Saturday, October 27, 2018

WAZIRI LUKUVI ALITAKA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA NHC KUWA MFANO KATIKA KUSIMAMIA NYUMBA ZAKE

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akitia saini kwenye kitabu cha wageni kwenye ofisi ya NHC mkoa wa Kilimanjaro huku Meneja wa NHC mkoa wa Kilimanjaro, Juma Kiaramba akishuhudia.
Meneja wa NHC mkoa wa Kilimanjaro, Juma Kiaramba akisoma taarifa ya utekelezaji wa NHC mkoa wa Kilimanjaro mbele ya Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akikaribishwa na wafanyakazi wa NHC mkoa wa Kilimanjaro.
wafanyakazi wa NHC mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi.

Meneja wa NHC mkoa wa Kilimanjaro, Juma Kiaramba akisoma taarifa ya utekelezaji wa NHC mkoa wa Kilimanjaro mbele ya Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akizungumza na wafanyakazi wa NHC mkoa wa Kilimanjaro.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi amelitaka shirika la nyumba la Taifa (NHC) liwe mfano katika ujenzi, kuhifadhi na kutunza nyumba zake pamoja na kujenga nyumba za gharama nafuu kwa wananchi.

Waziri Lukuvi  alisema hayo leo alipotembelea ofisi za shirika hilo katika mkoa wa Kilimanjaro akiwa katika ziara ya kushughulikia migogoro ya ardhi katika wilaya za Hai, Moshi na Same.

Alisema NHC lazima iwe mfano kwa taasisi nyingine katika ujenzi  wa nyumba bora na kuwapangisha wapangaji  kwa kipindi cha mwezi mmoja mmoja badala ya utaratibu uliozoeleka wa kupangisha watu kwa kipindi cha miezi sita au mwaka mmoja sambamba na kuepuka vishoka katika upangishaji nyumba zake.

Aidha, amelitaka shirika la NHC kuwa na mkakati maalum wa kukarabati nyumba zake na kubainisha kuwa haiwezekani shirika kubwa kama hilo kuwa na nyumba nyingi katika vitovu vya miji lakini zikiwa  zimechoka na kusisitiza kuwa asingependa kusikia shirika hilo linakuwa na nyumba mbovu.

Amelitaka shirika la nyumba la taifa kujipanga vizuri na kuhakikisha linashirikiana na halmashauri  zote nchini  kujenga nyumba kwa ajili ya watumishi  pamoja na kujitangaza katika shughuli zake kwa kuwa  lina kampuni imara ya ujenzi yenye wataalanu na inayoweza kujenga majengo mbalimbali kama vile  shule,hospitali, vituo vya afya, vituo vya afya, vyuo na majengo ya watu binafsi.

Lukuvi amelitaka shirika kuimarisha kitengo cha huduma kwa wateja na kutembelea wateja kwa lengo la kujua matatizo ya wapangaji katika nyumba zao ili kutatua kero zao.

Kwa upande wake Meneja wa NHC mkoa wa Kilimanjaro Juma Kiaramba alimueleza Lukuvi kuwa Shirika lake limekuwa na ushirikiano na halmashauri katika mkoa huo na tayari wameshaanza majadiliano kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu katika halmashauri ya Manispaa ya Moshi kujenga jumla ya nyumba ishirini na tano.

Wednesday, October 24, 2018

WAZIRI MKUU AKABIDHI CHETI CHA UDHAMINI WA MAONYESHO YA SIDO, SIMIYU KWA NHC

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa akimkabidhi cheti cha shukurani ya udhamini Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Mkoa wa Mwanza, Joseph John kwenye ufunguzi wa maonyesho wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa yaliyofanyika viwanja vya Nyakabindi, mkoani Simiyu. NHC lilidhamini kiasi cha shilingi milioni tano.
Cheti cha udhamini kilichokabidhiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa kwenye ufunguzi wa maonyesho hayo yaliyofanyika viwanja vya Nyakabindi, mkoani Simiyu.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa  akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa  akifurahia jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akipanda mti  mara baada ya kufungua Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, akijadiliana jambo na  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo, Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Mwanza, Joseph John na Afisa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa, Rhobi Wambura wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, akijadiliana jambo na Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Mwanza, Joseph John na Afisa wa Shirika la Nyumba la Taifa, Mkakaro wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, akijadiliana jambo na  Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Mwanza, Joseph John na Afisa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa, Rhobi Wambura wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.


Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo,  akijadiliana jambo na  Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Mwanza, Joseph John na Afisa wa Shirika la Nyumba la Taifa, Mkakaro wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi  Mkoani Simiyu.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameliagiza Shirika la viwanda vidogo nchini SIDO  kuweka mikakati ya kupanua wigo wa shughuli zake kwa kuanzisha vituo katika ngazi ya halmashauri za wilaya ili kuwafikia wajasiliamali wengi zaidi, kuwajengea uwezo, kuwapa miongozo bora ya namna ya kuendesha shughuli zao kwa tija na kuwaunganisha na taasisi za fedha  waweze kupata mikopo.

Waziri mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo katika ufunguzi wa maonesho ya SIDO Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu ambapo amesema umefika wakati kwa SIDO kutilia mkazo sekta ya viwanda na hivyo kuifanya jukwaa la kuwakutanisha wabunifu pia kuwapa fursa ya kuonyesha uwezo wao katika matumizi ya teknolojia rafiki na rahisi zitakazoharakisha maendeleo ya viwanda nchini.

