Wednesday, May 30, 2018

BUNGE LAPITISHA BAJETI YA WIZARA YA ARDHI KWA MWAKA WA FEDHA 2018/19

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi na Naibu wake; Angeline Mabula wakiwa na watendaji wa Wizara na Taasisi katika picha ya pamoja baada tu ya kupitishwa kwa bajeti ya Wizara ya Ardhi.
 Baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakifuatilia kwa kina bajeti ya Wizara wizara hiyo ilipokuwa ikiendelea kujadiliwa mapema leo asubuhi.

 Baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakifuatilia kwa kina bajeti ya Wizara wizara hiyo ilipokuwa ikiendelea kujadiliwa mapema leo asubuhi.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi na Naibu wake; Angeline Mabula wakiwa na watendaji wa Wizara na Taasisi katika picha ya pamoja baada tu ya kupitishwa kwa bajeti ya Wizara ya Ardhi.

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi na Naibu wake; Angeline Mabula wakiwa na watendaji wa Wizara na Taasisi katika picha ya pamoja baada tu ya kupitishwa kwa bajeti ya Wizara ya Ardhi.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi na Naibu wake; Angeline Mabula wakiwa na watendaji wa Wizara na Taasisi katika picha ya pamoja baada tu ya kupitishwa kwa bajeti ya Wizara ya Ardhi.

Monday, May 28, 2018

WAZIRI LUKUVI AFUNGUA MAONYESHO YA SIKU TATU YA SEKTA YA NYUMBA

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akielekea katika eneo la Maonyesho ya siku tatu ya sekta ya nyumba yanayoratibiwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Shirika la Nyumba la Taifa kwaajili ya kuwaelimisha wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya nyumba, kulia kwake ni Dk. Raphael Chegeni na nyuma yake ni Mbunge wa Jimbo la Manyoni Magharibi, Yahya Masare.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akikaribishwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi katika eneo la Maonyesho ya siku tatu ya sekta ya nyumba yanayoratibiwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Shirika la Nyumba la Taifa kwaajili ya kuwaelimisha wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya nyumba,
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akijadiliana jambo na Meneja wa Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa, Itandula Gambalagi na Meneja wa NHC mkoa wa Dodoma, Joseph John katika eneo la Maonyesho la viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya siku tatu ya sekta ya nyumba yanayoratibiwa na Shirika la Nyumba la Taifa kwaajili ya kuwaelimisha wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya nyumba,
Baadhi ya Wadau wa sekta ya nyumba wakiwa katika eneo la Maonyesho ya siku tatu ya sekta ya nyumba yanayoratibiwa na Shirika la Nyumba la Taifa kwaajili ya kuwaelimisha wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya nyumba. 
Mbunge wa Viti Maalumu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete akielekea kwenye eneo la Maonyesho ya Sekta ya Nyumba yanayofanyika katika viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akizungumza na Naibu Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde kuhusiana na masuala mbalimbali ya sekta ya nyumba.

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akitembelea banda la maonyesho la Benki ya Azania leo asubuhi.



Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akizungumza na Naibu Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa kuhusiana na masuala mbalimbali ya sekta ya nyumba.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Independent Planners Limited, Clemence Mero kuhusiana na masuala mbalimbali ya sekta ya nyumba wakati alipotembelea banda la maonyesho la IPL.

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Independent Planners Limited, Clemence Mero kuhusiana na masuala mbalimbali ya sekta ya nyumba wakati alipotembelea banda la maonyesho la IPL. 

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akielekea katika eneo la Maonyesho ya siku tatu ya sekta ya nyumba yanayoratibiwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Shirika la Nyumba la Taifa kwaajili ya kuwaelimisha wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya nyumba, kushoto kwake ni Dk. Raphael Chegeni 
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akizungumza na Naibu Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde kuhusiana na masuala mbalimbali ya sekta ya nyumba.

