Wednesday, July 09, 2014

WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII AZINDUA NEMBO MPYA YA AMREF HEALTH AFRICA TANZANIA

Mkurugenzi wa Amref Health Africa Tanzania Dr. Festus Ilako (wa kwanza Kushoto) Akimkaribisha Waziri wa Afya Dr. Seleman Seif Rashid kuzindua Nembo Mpya.
Waziri wa Afya, Mwenyekiti wa bodi ya kimataifa ya Amref Health Africa Mr. Omari Issa, Dr. Festus Ilako na wafanyakazi wa Amref Health Africa Tanzania katika picha ya pamoja baada ya Uzinduzi.
wadau na wageni waalikwa katika uzinduzi huo
Picha ya pamoja ya meza kuu na wadau wa Amref Health Africa baada ya Uzinduzi.
SHIRIKA la kimataifa lisilokuwa la kiserikali la Afrika Medical and Research Foundation (Amref) limezindua rasmi jina na nembo yake mpya ambapo sasa litajulikana kama Amref Health Africa Tanzania.
Uzinduzi huo ulifanywa jijini Dar es Salaam Ijumaa ya tarehe 4/7/2014 na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid ambapo Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Africa Tanzania, Dk. Festus Ilako, alisema imebidi kubadili jina na nembo yao ili kuendana na majukumu yao ya sasa ambayo yamekuwa ni zaidi ya utafiti na utoaji wa huduma za tiba.
“Kwa sasa tunajikita pia katika uimarishaji wa mifumo ya utoaji wa huduma za afya, mafunzo, mikakati ya utoaji wa huduma/miradi ya afya ya mama na mtoto, ukimwi, kifua kikuu, malaria, huduma za madaktari bingwa na maabara.
“Mabadiliko ya jina na nembo yetu hayataathiri aina ya walengwa wetu wakuu; tutaendelea kufanya kazi kwa karibu kabisa,” alisema Dk. Ilako.
Alitoa mfano kuwa kila siku wanawake 22 wanapoteza maisha nchini wakati wa kujifungua na kwamba mpango wa Amref ni kupunguza vifo hivyo.
Waziri Seif katika hotuba yake ya uzinduzi, alisema serikali inatambua mchango mkubwa wa taasisi hiyo na kwamba wamesaidia kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, mimba za utotoni na upatikanaji wa majisafi na salama.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...