Pia Waziri Mkuu Majaliwa amesema SIDO inapaswa kujielekeza katika kubuni mashine , mitambo na teknolojia rahisi zitakazotumika kuongeza thamani ya bidhaa na kusisitiza kuwa  kutokana na umuhimu wa sekta ya viwanda nchini katika kukuza ajira na kuongeza pato la taifa serikali itaendelea kuweka miundombinu wezeshi itakayoharakisha kasi ya ukuaji wa viwanda.

Wednesday, October 17, 2018

HAFLA YA KUMUAGA MENEJA MSTAAFU WA NHC MKOA WA KILIMANJARO


Meneja mstaafu wa NHC, Mkoa wa Kilimanjaro Shehe Salum Kombo akifurahia zawadi ya gitaa aliliopewa katika sherehe ya kumuaga rasmi iliyofanyika ijumaa iliyopita mjini Moshi.
Kaimu Meneja NHC Mkoa wa Kilimanjaro Stanley Msofe akitoa neno katika sherehe ya kuwaaga wastaafu ndh Shehe Kombo na Margareth Kimario. Watumishi hawa walistaafu utumishi mwezi June na Julai mwaka huu.
Kaimu Meneja wa NHC, Mkoa Kilimanjaro Stanely Msoffe akikabidhi zawadi ya Gitaa kwa Meneja mstaafu wa mkoa wa Kilimanjaro Shehe Salum Kombo.
Mhasibu wa mkoa Hellen Mosha akiserebuka na Meneja mstaafu Shehe Salum Kombo katika sherehe ya kuwaaga wastaafu iliyofanyika ktk ukumbi wa ofisi ya mkoa Kilimanjaro.
Kaimu Meneja wa Mkoa wa Kilimanjaro Stanely Msoffe akijiandaa kufungua shampen. Kulia kwake ni Fredrick Stephen Shoo ambae ni mume wa mstaafu Margareth Kimario na pia mtumishi wa NHC Arusha.
 Mstaafu Margareth Kimario akisindikizws na wafanyakazi wa Mkoa Kilimanjaro kwenda kupokea zawadi yake. Mama Shoo alipewa zawadi ya vyombo vya nyumbani na vitenge.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa Kilimanjaro wakishiriki katika tukio hilo.
 Baadhi ya watumishi wa Shirika la Nyumba la Taifa wakifurahia tukio la kuwaaga wastaafu. Tukio hili lilifanyika ktk ukumbi ulioko ofisi za mkoa.
Meneja mstaafu wa NHC Mkoa wa Kilimanjaro Shehe Salum Kombo akifurahia zawadi ya gitaa aliliopewa katika sherehe ya kumuaga rasmi iliyofanyika ijumaa iliyopita mjini Moshi.

Tuesday, October 02, 2018

NHC LINDI WAFANYA TAFRIJA FUPI KUMUAGA MSTAAFU MAMA ASHA MWAMBA

 Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa Lindi, Gibson Mwaigomole akimkabidhi bahasha ya zawadi kutoka kwa wafanyakazi wa Lindi, Mstaafu Mama Asha Mwamba ambaye amestaafu rasmi utumishi wa umma Septemba, 2018. Sherehe ya kumuaga Mama huyo ilifanyika mjini Lindi.
 Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa Lindi, Gibson Mwaigomole akimkabidhi bahasha ya zawadi kutoka kwa wafanyakazi wa Lindi, Mstaafu Mama Asha Mwamba ambaye amestaafu rasmi utumishi wa umma Septemba, 2018. Sherehe ya kumuaga Mama huyo ilifanyika mjini Lindi.
 Sherehe fupi ya kumuaga Mama Mwamba ikiendelea ambapo kulikuwa na viburudisho vya vyakula na vinywaji vya kutosha.
  Sherehe fupi ya kumuaga Mama Mwamba ikiendelea ambapo kulikuwa na viburudisho vya vyakula na vinywaji vya kutosha.


Monday, October 01, 2018

NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA ARDHI AFANYA ZIARA MRADI WA BUSWELU

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mathias Kabundugulu  akitembelea mradi wa nyumba za Makazi Buswelu NHC Mwanza akiongozana na Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa Mwanza Joseph John wakati Kiongozi huyo alipotembelea mradi huo katika ziara yake ya kulitembelea Shirika na kufahamu utendaji kazi unavyoendelea. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mathias Kabundugulu  akitembelea mradi wa nyumba za Makazi Buswelu NHC Mwanza.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mathias Kabundugulu  akishuhudia jambo wakati akifanya ziara kwenye mradi wa Nyumba za Makazi wa Buswelu Mwanza, kushoto kwake ni Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa Mwanza Joseph John, alipotembelea mradi huo katika ziara yake ya kulitembelea Shirika na kufahamu utendaji kazi unavyoendelea. 
Baadhi ya Nymba za mradi wa Nyumba za Makazi wa Buswelu Mwanza zinavyoonekana sasa.
 Baadhi ya Nymba za mradi wa Nyumba za Makazi wa Buswelu Mwanza zinavyoonekana sasa.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mathias Kabundugulu  akitembelea mradi wa nyumba za Makazi Buswelu NHC Mwanza.

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mathias Kabundugulu  akitembelea mradi wa nyumba za Makazi Buswelu NHC Mwanza akiongozana na Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa Mwanza Joseph John wakati Kiongozi huyo alipotembelea mradi huo katika ziara yake ya kulitembelea Shirika na kufahamu utendaji kazi unavyoendelea. 

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mathias Kabundugulu  akitembelea mradi wa nyumba za Makazi Buswelu NHC Mwanza akiongozana na Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa Mwanza Joseph John wakati Kiongozi huyo alipotembelea mradi huo katika ziara yake ya kulitembelea Shirika na kufahamu utendaji kazi unavyoendelea.