Friday, May 25, 2018

KAIMU MKURUGENZI MKUU AAGIZA MAREKEBISHO YA KODI NHC KONGWA ILI NYUMBA ZIPANGISHWE KULIINGIZIA MAPATO SHIRIKA

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Felix Manyama Maagi akielekea kwenye mojawapo ya nyumba za makazi za NHC Kongwa leo asubuhi.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Felix Manyama Maagi akielezwa jambo na Meneja wa NHC mkoa wa Dodoma,  Joseph John wakati Kaimu Mkurugenzi Mkuu alipofanya ziara kwenye nyumba za makazi za gharama nafuu Kongwa.  Kaimu Mkurugenzi Mkuu ameagiza kurekebishwa kwa kiwango cha kodi cha nyumba hizo ili ziweze kupangishika na kuliongezea Shirika mapato.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Felix Manyama Maagi akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa NHC mkoa wa Dodoma  wakati Kaimu Mkurugenzi Mkuu alipofanya ziara kwenye nyumba za makazi za gharama nafuu Kongwa.  Mkurugenzi Mkuu ameagiza kurekebishwa kwa kiwango cha kodi cha nyumba hizo ili ziweze kupangishika na kuliongezea Shirika mapato.
 Nyumba za makazi za gharama nafuu NHC Kongwa znavyoonekana kwa sasa zipo nyumba 44, za vyumba vitatu na viwili zilizokamilika tayari kwa matumizi ya makazi ya watu.

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Felix Manyama Maagi akielekea kwenye mojawapo ya nyumba za makazi za NHC Kongwa leo asubuhi.



 Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara, William Genya akieleza jambo wakati wa ziara hiyo iliyofanyika leo asubuhi kwenye makazi hayo ya gharama nafuu.



Friday, May 18, 2018

WAZIRI LUKUVI, MWENYEKITI WA KAMATI NAPE WAMWAGA SIFA UTENDAJI WA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akiongozana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Nape Moses Nnauye na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya siku moja ya miradi mbalimbali ya Shirika. Katika Ziara hiyo Waziri Lukuvi amesifia kasi ya utendaji wa Shirika la Nyumba la TAifa huku Mwenyekiti wa Kamati wa Ardhi, Maliasili na Utalii akisema Shirika hilo ni mfano wa kuigwa kwa utendaji wenye viwango ikilinganishwa na mashirika mengi nchini.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi  akizungumza na Arden Kitomari wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya siku moja ya miradi mbalimbali ya Shirika. 
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii, wakifuatilia maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi.
 Kaimu Mkurugenzi wa Ubunifu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Margreth Ezekiel akiwaeleza Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii, maendeleo ya ujenzi wa jengo la biashara na makazi la Morocco Square linalojengwa na NHC Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Nape Moses Nnauye akiongozana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya siku moja ya miradi mbalimbali ya Shirika. 
Msanifu wa Majengo wa Shirika la Nyumba la Taifa, Robert Kintu akiwaeleza Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii, maendeleo ya ujenzi wa jengo la biashara na makazi la Victoria linalojengwa na NHC Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akielezea mbele ya Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii juu ya utendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa. Kamat hiyo ilifanya ziara ya siku moja ya miradi mbalimbali ya Shirika.


 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akiwaelekeza wajumbe wa kamati kuelekea kwenye mradi wa Morocco Square NHC jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Nape Moses Nnauye akiongozana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya siku moja ya miradi mbalimbali ya Shirika. 


 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akijadiliana jambo na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge  ya Ardhi, Maliasili na Maliasili wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya siku moja ya miradi mbalimbali ya Shirika. 
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Nape Moses Nnauye akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa, Haikamen Mlekio katika ziara iliyofanyika leo mchana katika miradi ya Shirika la Nyumba la Taifa.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi  akijadiliana jambo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi na Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa, Haikamen Mlekio katika ziara iliyofanyika leo mchana katika miradi ya Shirika la Nyumba la Taifa.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akiweleza maendeleo ya mradi wa Morocco Square jijini Dar es Salaam leo.
Jengo la Morocco Square linavyoonekana kwa sasa

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akikagua miundombinu ndani ya jengo la Morocco.

Monday, May 14, 2018

KATIBU MKUU WA WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI DOROTHY MWANYIKA AFUNGUA KIKAO CHA BARAZA KUU NHC


Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dorothy Mwanyika akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa kinachofanyika leo jijini Dar es Salaam kinachojadili kwa mapana masuala ya utendaji kazi, maslahi ya wafanyakazi, utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Miaka 10 wa Shirika na kujadili bajeti ya Shirika na utekelezaji wake. Kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi na Kushoto kwake ni Katibu wa Baraza la Wafanyakazi, Mecktilda Mihayo na Wa kwanza Kushoto ni Naibu Katibu wa Baraza la Wafanyakazi, Adolf Kasegenya.

