIWA KWA BOMU

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas.
WANAKWAYA sita wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mt. Kalory Rwanga, Usa River, mkoani hapa, wamelazwa katika Hospitali ya Misheni na ya Tengeru, Arumeru baada ya kujeruhiwa kwa bomu.
Walikutwa na masahibu hayo juzi muda mfupi baada ya kutoka kanisani kwenye Mkesha wa Mwaka Mpya saa 6.30 usiku, meta 100 kutoka Kanisa hilo, eneo la Kisangani.
Mganga Msaidizi wa hospitali hiyo, iliyoko chini ya Kanisa Katoliki, Fredrick Mathew, alithibitisha jana kupokewa majeruhi watano, huku wawili wakiwa na hali mbaya na wengine wakiendelea vizuri.
Alitaja majeruhi hao kuwa ni Theresia Lesitare (33), Philipo Ambrose (22), Alphonce Nyigo (19), Mary Merikiory (40) na Anna Mathew (19) wote wakazi wa Lake Tatu, Usa River.
Majeruhi mwingine ambaye hali yake si nzuri, Annet Baltazar (16) amelazwa katika Hospitali ya Tengeru. Alisema majeruhi hao waliumia miguuni kwa kuchanwa na mlipuko huo na baadhi ya vipande vya bomu, vilitolewa kwenye miili yao na baadhi yao kushonwa kwa nyuzi kadhaa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alithibitisha kupata taarifa za tukio hilo na kueleza, kwamba uchunguzi wa tukio umeanza mara moja na atatoa taarifa ukikamilika.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana, Merikiory, alisema baada ya kutoka kanisani akiwa na wanakwaya wenzake, waliondoka kuelekea nyumbani, Lake Tatu.
Alisema wakiwa barabarani, waliona gari aina ya Toyota Land Cruiser likienda kwa kasi na lilipowakaribia, walisikia mlipuko na wakajikuta wamelala kando ya barabara huku baadhi yao wakivuja damu miguuni na tumboni.
Aliongeza kuwa gari hilo, halikusimama na lilipofika mbele waliokuwamo walifyatua mabomu ya kutoa machozi, kutawanya makundi ya watu mbalimbali waliokuwa wakionekana barabarani.
Alisema waliomba msaada kwa Paroko wa Kanisa hilo, Patrick Njau, ambaye alitoa gari na kuwapeleka Hospitali ya Misheni na wengine wakipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Tengeru kwa matibabu zaidi.
Askofu alia
Akizungumza huku akitokwa machozi baada ya kutembelea majeruhi, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha, Josephat Lebulu alisema ameshangazwa na tukio hilo. Alisisitiza kuwa Kanisa Katoliki, limechoka kuandamwa na matukio ya aina hiyo.
“Waumini wanakosa gani hadi watupiwe bomu, kwa nini polisi wako kimya hadi leo wasiseme? Kuna siri gani? Kwa nini kila siku ni Wakatoliki tu ndio wanapigwa mabomu, tunataka haki itendeke, watu wametoka kanisani usiku, wamekosa nini? Usalama uko wapi?” Alihoji.
Aliendelea: “Tumekosa nini, kupigwa mabomu kila siku hapa Arusha? Tumeshuhudia Olasiti, tukashuhudia Soweto sasa ni hapa Usa,” alisema. “Na kwa hili Kanisa hatutakubali hata kidogo, tunataka wahusika wawajibishwe na walioficha uovu huu wawajibishwe la sivyo viongozi walioficha uovu huu wawajibishwe, Mungu atasimama kwa ajili yetu,” alisema.
Mei mwaka jana, bomu lililorushwa liliua watu watatu na kujeruhi wengine zaidi ya 60 kwenye Kanisa
Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Parokia ya Olasiti, mjini Arusha.
Waumini walikuwa wamejumuika katika misa ya uzinduzi wa Kanisa hilo. Misa hiyo ilikuwa ikiongozwa na Balozi wa Vatican nchini na Mwakilishi wa Papa Francis, Askofu Francisco Padila kwa kushirikiana na Askofu Lebulu.
Taharuki Dar
Katika hatua nyingine, hali ya taharuki ilizuka jana maeneo ya Shekilango, Dar es Salaam baada ya kudaiwa kuwapo bomu la kurushwa kwa mkono kwenye eneo la njia ya waenda kwa miguu, karibu na eneo la ujenzi wa barabara ya Morogoro.
Gari la Polisi kutoka Kituo kidogo cha Urafiki, lilifika eneo hilo saa 4 asubuhi na kuzungushia mkanda wa hadhari eneo lililodaiwa kuwapo bomu.
Walifanya hivyo baada ya kupata taarifa kutoka kwa mpita njia, aliyeona kitu hicho kilichoelezwa kuwa ni bomu, ingawa baadaye taarifa ya Polisi ilisema halikuwa bomu.
Gazeti hili lilifika eneo la tukio na kushuhudia, ambapo polisi walilazimika kufukuza mamia ya watu waliokuwa wakimiminika kuliangalia, jambo ambalo ilikuwa hatari.
Alpha Sidadi (29) ambaye alikuwa wa kwanza kuona kifaa hicho, alisema ndiye aliwasiliana na polisi kuwaeleza juu ya kitu hicho.
Kwa mujibu wa Sidadi, alimsubiri mama yake, Asha Sidadi aliyekuwa akitoka Kinondoni na kumweleza kuwa waliwasiliana na polisi wanayefahamiana naye, aliyewasiliana na wenzake na kufika eneo la tukio.
Mama huyo alisema alipofika na kuelezwa na mwanawe na kuona kitu hicho kikiwa kama nanasi jeusi na aliwasiliana na polisi ambao walifika mara moja na kusema wanasubiri wataalamu wa kutegua mabomu.
Mmoja wa Polisi aliyefika eneo hilo, ambaye hakutaka jina lake litajwe, alikiri kitu hicho kufanana na bomu la kutupa kwa mkono. Alisema walikuwa wakisubiri wataalamu wathibitishe na akataka wananchi kuacha kukimbilia katika maeneo ya hatari kwa nia ya kutaka kushuhudia.
Juma Maulid ,mfanyabiashara wa maeneo hayo alidai waliwahi kukuta kifaa kama hicho katika eneo hilo.
Akizungumzia kuhusu suala hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura alisema tofauti na ilivyodhaniwa na watu wengi, kitu hicho hakikuwa bomu, isipokuwa ni mwanasesere mwenye umbo mfano wa bomu.
“Hata hivi sasa ninavyokueleza kipo hapa ofisini kwangu. Unajua siku hizi kuna vitu vinatengenezwa kwa mifano, mfano unaweza kukuta chupa za manukato zenye mfano wa bomu au wanasesere wa kuchezea watoto wenye mfano huo, ukweli kitu kile hakikuwa bomu kama ilivyodhaniwa,” alisema Wambura.
Alisema vitu vingi siku hizi vikiwamo vifaa vya kuchezea watoto, vimetengenezwa kwa maumbo mbalimbali.
CHANZO: HABARI LEO

