Thursday, July 24, 2014

Mbunge Namelok Sokoine, wadau watoa misaada Sekondari iliyoungua


Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Arusha(CCM) Namelok Sokoine akimkabidhi mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Irkisongo wilayani Monduli Happiness Nyange msaada wake wa shilingi millioni moja kufuatia kuungua kwa mabweni ya shule hiyo jana.
 Mjumbe wa kamati ya siasa(CCM) wilaya Monduli, Paulina Ngoyai(mama Kalaine) akikabidhi msaada wake wa mifuko mitano ya sementi kwa shule hiyo.
Mwakilishi wa kiwanda chaTanfoam cha jijini Arusha Sajid Ibrahim(kulia) akimkabidhi sehemu ya msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya shilingi millioni 3 kwa mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Irkisongo Wilayani Monduli Happness Nyange(kushoto), kufuatia mabweni ya shule hiyo kuteketea kwa moto hapo jana.Msaada huo unatokana na harambee ya papo kwa papo aliyoifanya mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akitumia simu yake ya kiganjani. Wadau kadhaa wa elimu wamejitokeza kusaidia ambapo mbunge wa Arusha Viti maalum Namelok Sokoine amechangia shilingi millioni moja.
 Mapacha wanaoishi Wakaazi wa New York Marekani Joy na Jane wakimkabidhi mkuu wa shule hiyo mama Nyange sehemu ya msaada wao wa kilo zaidi ya kumi za misumar
 Mbunge  wa Viti maalum(CCM) mkoa wa Arusha Namelok Sokoine akiangalia bweni la shule hiyo ya Irkisongo wilayani Monduli lililoteketezwa na moto jana
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Irkisongo wakibeba magodoro hayo

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...