Tuesday, January 30, 2018

Wajasiliamaji watakiwa kuendelea kutengeneza bidhaa bora kujenga uchumi wa Tanzania

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bathow Mmuni ambaye alikuwa mgeni rasmi akifunga mfunzo ya wajasiliamali yaliyoendeshwa na Sido mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Mkurugenzi wa Sido Dar es Salaam, MacDonald Maganga. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bathow Mmuni akiwa ameshika chaki iliyotengenezwa na wajasiliamali waliokuwa waliopata mafunzo ya Sido-Dar es Salaam. 
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bathow Mmuni akionyeshwa nguo ya batiki iliyotengenezwa na wajasiliamali waliokuwa waliopata mafunzo ya Sido-Dar es Salaam. 
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bathow Mmuni akionyeswa mafuta na sabuni walizotengeneza wajasiliamali waliopata mafunzo ya Sido-Dar es Salaam. Pembeni ni Mkurugenzi wa Sido Dar es Salaam, MacDonald Maganga. 
Mjasiliamali Suleiman Nassoro Mohamed ambaye ni Katibu wa BAKWATA akisoma risala wakati wa hafla ya kuhitimu mafunzo.
Baadhi ya wajasiliamali wakipatiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo. 
Wajasiliamali wakiwa katika picha ya pamoja.

. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji NSSF, Bathow Mmuni wakati akifunga mfunzo ya Sido yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam ambapo aliwataka wajasiliamali kuendelea kuwa wabunifu kwa kutenegeza bidhaa zenye ubora.

 "Nawaomba wajasiliamali mtengeneze bidhaa zenye ubora na nzuri zitakazowavutia wateja ili mtakapoziuza zitachangia pato la taifa kukua zaidi," alisema Mmuni. Aliongeza kuwa kwa sasa NSSF wamejipanga kurudi kuanza kuwasaidia wajasiliamali ili kukuza kipato chao ili waweze kuendeleza uchumi wa viwanda. Kwa upande wa Mkurugenzi wa Sido- Dar es Salaam, MacDonald Maganga aliwaomba wajasiliamali wote walipo mtaani kuchangamkia mafunzo ya Sido ili yaweze kuwaongezea ujuzi na kuzifanya bidhaa zao zikawa na thamani zaidi.

"Wajasiliamali jitokezeni kokote pale mlipo mchangamkie mafunzo tunayoyatoa maana yamekuwa yakiwajenga zaidi kwa kuongeza ubora wa bidhaa mnazozitengeneza, ukiangalia katika kundi lenu hili kuwa watu wameshaanza kutengeneza bidhaa ila wamekuja kujiongezea ujuzi zaidi jambo ambao ni jema zaidi maana unapopata cheti cha Sido kitakusaidia kuweza kupenya katika soko," alisema Maganga.

Zawadi kem kem promosheni ya Jero Yako ya Zantel

 Meneja Masojo wa Zantel, Bi.  Rukia Mtingwa (kulia) akikabidhi zawadi ya simu ya kisasa aina ya Moto C 4G toka Zantel kwa Bwana Moiz Johar Hussein Hassanali  mmoja wa washindi wa wiki wa promosheni ya ‘Jero yako tu’ ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam ambayo mteja wa Zantel  akiongeza muda wa maongezi kuanzia shs mia tano hujipatia nafasi kushiriki. Zawadi za pikipiki, baiskeli, simu na pesa taslimu hutolewa kila wiki.
 Meneja Masoko wa Zantel, Bi. Rukia Mtingwa akizungumza katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mshindi huyo Bwana Moiz Johar Hussein Hassanali .
 Meneja Masoko wa Zantel, Bi. Rukia Mtingwa (kulia) akipiga simu kwa  kwa simu na mmoja wa washindi wa promosheni ya Jero yako ya Zantel huku mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kuabahatisha Jehud Ngolo (kushoto) akisikiliza pamoja na mfanyakazi mwingine wa Zantel katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Zantel mjini Zanzibar, Mohammed Mussa Baucha (kulia), akikabidhi zawadi ya simu kwa Taimur Mohamed Hussein  mmoja wa washindi wa promosheni ya Jero yako, kisiwani humo juzi.

MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE(CSEE) NA MAARIFA(QT) 2017

Friday, January 26, 2018

KATIBU MKUU WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI ATEMBELEA USA RIVER NA SAFARI CITY AFURAHISHWA NA MPANGILIO WA MIRADI HIYO

Katibu Mkuu akipata maelezo ya mradi wa Usa River Satellite City kutoka kwa Meneja wa Mradi, James Kisarika.
 
 Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mama Dorothy Mwanyika, ametembelea Miradi ya Safari City na Usa River Satellite City, iliopo katika Jiji la Arusha na kufurahishwa na mpangilio wa miradi yote miwili. Amehimiza uongozi wa NHC kusimamia miradi hiyo kuhakikisha kwamba matarajio ya wateja katika kuwekeza pesa zao kwa ununuzi wa viwanja na baadaye kujenga nyumba, yanatimia.
 Katibu Mkuu, Mama Dorothy Mwanyika akiongozana na Meneja wa Singida, Ndugu Nistas Mvungi na Meneja wa Arusha, Ndugu Bamanyisa, akipokelewa Safari City na Meneja wa Mradi, Ndugu James Kisarika.
 Katibu Mkuu akiongozwa na Meneja Mradi kuingia katika ofisi ya Mradi.
 Picha ya pamoja ya Katibu Mkuu na viongozi aliofuatana nao,  kutoka ofisi ya Mkoa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Vitengovya Ardhi na Usajili wa Hati.
 Viongozi wa Shirika Mikoa ya Arusha na Singida pamoja na wa Wizara wakitafakari maswala yahusuyo maendeleo ya mradi wa Safari City.

 Meneja wa Mradi, James Kisarika, akitoa maelezo ya jumla kuhusu maendeleo ya Safari City.
 Katibu Mkuu na viongozi wengine akisikiliza mawasilisho kwa makini.


 Afisa Mipango Miji wa Shirika la Nyumba la Taifa, Devota Zephrine, akielezea mpangilio wa Mji wa Safari City.
                 
Katibu Mkuu akikagua nyumba za mfano.
Afisa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa, Loreen Uronu, akielezea maendeleo ya mauzo ya viwanja Safari City.
 Viongozi wakiikiliza mawasilisho kwa makini.
 Mwanasheria wa Mradi, Neema Mapunda, akiwasilisha mada kuhusu utaratibu wa kusimamia usagi na ulinzi katika Mji wa Safari City ikiwa ni pamoja na kuanzisha umoja wa Wamiliki nyumba.
 Katibu Mkuu akitoa nasaha zake baada ya mawasilisho ya mradi. Alikiri kufurahishwa na mpangilio wa mradi na kuahidi kwamba Wizara ipo pamoja na Shirika katika uendelezaji huu na kwamba wadau kama TARURA washirikishwe pia katika ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami na kushirikisha watumiaji kwa njia ya "road tolls charges".
 Katibu Mkuu awasili Usa River Satellite City.


 Katibu Mkuu afurahia maelezo kuhusu mkakati wa uendelezaji mradi wa Usa River. Akiri uwekezaji wa Shirika katika mradi huo ni mzuri. Mradi unao miundo mbinu yote muhimu kama maji na umeme tayari na uko karibu kabisa na barabara kuu ya Arusha Kuelekea KIA na Moshi.
 Katibu Mkuu akizungumza na viongozi wote baada ya maelezo ya mradi.
 Katibu Mkuu akipata maelezo kuhusu hatua za uendelezaji wa mradi wa Usa River.
 Viongozi wa Shirika Mkoa na wa Wizara Kanda ya Kaskazini, wakifurahia mafanikio ya ziara ya Katibu Mkuu wa wizara ya Ardhi. Viongozi hao ni pamoja na Mameneja wa Arusha na Singida na  Kamishina Msaidizi wa Ardhi.
Picha ya pamoja. Mpango  wa uendelezaji mji wa Usa River utabakiza asilimia 95% ya miti yote ilopo kwa sada ili kuhakikisha mji unabakia kijani na wenye mandhari ya kipekee kabisa. Tunasema karibu tena Katibu Mkuu.

