Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Sanaa Chamwino ‘CAC’, Dr. Kedmon Mapana (katikati) akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa utambulisho wa tamasha la saba la muziki wa cigogo 2014. Kushoto kwake ni Katibu wa CAC, Sospeter Elisha Mapana na wa upande wa kulia ni Nason Mazengo, Kaimu Mkurugenzi.
Baadhi ya wageni mbalimbali wakiwa wamewasili Kijijini hapo Chamwino Ikulu, Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa kamati wa CAC wakifuatilia kwa makini mkutano huo.
Baadhi ya wageni mbalimbali wakiwa wamewasili Kijijini hapo Chamwino Ikulu, Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa kamati wa CAC wakifuatilia kwa makini mkutano huo.
Na Andrew Chale, Dodoma
SHAMRA shamra za tamasha la Muziki wa Cigogo zitatarajia kulipuka hiyo kesho Julai 25, kwenye kijiji cha Chamwino Ikulu, Mkoani hapa kwa kushuhudia vikundi zaidi ya 30, vikiwasha moto wa ngoma na muziki wa kitamaduni huku Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi akitarajiwa kulifungua rasmi.
Katika kukuza na kuendeleza sanaa nchini, tamasha hilo ambalo kwa mwaka huu ni la msimu wa Saba (7) likifahamika kama (Wagogo music festival 2014) lenye kauli mbiu ‘Utamaduni na Amani’ linatarajia kulindima kwa siku tatu, Julai 25 hadi 27, Kijijini hapo Chamwino Ikulu.
Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika mapema leo kwenye ukumbi wa Maktaba ya Mkoa wa Dodoma, Mkurugenzi mkuu wa tamasha hilo, Dk. Kedmon Mapana, wa Kituo cha Sanaa Chamwino (Chamwino Arts Center-CAC) alisema jumla ya vikundi 31 vinatarajiwa kushiriki tamasha hilo.
“Tamasha la Wagogo mwaka huu ni la saba, ambapo shamrashamra ya tamasha hilo zinatarajia kuanza majira ya saa nane mchana Mkuu wa Mkoa atakapolifungua rasmi huku tukitaraji pia kuwa na wageni wasiopungua 1000” alisema Dr. Kedmon Mapana.
Na kuongeza kuwa, kituo hicho cha CAC kimekuwa kikiandaa tamasha hilo kila mwaka huku lengo kuu likiwa ni kudumisha mila na tamaduni za Wagogo.
Aidha, alisema jumla ya wasanii 750 wanaotoka kwenye vikundi hivyo 31, wanatarajia watawasha moto wa aina yake kwa kuonyesha sanaa ya muziki wa kabila hilo.
No comments:
Post a Comment