Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika
akitoka katika ukumbi wa Bunge la Tanzania leo mjini Dodoma baada ya
kukataa kufuta kauli ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kuwa dhaifu. Mbunge huyo alitoa kauli hiyo wakati akichangia
Bajeti ya serikali ya mwaka 2012/13 katika mkutano unaoendelea.
(Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dodoma)
Mbunge wa Jimbo la Ubungo John Mnyika akiteta na Mbunge wa jimbo la Wawi
Hamad Rashid Mohamed (kushoto) na Mbunge wa Bariadi Mashariki John
Cheyo mara baada ya kuondolewa Bungeni leo mjini Dodoma baada ya

Comments