Tuesday, July 08, 2014

RAIS DR. JAKAYA KIKWETE AFURAHISHWA NA MIRADI YA SHIRIKA LA NYUMBA (NHC)

=1w
Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na David Shambwe Kulia  Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara  wa Shirika la Nyumba (NHC) na   Felix Maagi Kaimu Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika hilo,   Wakati alipowasili katika banda la (NHC)  na kukagua, Kupata maelezo  mbalimbali ya  shughuli za miradi inayotekelezwa na shirika hilo.  Wakati alipotembelea maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa (TANTRADE) maarufu kama Sabasaba  kwenye Viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere Barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam. Yanayofikia tamati kesho jijini Dar es salaam , Katikati ni Dr. Abdallah Kigoda Waziri wa Viwanda na Biashara.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
2w 
Rais Dr. Jakaya Kikwete akimsikiliza  Bw.  David Shambwe  Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara Shirika la Nyumba (NHC) wa pili kutoka kulia ni  Elias Msese Meneja Miliki Uendeshaji Makao Mkuu na Edith Ngunwe Afisa Mawasiliano NHC.
4w
Rais Dr. Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea banda la Shirika la Nyumba NHC kwenye maonyesho ya Sabasaba Viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere Barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam wanaoshuhudia ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Dr. Abdalla Kigoda na  Nalindwa Norbert mmoja wa maofisa wa Shirika la Nyumba NHC.
5w
Baadhi ya maofisa wa Shirika la Nyumba NHC wakiwahudumia watu mbalimbali waliotembelea banda lao ili kupata maelezo mbalimbali ya shughuli zinazofanywa na shirika hilo.
6w
Baadhi ya wakuu wa vitengo wa shirika hilo na maofisa kutoka kulia ni Yahya Charahani Meneja Uhusiano wa NHC , Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara  (NHC) Bw. David Shambwe , Kaimu Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha Bw. Felix Maagi , Benedict Kilimba Mkurugenzi wa Uendeshaji Miliki na Bw. Muungano Saguya Meneja wa Huduma za Jamii (NHC). 
7w
Baadhi ya wakuu wa vitengo wa shirika hilo na maofisa kutoka kulia ni  Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara  NHC Bw. David Shambwe , Kaimu Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha  Bw. Felix Maagi, Bw. Muungano Saguya Meneja wa Huduma za Jamii (NHC) na Yahya Charahani Meneja  Uhusiano wa (NHC)  wakisubiri kuwasili kwa Mh. Rais Dr. Jakaya Kikwete katika banda lao.
3w
Rais Dr. Jakaya Kikwete akiendelea kupata maelezo kutoka kwa Bw. David Shambwe Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara Shirika la Nyumba (NHC) wakati alipotembelea banda hilo.

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...