Wednesday, April 01, 2026

WATENGENEZA MAUDHUI MTANDAONI WATAKIWA KUTENGENEZA MAUDHUI YANAYOLINDA TASWIRA YA NCHI

 

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana iliyopo mkoani Mwanza, Mhe. Amina Makilagi {pichani juu] amewataka Watengeneza Maudhui Mtandaoni kuzingatia maadili, uzalendo pamoja na kulinda taswira ya Tanzania kwenye maudhui wanayoyatengeneza.

Mhe. Amina ametoa rai hiyo Aprili 1, 2026 mkoani hapo wakati akizungumza kwenye Mafunzo kwa Watengenza Maudhui Mtandaoni (Content Creators) awamu ya kwanza yaliyoandaliwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. 

“Msisitizo kwenu watengeneza maudhui, mafunzo mliyoyapata hapa yasiishie hapa bali yatumieni katika kuboresha kazi zenu ili muweze kuongeza kipato cha familia na Taifa kwa ujumla” alisistiza Mhe. Amina.

Aidha, amewataka washiriki hao kuongeza ujuzi kupitia njia mbalimbali ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania, CPA (T) Nyakaho Mahemba amesema kuwa, lengo la mafunzo hayo ni kuwasaidia wazalisha maudhui mtandaoni kupata elimu ya mkopo, uandishi wa mradi pamoja na namna ya kuzalisha kazi bora zaidi zitakazokidhi soko la ndani na nje pamoja na kuweza kuweka ushindani.

Naye Bw. Andrew Ngonyani (Brother K) aliyeshiriki mafunzo hayo aliishukuru Serikali kwa kutoa mafunzo hayo ambayo yamewasaidia vijana wengi kuweza kutumia maudhui yao kupata pesa, akiishauri Serikali kuendelea kuweka mazingira bora kwa wasanii kufanya sanaa na kunufaika nayo.

Mafunzo hayo yamekuwa na mada mbalimbali ikiwemo Elimu ya Mtaji, Kubiasharisha Maudhui Mtandaoni, Uaminifu uwajibikaji kwa wafuasi wako pamoja na hatua kwa hatua namna ya kutengeneza akaunti ya biashara na kuingiza kipato.










NCHIMBI AKISALIMIANA NA BABA MTAKATIFU BAADA YA IBADA YA HIJA VATICAN

 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, akisalimiana na Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Baba Mtakatifu Leo XIV, mara baada ya Ibada ya Hija iliyofanyika katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro – Vatican, leo tarehe 01 April 2026.




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akifurahi jambo na Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Baba Mtakatifu Leo XIV, wakati wakiagana mara baada ya Ibada ya Hija iliyofanyika katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro – Vatican leo tarehe 01 Aprili 2026.

RAIS SAMIA AKUTANA NA WAGOMBEA URAIS: ASISITIZA UMOJA, DEMOKRASIA NA MAENDELEO ENDELEVU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Wagombea wa Nafasi ya Urais na Wagombea Wenza kutoka vyama vya Siasa 16 vilivyoshiriki Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Oktoba, 2025. Mazungumzo hayo yalifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 31 Machi, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Wagombea wa nafasi ya Urais pamoja na Wagombea Wenza wa Vyama vya Siasa 16 vilivyoshiriki Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Oktoba, 2025 mara baada ya Mazungumzo yao, Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 31 Machi, 2026.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Wagombea wa nafasi ya Urais Wanawake ambao ni Saum Hussein Rashid kutoka chama cha UDP na Mwajuma Noty Mirambo kutoka chama cha UMD walioshiriki Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Oktoba, 2025 mara baada ya mazungumzo yao, Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 31 Machi, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na Wagombea wa nafasi ya Urais pamoja na Wagombea Wenza kutoka vyama vya siasa 16 vilivyoshiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, katika mazungumzo yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 31 Machi, 2026.

Mkutano huo umebeba uzito wa kipekee katika kuendeleza misingi ya demokrasia jumuishi, maridhiano ya kisiasa, na mshikamano wa kitaifa. Kupitia majadiliano hayo, viongozi hao walipata fursa ya kubadilishana mawazo, kujenga uelewano wa pamoja, na kuweka msingi imara wa ushirikiano kwa maslahi mapana ya Taifa.

Rais Samia alisisitiza umuhimu wa siasa za ustaarabu, kuheshimu tofauti za kiitikadi, na kuweka mbele maslahi ya wananchi. Alieleza kuwa maendeleo endelevu hayawezi kupatikana bila kuwepo kwa mazingira ya amani, utulivu na mshikamano wa kisiasa.

Kwa upande wao, wagombea walionesha utayari wa kushirikiana na Serikali katika kujenga Taifa lenye umoja na lenye kulenga maendeleo ya kiuchumi na kijamii, wakitambua nafasi yao katika kuimarisha demokrasia na uwajibikaji.

Hatua hii inaakisi dhamira ya dhati ya uongozi wa juu wa nchi katika kukuza diplomasia ya ndani (internal political diplomacy) na kuimarisha misingi ya utawala bora. Ni ishara kwamba Tanzania inaendelea kusonga mbele kwa umoja, kwa misingi ya kazi, utu, na mshikamano wa kitaifa.

#KaziNaUtuTunasongaMbele #TabasamuLaUtu #MaendeleoEndelevu #DiplomasiaYaKiuchumi

WATENGENEZA MAUDHUI MTANDAONI WATAKIWA KUTENGENEZA MAUDHUI YANAYOLINDA TASWIRA YA NCHI

  Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana iliyopo mkoani Mwanza, Mhe. Amina Makilagi {pichani juu] amewataka Watengeneza Maudhui Mtandaoni kuzingatia ...