MKWASA, PONDAMALI, KUINOA YANGA

Uongozi wa Young Africans SC umepata warithi wa nafasi tatu za benchi la ufundi (Charles Boniface Mkwasa, Juma Pondamali na Dr. Suphian Juma), huku wakiendelea na mchakato kumpata kocha mkuu ambaye atachukua nafasi ya mholanzi Ernie Brandts aliyesitishiwa mkataba wake mwishoni mwa mwaka 2013.
Charles Boniface Mkwasa 'Master' aliyekua kocha mkuu wa timu ya Ruvu Shooting katika mzunguko wa kwanza anachukua nafasi ya aliyekua kocha msaidizi Fred Felix "Minziro" ambaye muda wake umemalizika mwishoni mwa mwaka 2013.
Mkwasa ambaye aliichezea Young Africans miaka ya 80's kwa kiwango cha hali juu pia alishawahi kuwa Kocha Mkuu/Msaidizi kwa kikosi cha Jangwani kwa vipindi tofauti jambo ambalo linamfanya aiwe mgeni katika mitaa ya Twiga na Jangwani.
Kocha wa makipa wa timu ya Taifa Tanzania "Taifa Stars" Juma Pondamali "Mensah" anachukua nafasi ya aliyekua kocha wa makipa mkenya Razaki Siwa ambaye pia alistishiwa mkataba wake mwishoni mwa mwaka 2013.
Pondamali golikipa aliyeichezea Yanga miaka ya 80's kwa kwa kiwango cha hali ya juu hata kufikia kuwa katika kikosi cha Tanzania kilichoshiriki mashindano ya Mataifa Afrika nchini Nigeria mwaka 1980, sio mgeni katika timu ya Young Africans kwani awali alishwahi kuwa kocha msaidizi kwa vipindi tofauti.
Dr Suphian Juma anachukua nafasi ya Dr Nassoro Matuzya ambaye pia alisitishiwa ajira yake mwishoni mwa mwaka 2013 pamoja benchi la Ufundi.
Mara baada ya kuwapata viongozi hao watatu wa Benchi la Ufundi kikosi cha Young Africans kesho kitaanza mazoezi jioni katika Uwanja wa Bora Kijitonyama kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na mashindano ya Kimataifa huku kocha Mkwasa akiongoza benchi hilo la Ufundi mpaka atakapopatikana kocha mkuu ambaye watafanya watafanya kazi kwa pamoja.

