Friday, July 11, 2014

ZIARA YA DKT JOHN POMBE MAGUFULI MKOANI DODOMA

 Waziri wa Ujenzi Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli leo amefungua Mradi wa Taa za kuongozea Magari katika mji wa Dodoma.Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng.Musa Ibrahim Iyombe Mradi huo ambao umefanywa na wakandarasi Wazawa umegarimu shilingi Milioni 384.Mataa yaliyozinduliwa jana ni yaliyopo ANJIA PANDA ya Barabara ya Nyerere na Mpwapwa na yale yaliyopo njia panda ya Barabara ya Area D na barabara  ya kuelekea Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma  Dkt.Rehema Nchimbi kulia akimkaribisha  Waziri wa Ujenzi,Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli Kufungua Mradi wa Taa za kuongozea Magari Mjini Dodoma.
 Waziri wa Ujenzi,Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Mradi wa Taa za kuongozea Magari Mjini Dodoma.
 Waziri wa Ujenzi,Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli akifunguwa pazia la jiwe la msini wakati wa kufungua  Mradi wa Taa za kuongozea Magari Mjini Dodoma.
 Mkuu wa Mkoa akimpongeza Waziri Magufuli
Magari yakipita katika mataa mara baada ya Waziri wa Ujenzi,Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli Kufungua Mradi wa Taa za kuongozea Magari Mjini Dodoma katika makutano ya barabara ya Nyerere na Mpwapwa.
Vikundi vya ngoma na nyimbo kutoka JKT Makutopora vikitoa burudani wakati Waziri wa Ujenzi Dkt.John Magufuli akizindua mradi wa mataa ya kuongozea magari mjini Dodoma.(Mhe.Maguguli ambaye alipitia JKT Makutopora amewazawadia Shilingi laki tatu baada ya kuvutiwa na burudani ya vikundi hivyo.
 Vikundi vya ngoma na nyimbo kutoka JKT Makutopora vikitoa burudani wakati Waziri wa Ujenzi Dkt.John Magufuli akizindua mradi wa mataa ya kuongozea magari mjini Dodoma.(Mhe.Magufuli ambaye alipitia JKT Makutopora amewazawadia Shilingi laki tatu Baada ya kuvutiwa na burudani ya vikundi hivyo.
 Ngoma 
 Kwaya

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...