Thursday, July 17, 2014

KONGAMANO LA KUJADILI MADINI,MAFUTA NA GESI LAZINDULIWA JIJINI ARUSHA

DSC_0799Baadhi ya washiriki wa kongamano la Global Academy for Oil and Gas wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kwa kongamano hilo
DSC_0808Mtendaji wa TMAA, Giley shumika akiwa na mratibu wa kongamano hilo kutoka nchini uingereza wakielekea ndani ya ukumbi wa hotel ya Maount meru
Mahmoud Ahmad Arusha
Zaidi ya washiriki 56 wanashiriki katika Kongamano la kujadili sekta ya uziduaji na uchanjuaji wa sekta ya madini mafuta na gesi katika sekta za sheria,kanuni,sera na mikataba kwa watendaji wa sekta hiyo kutoka kwenye nchi za jumuiya ya Afrika mashariki.
Akizungumza na vyombo vya habari   mkuu wa kitengo cha madini kanda ya kaskazini(tmg) Mhandisi Gilay Shamika alisema kuwa kongamano hilo la siku mbili lilovuta wadau wa sekta ya madini kutoka nchi za Kenya Uganda na wenyeji Tanzania na kuandaliwa na taasisi ya Global Academy ya nchini Uingereza.
Shamika alisema kuwa sekta ya madini na gesi imekuwa na changamoto mbali mbali ambazo zinahitaji elimu na ufahamu wa hali ya juu kwenye Nyanja hiyo hivyo wanakutana kujadiliana kwa pamoja na wenzao kuweza kupata uelewa zaidi.
Aidha alisema kuwa wadau hao kutoka sekta za sheria,madini na fedha ndioyo wanahusika katika kongamano hilo huku wakipata uelewa ni jinsi gani watakavyoweza kuongeza kiwango cha uchangiaji wa pato la taifa kutokana sekta ya madini hususani Mafuta na Gesi.
Giley alisema kuwa sekta ya madini hususani kwenye eneo la Mafuta na gesi limekuwa na changamoto mbali mbali hivyo ni sekta muhimu kuielewa kwa mapana hivyo wao na taasisi hiyo wanajadili kuweza kuzinufaisha nchi za ukanda huu.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...