JAJI WARIOBA AKUTANA NA JUKWAA LA WAHARIRI NCHINI (TEF) NA BARAZA LA HABARI (MCT)

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (kushoto) akikabidhi nakala za Rasimu ya Katiba kwa Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Neville Meena (katikati) wakati wa mkutano baina ya Tume hiyo na Jukwaa la Wahariri Nchini (TEF) uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar esa Salaam leo Alhamisi Januari 2, 2014. Anayeshuhudia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. Kajubi Mukajanga.

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji…
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (kushoto) akikabidhi nakala za Rasimu ya Katiba kwa Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Neville Meena (katikati) wakati wa mkutano baina ya Tume hiyo na Jukwaa la Wahariri Nchini (TEF) uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar esa Salaam leo Alhamisi Januari 2, 2014. Anayeshuhudia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. Kajubi Mukajanga.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (wa pili kulia) akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini wakati wa mkutano baina yake ya Jukwaa la Wahariri Nchini (TEF) uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Januari 2. 2014. Wengine Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. Kajubi Mukajanga, Katibu wa Tume, Assaa Rashid na Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mkuu mstaafu Augstino Ramadhani.
(PICHA NA TUME YA KATIBA).

Thursday, January 02, 2014

IGP ERNEST MANGU, NAIBU WAKE WAAPISHWA NA JK, DAR



Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Mkuu mpya wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Ernest Mangu, kwenye hafla iliyofanyika viwanja vya Ikulu, Jumanne jioni Disemba 31, 2013. Rais pia alimuapisha naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi (D-IGP), Abdulrahman O.J.Kaniki. nafasi hiyo ya D-IGP ni mpya. Katika hafla hiyo, Makamu wa rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, waziri wa nchi ofisi ya rais (Uratibu na Mahusiano ya Jamii), Steven Wasira, waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu (Bunge na Uratib), William Lukuvi, Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Mathias Chikawe na Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima walihudhuria. Halikadhalika wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, walikuwepo bila kuwasahau maafisa wote wa vyeo vya juu wa jeshi la polisi nao walihudhuria sherehe hiyo

D-IGP Kaniki alika kiapo mbele ya Amiri Jeshi Mkuu, Rais Kikwete

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Jakaya Kikwete, akiwasili eneo la tukio, Ikulu

Huyu ndiyo Ernest Mangu, IGP mpya

Huyu ndiyo Abdulrahman O.J Kaniki (D-IGP), mpya. Kaniki anakuwa mtanzania wa kwanza kushika cheo hicho kipya

D-IGP, Kaniki akifunga kamba za viatu kabla ya kuanza kwa kiapo

Rais Kikwete, makamu wa rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, IGP mpya Ernest Mangu (Watatu kulia) D-IGP Abdulrahman O.J.Kaniki (Kulia) na IGP aliyemaliza muda wake, Said Mwema (Kushoto)

JK akifanya mzaha na IGP wake Mangu

JK na familia ya Mangu

JK na familia ya Kaniki

JK na familia ya Mwema

JK na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama

IGP Mangu (Kulia) na D-IGP Kaniki

IGP Mangu akijibu maswali ya waandishi mara baada ya kuapa kushika wadhifa huo

JK akimpongeza D-IGP, Kaniki

JK akimkabidhi muongozo D-IGP, Kaniki

JK akipokea saluti kutoka kwa IGP Mangu

JK akimpongeza IGP Mangu

IGP Mangu akipokea kadi ya kumtakia heri kutoka kwa mtangulizi wake, Said Mwema

D-IGP, Kaniki, akipokea kadi ya kumtakia heri kutoka kwa bosi wake wa zamani IGP mstaafu Mwema, huku mama Mwema kulia na IGP mpya Mangu wakishuhudia

IGP Mangu akipokea shada la maua kutoka kwa mkewe wakati wa pongezi baada ya kula kiapo cha kushika wadhifa huo

RAIS KIKWETE AOMBOLEZA KIFO CHA DKT WILLIAM MGIMWA

Marehemu Dkt. William Mgimwa.…

Waziri Mkuu azindua boti mbili za doria na uokozi

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba ametoa siku 14 kwa wizara na taasisi zinazohusika na Kituo cha Kitaifa cha pamoja cha Oparesheni zipeleke w...