Wednesday, January 24, 2018

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA LAKABIDHI NYUMBA ZA MAKAZI 63 ZA IYUMBU SATELLITE CENTER KWA UHAMIAJI

Meneja wa Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa, Itandula Gambalagi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa na Kamishna wa Fedha, Ndugu Peter Chogero kwa niaba ya Kamishna Mkuu wa Uhamiaji wakikabidhiana hati ya makabidhiano ya nyumba baada ya kukabidhi nyumba 63 kwa Jeshi la Uhamiaji.
 Picha ya pamoja ya uongozi wa Shirika la Nyumba na Uhamiaji baada ya makabidhiano ya nyumba 63 za makazi katika mradi wa Iyumbu Satellite Center. Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limekabidhi nyumba za makazi zilizojengwa kwenye mradi wa kitovu cha mji wa kisasa wa nyumba za gharama nafuu wa Iyumbu Satellite Centre kwa Idara ya Uhamiaji.
 Picha ya pamoja ya uongozi wa Shirika la Nyumba na Uhamiaji baada ya makabidhiano ya nyumba 63 za makazi katika mradi wa Iyumbu Satellite Center. Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limekabidhi nyumba za makazi zilizojengwa kwenye mradi wa kitovu cha mji wa kisasa wa nyumba za gharama nafuu wa Iyumbu Satellite Centre kwa Idara ya Uhamiaji.
Wafanyakazi na uongozi wa Jeshi la Uhamiaji wakiwa wameshika mfano wa ufunguo baada ya makabidhiano ya nyumba 63 za makazi katika mradi wa Iyumbu Satellite Center. Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limekabidhi nyumba za makazi zilizojengwa kwenye mradi wa kitovu cha mji wa kisasa wa nyumba za gharama nafuu wa Iyumbu Satellite Centre kwa Idara ya Uhamiaji.

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo limekabidhi nyumba za makazi zilizojengwa kwenye mradi wa kitovu cha mji wa kisasa wa nyumba za gharama nafuu wa Iyumbu Satellite Centre kwa Idara ya Uhamiaji.
Mradi huu ambao ujenzi wake ulianza Desemba 2016 una ukubwa wa ekari 234 na ni moja ya sehemu ya mji uliopangiliwa kitaalamu kwa kuzingatia sheria na kanuni za mipango miji na utajengwa katika awamu tatu. Nyumba hizi 63 ambazo zimeshakamilika na kuanza kukaliwa zinakabidhiwa leo kwa Idara ya Uhamiaji.
Makabidhiano haya yamefanywa na Meneja Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa, Ndugu Itandula Gambalagi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NHC na Kamishna wa Fedha, Ndugu Peter Chogero kwa niaba ya Kamishna Mkuu wa Uhamiaji.
Makabidhiano haya yanafanyika baada ya ahadi ya Shirika la Nyumba kwa Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli ya kujenga nyumba makao makuu ya nchi Dodoma.
Katika uzinduzi wa nyumba hizi, Mkurugenzi Mkuu wa NHC alimhakikishia Mh. Rais kwamba nyumba hizi zimekamilika na ziko tayari kwa kukaliwa.
Leo ni siku ya furaha kuona kwamba NHC inakabidhi nyumba kwa Uhamiaji ambaye ni mmoja wa wanunuzi wakubwa wa nyumba katika mradi huu.
Nyumba hizi ni bora kabisa zimejengwa kwa ustadi mkubwa. Ni wito wetu kwamba nyumba hizi watazitunza ikiwa na mazingira yake.
Mradi huu wa nyumba 300 ikiwa 150 zimekamilika ni kati ya miradi mingi ambayo NHC inatekeleza.

Saturday, January 13, 2018

DC ALI HAPI AZIPONGEZA DAWASA NA DAWASCO KWA USIMAMIZI MZURI UTEKELEZAJI WA UJENZI WA MIRADI YA UBORESHAJI MAJI

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Mhe., Ali Hapi, (katikati), akiteremka kutoka juu ya tenki kubwa la kuhifadhia maji linalojengwa huko Mabwepande nje kidogo ya jiji, wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya maji wilayani kwake Januari 13, 2018.
  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

