Friday, January 02, 2015

FUNGA MWAKA YA JUMUIYA DMV YAFANA

 Aliyekuwa mwakilishi wa Diaspora bunge la katiba Mhe. Kadari Singo akielezea shughuli za bunge hilo na jinsi gani alivyopigana kutetea swala la uraia pacha huku akiwasihi wanaDiaspora kubadili mtizamo wao kwa nchi yao.
Mwakilishi wa maswala ya uhamiaji Bi. Fatmata Barrier akifafanua sera ya uhamiaji ya Obama kuhusiana na kutoa vibali vya kazi kwa wasiokua na makaratasi kwenye sherehe ya mkesha ya Jumuiya ya Watanzania DMV iliyofanyika Lanham, Maryland Jumamosi Desemba 31, 2014.
Mgeni Rasmi Balozi wa African Union Mhe. Amina Salum Ali (wapili kushoto) akiwa pamoja na Balozi Mstaafu Mhe. Mustafa Nyang;anyi, Rais wa Jumuiya ya Wanzania DMV bwn. Iddi Sandaly na Mkuu wa Utawala na Fedha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Mama Lily Munanka.
 Watanzania wakifuatialia wasemaji wa maswala mbalimbali yakiwemo maswala ya bunge la katiba na maswla ua uhamijai kwenye sherehe ya kuaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka 2015 iliyofanyika ndani ya ukumbi wa Oxford Center uliopo Lanham, Maryland.
Mwenyekiti wa CCM tawi la DMV bwn. George Sebo akiwa na mkewe Aunty Grace(kulia) wakiwa na wageni wao kwenye sherehe ya Jumuiya ya Watanzania DMV ya kuuaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka 2015 iliyofanyia Lnham Maryland nchini Marekani.
Bwn. Jacob Kinyemi na mama mwenye nyumba wake na wakijumuika na wanajumuia wengine katika kusherehekea kuukaribisha mwaka 2015.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi



MBUNGE WA MOROGORO MJINI MH ABOOD ATOA MILION 11 KUTATUA KERO YA MAJI MKUNDI MOROGORO

 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akizindua Tawi la CCM la Wajasiriamali Bodaboda na Mama lishe lililopo Mgulu wa Ndege Kata Ya Mkundi Manispaa ya Morogoro.Mara Baada ya Kuzindua Tawi Hilo Mh Abood Aliongea na Wanachama wa Tawi Hilo Kisha Kuwaelekeza Kujiunga Kwenye Vikundi vya Wajasiriamali Yeye Atakuwa Tayari kuwawezesha Mitaji ya Kufanya Shuguli za Kujiletea Maendeleo.
 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akiwa Meza Kuu Sambamba na Katibu wa CCM Kata Ya Mkundi tayari Kusikiliza Kero zinazowakabili wakati wa Kata Hiyo Ambapo walimwambia Wanakabiliwa na Kero Kubwa ya Umeme,Maji na Barabara.Aidha Mh Abood Akitoa Majibu Kuhusu Kero Hizo Alesema Kuhusu Umeme Serikali Imeiweka Kata Hiyo Kwenye Bajeti ya Serikali ya Mwaka huu .Kuhusu Maji Mh Abood alitoa Shilingi Milioni 11 Kwajili ya Kununua Vifaa vya Kuwezesha Kufikisha Maji katika eneo la Mgulu wa Ndege Kata ya Mkundi.Pia Alitoa Shilingi Milion 2 kwajili ya Mafuta Ili Greda la Manispaa ya Morogoro Kuweza Kuchonga Barabarfa Zote za Kata Hiyo.
 Mwenyekiti wa Mtaa wa Mgulu wa Ndege Kata ya Mkundi Jimbo la Morogoro Mjini Akisoma Risala yake Kwa Mbunge wa Jimbo Hilo
Mh Aziz Abood.
 
Mmoja wa Wakazi   wa Kata ya Mkundi waliojitokeza Kwa Wingi Kwenye Ziara ya Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Akieleza Kwa msisitizo Kero Kubwa Inayowakabili wakazi wa Kata Hiyo                   
 
 
  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akiandika Baadhi ya Keo ambazo wananchi wa Kata ya Mkundi walimweleza wakati wa Ziara yake ya kutembelea Kata za Jimbo la Morogoro Mjini.
 Wakazi wa Kata ya Mkundi wakimsikiliza kwa Makini Mbunge wao
Wakazi wa Kata ya Mkundi wakimshangilia Mh Abood mara Baada ya Kutatua kero Kubw ya kata hiyo tatizo la Maji. 
  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akijibu Baadhi ya Kero zinazowakabili wakazi wa Kata ya Mkundi.

Rais Jakaya Kikwete Asherekea na Wananchi Katika Kuukaribisha Mwaka Mpya 2015 Kijijini Msoga, Chalinze, Mkoa wa Pwani

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mbunge  wa Chalinze Mhe Ridhiwani Kikwete wakijumuika na wananchi katika kuukaribisha mwaka mpya kijijini Msoga, Chalinze, Mkoa wa Pwani.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mbunge  wa Chalinze Mhe Ridhiwani Kikwete wakijumuika na wananchi katika kuukaribisha mwaka mpya kijijini Msoga, Chalinze, Mkoa wa Pwani.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa neno la shukurani kwa  Mashekhe wa Bagamoyo na wananchi  kwa kumuandalia  hafla ya kumuombea dua katika mkesha wa mwaka mpya kijijini Msoga, Chalinze, Mkoa wa Pwani
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na viongozi wa jamii ya wamasai wanaoishi mkoa wa Pwani. Kiongozi mkuu wa jamii hiyo, Laiboni Tikwa Moreto (wa pili kushoto), Majaliwa Lihalei na Zuberi Tangono katika hafla ya  kuukaribisha mwaka mpya kijijini Msoga, Chalinze.Picha na IKULU

SERIKALI YARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA KITUO CHA KISASA CHA UTALII KUSINI, KUKAMILIKA DESEMBA

  Na Mashaka Mhando, Iringa UJENZI wa kituo cha kisasa cha utalii mkoani Iringa, kinachotarajiwa kuwa mkombozi na kiungo muhimu cha kukuza u...