Mmoja  wa waombolezaji akipitishwa juu juu kwenye vichwa vya waombolezaji ili  kupata huduma ya kwanza baada ya kuzirai, katikati anayetazama mbele ni  Mussa Kisoky Mkurugenzi wa kampuni ya Sofia Production ya jijini Dar es  salaam.
Rais  wa Shirikisho la wasanii wa Filamu Saimon Mwakifwamba akizungumza  katika msiba huo kutoa salamu zao za rambirambi kwa marehemu Steven  Kanumba
Askari wa kike wakiweka sawa utaratibu wa waombolezaji kupita katika eneo hilo ili kukaa.
Ndugu  wa karibu wakielekea sehemu waliyotengewa kukaa.
Jeneza la mwili wa marehemu Kanumba likiwa limewekwa tayari kwa waombolezaji kutoa heshima zao za mwisho
Kundi maalum lililoandaliwa kwa nyimbo za maombolezo likiimba nyimbo za maombolezo katika katika msiba huo.Mama wa Marehemu Steven Kanumba Flora Mtegoa akiwa katika hali ya majonzi mwisho kushoto ni Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka akimfariji Mama Kanumba
Kutoka  kulia ni Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel  Nchimbi, Ridhiwan Kikwete, Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Idd Azzan na  waombolezaji wengine wakiwa katika msiba huo.
Mbunge  wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi akipiga sal;ute mbele ya jeneza lenye  mwili wa marehemu Steven Kanumba kama ishara ya kumkubali kwake na kutoa  heshima kwa marehemu Steven Kanumba.
Makamu  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Gharib Bilal akitoa  heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu Steven Kanumba ulioagwa leo  kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam huku viongozi  mbalimbali wa Serikali, viongozi wa dini, Wanasiasa, Wanamuziki  Waigizaji na watu maarufu wamejitokeza kuuaga mwili wa mwigizaji huo  aliyekuwa maarufu zaidi nchini Tanzania na nje ya  nchi pia, Marehemu Steven Kanumba anazikwa mchana huu kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam

Jeneza lenye Mwili wa Marehemu,Steven Kanumba likiwasili kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam asubuhi hii. Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Steven Kanumba asubuhi hii kwenye viwanja vya Leaders Club,Jijini Dar es Salaam.akifuatiwa na Mkewe,Pamoja na Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete (mwenye nguo nyeupe kulia). Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu akitoa heshima za mwisho.
Mmoja wa waombolezaji akisidiwa na wafanyakazi wa msalaba mwekundu mara baada ya kuzimia katika msiba huo mkubwa.
Picha zote hizi ni kwa hisani ya
http://www.fullshangweblog.com
Picha zote hizi ni kwa hisani ya
http://www.fullshangweblog.com