MKUU wa wilaya ya Kinondoni Mhe. Ali Hapi, amewataka wakandarasi wanaotekeleza ujenzi wa mradi wa uboreshaji wa huduma za ugawaji na usambazaji maji wilayani kwake kuongeza kasi ya kukamilisha mradi huo kama ambavyo mkataba unaelekeza.
Mhe. Hapi aliyasema hayo leo Januari 13, 2018 mwishoni mwa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundomnbinu hiyo inayohusisha matenki makubwa manne na vituo vinne vya kusukuma maji (Booster Stations) ikiwa ni pamoja na utandikaji  wa mabomba ya kusafirisha maji.
Mradi huo ambao unatekelezwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka jijini Dar es Salaam, (DAWASA), ni sehemu ya mradi mkubwa wa uboreshaji wa huduma za ugawaji na usambazaji maji katika baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Pwani,  Dar es Salaam, sehemu ya mikoa ya Morogoro na Tanga na ulianza kutekelezwa mwezi Machi 2016.
“Mradi huu ulipaswa kuwa umekamilika Novemba mwaka jana, lakini hatua waliyofikia baadhi ya maeneo wako asilimia 80, mengine asilimia 75 na mengine asilimia 50, ahadi yao ni kwamba ndani ya kipindi kifupi kijacho wataweza kukamilisha mradi huu.” Alisema
Hata hivyo Mheshimiwa Hapi amepongeza usimamizi na ufuatiliaji wa karibu unaofanywa na mamlaka husika zinzosim amia mradi huo. “Niwapongeze DAWASA na DAWASCO kwa kazi nzuri ya kuhakikisha wanasimamia na kufuatilia utekelezaji wa mradi huu.” Alisema Mhe. Hapi.
Alitaja maeneo yatakayofaidika na mradi huu kuwa ni pamoja na wakazi wa Makongo, Changanyikeni, Salasala, Bunju, Mabwepande na Wazo.
“Mradi ukikamilika utaondoa kero ya maji katika wilaya yetu  kwa asilimia 95, kwa hivyo, hii nifaraja kubwa kwa wananchi wa Kinondonbi hususan katika maeneo nilkiyoyataja.” Alifafanua. Mhe. Hapi, akimsikiliza Mkandarasi,   Mhandisi P.G. Rajani wa kampuni ya WAPCOS limited ya India, alipotembelea sehemu ya ujenzi wa mtambo wa kusukuma maji huko Salasala jijini Dar es Salaam.
 Mhe. Hapi, akimsikiliza Mkandarasi,   Mhandisi P.G. Rajani(kulia) wa kampuni ya WAPCOS limited ya India, alipotembelea sehemu ya ujenzi wa tenki kubwa la kuhifadhia maji huko Salasala jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Modester Mushi kaimu mkurugenzi wa ufundi DAWASA.
 Mhe. Hapi na msafara wake wakipanda juu ya tanki linalojengwa.
 Mafundi wakiwa kazini huko Salasala.
 Mhe. Hapi akipokelewa na Meneja Uhusiano wa Jamii, DAWASA, Bi. NMelly Msuya, wakati akiwasili huko Makongo Juu, kuanza ziara ya kukagua miradi hiyo.
 Meneja Uhusiano wa Jamii, Bi. Nelly Msuya, (wapilia kushoto) na Afisa Uhusiano wa Jamii wa DAWASA, Bi. Mecky Mdakju, wakimsubiri Mkuu wa wilaya Mhe. Hapi, alipozuru eneo la Makongo Juu kukagua ujenzi wa kituo cha kusukuma maji.
 Mhe. Hapi, (kulia), akifurahia jambo na afisa kutoka DAWASCO, Bi.Judith Singinika(katikati), baada ya kutembelea eneo la ujenzi Bunju.
 Tenki kubwa likifunikwa huko Salasala.
 Mhe. Hapi, (kushoto), akiwa na Bi.Modester Mushi kaimu mkurugenzi wa ufundi DAWASA, (kulia) na Bi. Nelly Msuya, Meneja Uhusiano wa Jamii, DAWASA, walipotembelea ujenzi wa kituo cha kusukuma maji Bunju.
 Mkuu wa wilaya akizungumza na vibarua.


 Mkuu wa Wilaya Mhe. Hapi, akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa ziara hiyo, huko Mabwepande.
Bi.Mecky Mdaku, Afisa Uhusiano wa Jamii, DAWASA, akipanda juu ya tenki la Makongo Juu lililofikia asilimia 80 kukamilika.