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dorothy Mwanyika akishiriki wimbo wa pamoja wa wafanyakazi maarufu kama "Solidarity Forever"na Viongozi wa Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Felix Manyama Maagi (wa pili kushoto) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, kushoto ni Katibu Msaidizi wa Baraza hilo, Adolph  Kasegenya na kulia ni Katibu wa Baraza, Mecktilda Mihayo wakazi wa kikao cha baraza hilo kinachofanyika kwa siku mbili makao makuu ya 
Shirika hilo Kambarage House.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dorothy Mwanyika akisindikizwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Felix Manyama Maagi (katikati) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, kulia ni Katibu Msaidizi wa Baraza hilo, Adolph  Kasegenya baada ya ufunguzi wa kikao cha baraza hilo kinachofanyika kwa siku mbili makao makuu ya Shirika hilo Kambarage House.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa  huku Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dorothy Mwanyika . Kulia kwake ni Katibu wa Baraza la Wafanyakazi, Mecktilda Mihayo na Kushoto ni Naibu Katibu wa Baraza la Wafanyakazi, Adolf Kasegenya.


 Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dorothy Mwanyika akisindikizwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Felix Manyama Maagi (katikati) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, kulia ni Katibu Msaidizi wa Baraza hilo, Adolph  Kasegenya baada ya ufunguzi wa kikao cha baraza hilo kinachofanyika kwa siku mbili makao makuu ya Shirika hilo Kambarage House.

 Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dorothy Mwanyika akisindikizwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Felix Manyama Maagi (katikati) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, kulia ni Katibu Msaidizi wa Baraza hilo, Adolph  Kasegenya baada ya ufunguzi wa kikao cha baraza hilo kinachofanyika kwa siku mbili makao makuu ya Shirika hilo Kambarage House.
Picha ya pamoja ya Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dorothy Mwanyika na baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa
 


Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dorothy Mwanyika akisindikizwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Felix Manyama Maagi (katikati) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, baada ya ufunguzi wa kikao cha baraza hilo kinachofanyika kwa siku mbili makao makuu ya Shirika hilo Kambarage House.


HOTUBA YA KATIBU MKUU WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI, DOROTHY MWANYIKA KWENYE UFUNGUZI WA KIKAO CHA BARAZA KUU LA WAFANYAKAZI LA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC), JIJINI DAR ES SALAAM TAREHE 14/05/2018.

Ndugu Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC na  Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Wafanyakazi,  Felix Manyama Maagi,

Ndugu Wakurugenzi wa Shirika,

Ndugu Wajumbe wa Baraza,

Ndugu Wageni Waalikwa,

Ndugu Wanahabari,

Mabibi na Mabwana.

Nianze kwa kueleza faraja yangu kwa mapokezi yenu mliyonipa na kuishukuru Menejimenti ya Shirika kwa kunipa heshima ya kuja kuwafungulia kikao hiki cha Baraza Kuu la Wafanyakazi. Nawashukuru kwasababu tukio hili la leo linanipa fursa ya kukutana na watendaji wakuu na wawakilishi wa wafanyakazi kutoka mikoa yote ya Shirika kwa mara ya kwanza tangu niteuliwe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara yetu. Hivyo, ni fursa kwangu kuweza kufikisha ujumbe kwa wafanyakazi na umma juu ya Shirika letu.

Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe, kwanza kabisa naomba nitumie fursa hii kuwapa pole wote mliosafiri safari ndefu ya kuja hapa Dar es Salaam. Tumshukuru Mungu kwa kuwawezesha kufika hapa salama salimini.

Pili, Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe, nimeelezwa kwamba ajenda za kikao Baraza hili zimejielekeza katika masuala ya utendaji wa Shirika. Aidha, nimeelezwa kuwa kikao chenu kitapitia mizania ya hesabu za Shirika kwa mwaka wa fedha 2018/2019, pamoja na kujadili taarifa za utekelezaji wa kazi mlizozipanga kuendana na Mpango Mkakati wenu. Naupongeza sana utaratibu huu maana unaleta mezani utekelezaji wa majukumu ya kazi na kuanisha changamoto mnazokumbana nazo kwa nia ya kuzipatia ufumbuzi sahihi kwa pamoja.

Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe, Sina haja ya kusisitiza umuhimu wa ajenda zote hizi zilizoko mbele yenu, kwani naamini wajumbe wote wa Baraza hili mnatambua umuhimu wake. Hivyo ni matarajio yangu kuwa ajenda hizi, ambazo zinagusa uhai na maendeleo ya Shirika letu, mtazijadili kwa kina ili hatimaye muweze kutoka na maazimio ya msingi yatakayoliwezesha Shirika hili kuongeza tija na kukidhi matarajiyo ya umma wa Watanzania ambayo kwa sasa yako juu sana kutokana na imani mliyowajengea.


Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe, Baraza hili ni jukwaa muhimu sana mahala pa kazi kwani ni kiunganishi kati ya Menejimenti na Wafanyakazi. Ni matumaini yangu kuwa mtaendelea kushirikiana ili kuleta ufanisi kwa Mamlaka na Taifa kwa ujumla. Hata hivyo ikumbukwe kuwa Serikali inazingatia sana suala la taasisi zake kuwa na mabaraza ya Wafanyakazi kwani yalianzishwa kisheria kwa madhumuni ya kuishauri Serikali katika ngazi za idara, taasisi na Wizara kuhusu usimamizi wa kazi na rasilimali watu, utekelezaji wa majukumu, kulinda haki na wajibu wa waajiri na wafanyakazi, kutoa ushauri kuhusu kujenga hali bora za kazi, maslahi ya Wafanyakazi na kusimamia haki na ustawi katika sehemu za kazi. Wajibu wa mabaraza haya kama vyombo vya ushauri na usimamizi ni kuhakikisha kuwa waajiri na watumishi wanatambua wajibu na haki zao, pia wanazingatia maadili ya utumishi wao ili kuleta matokeo ya utendaji wa kazi yenye tija, staha na upendo.

Kadhalika, niwapongeze kwa kutengeneza na kisha kuufanyia mapitio Mpango Mkakati wa miaka kumi ambao mkiufanyia kazi na kuutekeleza kwa wakati mtaleta mabadiliko makubwa katika sekta ya nyumba hapa nchini. Nimesoma Mpango Mkakati huo kwa makini na kuyapitia malengo yote sita mliyojiwekea.

Nataka niwaambie kuwa malengo haya siyo mepesi, ni mazito na yanahitaji uwajibikaji wa hali ya juu ili kuweza kuyatekeleza kwa ufanisi la sivyo yatabaki kwenye makaratasi. Hivyo, nitoe rai kwenu kuwa muweke mbele maslahi ya Shirika na ushirikiano mkubwa ili muyafikie malengo yenu. Wakati nikiwapongeza kwa kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kutekeleza Mpango Mkakati huu wa miaka kumi (2015/16-2024/25), ni vema mkajua kuwa Serikali imewapa dhamana kubwa ya kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya nyumba. Shirika lina changamoto ya kuhakikisha kuwa linakuwa na uwezo wa kifedha ili kuweza kutekeleza mikakati ya ujenzi wa nyumba hizi hasa nyumba za gharama nafuu. Niseme tu kuwa Wizara inaungana nanyi katika kuhahakikisha kuwa yale yote ambayo yanahitaji msukumo wa Wizara yanatekelezwa ili kuweza kufikia malengo mliyojiwekea kwa wakati.

Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe, Nipende kuwakumbusha kwamba Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kwa dhati, katika ujenzi wa uchumi wa viwanda ili kuchochea mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya watu. Lengo kuu la Mpango huo ni kuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati inayoongozwa na viwanda ifikapo mwaka 2025. Ni dhahiri, Shirika la Nyumba mtachochea azma hii ya viwanda kwa kuongeza kasi ya ujenzi wa nyumba na tija katika ujenzi.

Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe, kupitia hotuba yangu, napenda kuwahamasisha muendeleze ushirikiano na mabenki kutoa elimu ya mikopo ya nyumba ili kuwawezesha watanzania wengi zaidi kutumia fursa zilizopo za mikopo ya benki kununua nyumba zinazojengwa na Shirika. Itakuwa fahari kubwa kwa mwananchi kumiliki majengo ya ofisi, biashara na makazi katikati ya miji na Halmashauri zetu zinazojengwa na NHC.

Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe, sitaki kuwachosha hata kabla hamjaanza kazi nzito iliyoko mbele yenu. Hivyo, naomba niishie hapa kwa kuishukuru tena Menejimenti kwa kunialika kuja kufungua kikao chenu hii leo. Aidha, naomba nimalizie kwa kuwatakia wajumbe wote safari njema mtakaporejea majumbani na sehemu zenu za kazi.

Baada ya kusema haya sasa napenda kutamka kuwa kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi kwa mwaka 2018, kimefunguliwa rasmi.  Asanteni sana kwa kunisikiliza.