Wednesday, July 16, 2014

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WASANII KUTOKA MAREKANI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wasanii nyota wa filamu na muziki kutoka Marekani walioko nchini kwa ziara ya kutoa mafunzo kwa wasanii wa Tanzania.Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitumia simu yake ya mkononi kuwaonesha vivutio vya kitalii wasanii nyota wa muziki na filamu wa Kimarekani walioko nchini kwa ziara ya kutoa mafunzo kwa wasanii wa Tanzania.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete…

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibadilishana mawazo na wasanii nyota wa muziki na filamu kutoka Marekani. Wasanii hao ni Terrence J. (Jenkins), mwendeshaji wa kipindi cha muziki kwenye televisheni ya E! Entertainment, mwigizaji wa filamu na mtunzi wa vitabu na Revi Shelton, Mtendaji wa Shughuli za Muziki katika Kampuni ya Outlet Media Group. Wengine ni Chaka Zulu, Mtendaji wa Shughuli za Muziki kutoka Kampuni ya Disturbing The Peace Records na Davis Banner, mwigizaji, mwanamuziki, mtunzi na msimamizi wa shughuli za muziki ambaye amepata kushinda tuzo maarufu ya Grammy.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na wasanii hao.
(PICHA NA IKULU)

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...