Wednesday, July 09, 2014

TBL YATOA MSAADA WA SH. MIL. 25 ZA KUCHIMBA KISIMA CHA MAJI ZAHANATI YA MAKUBURI, DAR

 Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kinondoni, Joseph
Nicholous (kushoto) akimkabidhi Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, 
ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Dk. Gunini Kamba mfano
wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 25 ikiwa ni msaada uliotolewa na TBL
kwa ajili ya ujenzi wa kisima cha maji katika Zahanati ya Makuburi, Dar
es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika zahanati hiyo.
Kulia ni Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo, Stella Kivugo na katikati ni
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mwongozo katika kata hiyo ya
Makuburi. James Ngoitanile.
 Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni,  ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Dk. Gunini Kamba (wa pili kulia) akimkabidhi  mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 25 Mkurugenzi wa Kampuni ya Drima Drilling, Mhandisi Amiri Msangi msaada uliotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa ajili ya ujenzi wa kisima cha maji katika Zahanati ya Makuburi, Dar es Salaam katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki  katika zahanati hiyo. Kulia ni Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo, Stella Kivugo na katikati ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mwongozo katika kata hiyo ya Makuburi.James Ngoitanile.
 Jengo la zahanati ya Makuburi
 Viongozi wa Manispaa ya Kinondoni,viongozi wa na wahudumu wa zahanati hiyo pamoja na Wajumbe wa kamati ya maji ya mtaa huo Mwongozo wakifurahia kupata msaada huo kutoka TBL.
Ofisa  Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu akielezea mikakati ya kampuni hiyo kutoa sehemu ya faida ya mauzo ya vinywaji vyao kuwapatia wananchi misaada ya maji nchini.
 Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Dk. Kamaba akitoa shukrani kwa TBL kwa msaada huo wa kisima cha maji.
 Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo, Kivugo akitoa shukrani kwa TBL kwa kuwapatia msaada wa kisima cha maji na kwamba kitendo hicho kitawapunguzia kwa asilimia kuwa tatizo la maji lililokuwa linaikumba zahanati hiyo.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Mkazi wa Makuburi, akielezea kwa hisia kufurahishwa na msaada huo wa TBL  kwa wakazi wa eneo hilo.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...