Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Jacquline Maleko akimfafanulia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kushoto), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Ernest Mangu (kushoto) na Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova (kulia) jinsi Mamlaka hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi walivyojipanga kuimarisha usalama katika Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (aliyevaa tai) akiongozwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Soko la Ndani, Edwin Rutageruka (watatu kulia) kuelekea kuangalia usalama katika sehemu mbalimbali ya Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba). Nyuma ya Waziri Chikawe upande wa kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu na Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova (wapili kulia). Waziri Chikawe na Maafisa wa Jeshi la Polisi wametembelea viwanja hivyo vilivyopo Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, kuangalia hali ya usalama katika viwanja hivyo.Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akikiangalia cheti cha usajili wa vyama katika Banda la Wizara yake wakati wa Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu. Waziri Chikawe na Maafisa wa Jeshi la Polisi wametembelea viwanja hivyo vilivyopo Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, kuangalia hali ya usalama katika viwanja hivyo. Kushoto ni Afisa Sheria, Flora Mlope ambaye alikuwa akitoa maelezo ya usajili wa vyama. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.aziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akitoka kwenye Banda la Wizara yake wakati wa Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Soko la Ndani, Edwin Rutageruka na kulia ni Afisa Habari wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christina Mwangosi. Waziri Chikawe na Maafisa wa Jeshi la Polisi wametembelea viwanja hivyo kuangalia hali ya usalama. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma
Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
No comments:
Post a Comment