Thursday, July 24, 2014

MAENDELEO BANK YAANZISHA HUDUMA ZA BIMA

0D6A0674
Ofisa Mtendaji Mkuu  wa Maendeleo Bank Ibrahim Mwangalaba akiongea wakati wa uzinduzi wa hudua ya Maendeleo Insurance Agency iliyoanza kutolewa na benki hiyo kwa wateja wake..
0D6A0704
Wafanyakazi wa Maendeleo Bank na wa UAP wakiwa katika picha ya Pamoja.
maendeleo
Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Ibrahim Mwangala (kulia) akipeana mkono na Nick Itunga Mkurugenzi mtendaji wa UAP Insurance Nick Itunga baada ya kuzindua huduma ya bima kupitia Maendeleo Bank
…………………………………………………………………………
Maendeleo Bank imezindua huduma ya bima ikiwa ni lengo la kuwapatia wateja huduma zote muhimu ndani ya dari moja. Pia inachangia juhudi za serikali kuboresha na kufikisha elimu na huduma za bima kwa wananchi wengi ambao hawajafikiwa. Maendeleo Bank Insurance Agency imeanzishwa ili kuunga mkono mkakati wa Serikali wa huduma za kifedha jumuishi ambazo zitahamasisha wananchi wengi watumie na wafikiwe na huduma za kifedha ikiwa ni pamoja na bima.
Katika huduma za bima, Maendeleo Bank Insurance Agency imejipanga kutoa huduma zote za bima isipokuwa za maisha. Huduma zifuatazo zinapatikana Maendeleo Bank Insurance Agency: Bima za binafsi na za biashara zikiwemo bima za moto na wizi, bima za magari ya aina zote pamoja na mitambo, bima za nyumba na vitu vya majumbani, bima za wafanyakazi, bima za maofisini, bima za biashara, bima za wakandalasi, bima za vitu vinavyosafirishwa na bima za afya.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ‘’Maendeleo Insurance Agency ‘’ Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Ndugu Ibrahim Mwangalaba alisema ‘’Kwa kuungana na kampuni ya kimataifa ya Bima yaani, UAP Insurance ni faida kubwa kwa wateja wa Maendeleo Bank Insurance Agency kwani UAP Insurance inauwezo mkubwa wa kubeba bima zote zitakazopelekwa kwao na iwapo itatokea tatizo linalohitaji kugharimia madhara ya kilichowekewa bima, basi mteja wetu hatasumbuka kwani Maendeleo Bank Insurance Agency itafuatilia mambo yote kwa muda mfupi iwezekanavyo ili mteja asisumbuke. Mwangalaba aliongeza ‘’ Bima binafsi au za biashara ni muhimu mno katika kulinda kipato na mali za wateja wetu, uanzishwaji wa huduma za bima ni kuishi kwa vitendo katika kauli mbiu yetu ya pamoja nawe katika maendeleo, kwani tunapenda kuona maendeleo ya wateja wetu yakienda mbele si kurudi nyuma kwa matukio yanayoweza kuzuilika kwa kuwa na bima’’

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...