Wednesday, July 16, 2014

MBUNGE KABATI ATEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO

3
Mganga Mfawishi wa Hospitali ya wilaya ya Frelimo Dk. Hassan Mtani akitoa taarifa kuhusu hospitali hiyo mbele ya mbunge wa Viti maalum CCm Lita Kabati
4 
Baadhi ya wahudumu wa hospitali ya Frelimo
6
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Iringa kwa tiketi ya chama cha mapinduzi(CCM), Lita Kabati akikagua mradi wa barabara kiwango cha lami katika eneo la Ngome
7
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Iringa kwa tiketi ya chama cha mapinduzi(CCM), Lita Kabati akishiriki katika ujenzi wa mitaro ya maji katika barabara ya ngome. (Picha zote na Denis Mlowe)
……………………………………………………………………
Na Denis Mlowe,Iringa
MKOA wa Iringa umeanza kutekeleza mkakati wa serikali wa Matokeo Makubwa Sasa ili kuwaletea wananchi maendeleo ya haraka katika sekta za Kilimo, Maji, Elimu, Uchukuzi, Nishati na Madini, na Uwezeshaji wa wananchi kupitia miradi ambayo imetekelezwa kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2013/2014.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Iringa kwa tiketi ya chama cha mapinduzi(CCM), Lita Kabati ametembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya mkakati wa matokeo makubwa sasa ili kujua maendeleo yake pamoja na changamoto zilizopo.
Mmoja wa mradi aliotembelea ni mradi wa ujenzi wa barabara kiwango cha lami katika eneo la Mkimbizi, Kihesa hadi Tumaini uliogharimu sh. bilioni 1.8 wenye km 2.5
Mradi mwingine uliotembelewa ni mradi wa ujenzi wa machinjio ya kisasa yaliyoko Ngelewala yaliyopo katika kata ya Isakalilo yaliyogharimu sh. Bilioni 1.4 na hadi sasa matengenezo yake yakiwa yamegharimu nusu ya fedha hizo na ujenzi unaendelea mradi uliopangwa kutekelezwa kwa awamu tano.
Mradi huo wa machinjio ulianzishwa baada ya Halmashauri kuona machinjio iliyopo haikidhi mahitaji ya uchinjaji kwa sasa ikiwemo kuchakaa kwa miundombinu,kuwa jirani na makazi ya watu,kuwa na eneo dogo la uchinjaji kutokana na ongezeko la hali ya uchinjaji.
Aidha mbunge Kabati alitembelea mradi wa hospitali ya wilaya ya Frelimo ambayo inafanya kazi na wagonjwa wameshaanza kuitumia baada ya kukamilika na moja ya hospitali zinaztoa huduma bora za meno
Akizungumza katika mrejesho wa majumuisho ya ziara hiyo Lita Kabati alisema kuwa amelidhishwa na maendeleo yaliyopo kulingana na fedha iliyotumika katika kufanikisha miradi hiyo.
Alisema mradi wa machinjio unatakiwa kupiganiwa zaidi ili uweze kukamilika kwani utasaidia kuwapatia ajira vijana zaidi ya 200 mara baada ya kukamilika kwake.
Mbali na hayo alisema kuwa wabunge wanapaswa kujua fedha zinazoletwa kwa ajili ya miradi inaendana na mradi wenyewe kutokana na kuwa fedha nyingi zimekuwa zikitumika tofauti na nyingine kupotea.
Kabati aliahidi kuwa atashirikiana na manispaa kwa kuhakikisha wanafatilia miradi hiyo na kusaidia changamoto ziweze kukabiliwa na kutimizwa kwa wakati.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...