Thursday, July 24, 2014

WATOTO WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU WA KITUO CHA CHILD IN THE SUN WAPEWA MSAADA WA VIFAA VYA SHULE NA TCAA

01 (1)Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)Ally CHangwila  akimkabidhi  msaada wa Madaftari na vyakula mbalimbali  Samson Ali (12) ambaye ni mmoja wa watoto waishio katika mazingira magumu ambao hivi sasa wanalelewa katika Kituo cha Child In The Sun kilichopo Manzese Dar es Salaam kituo hicho kinachomilikiwa na Kanisa Katoliki.watoto hao wanapatikana kwa kukusanywa mitaani.
002 (1)Mwalimu  wa Kituo cha Kulea watoto waishio katika mazingira Magumu cha Child In The Sun kilichopo Manzese Dar es Salaam, Martin Modest akipokea Msaada wa Vyakula na Vifaa vya Shule yakiwemo Madaftari kutoka kwa Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Ally Changwila ,Watoto hao wanapatika kwa kukusanywa kutoka mitaani na kulelewa hapo  ambapo wanapatiwa ushauri kabla ya kuanzishwa shule.
003 (1)Watoto wanaolelewa katika kituo cha kuleya watoto waishio katika mazingira magumu cha Child In The Sun kilichopo Manzese Dar es Salaam, wakifurahia madaftari waliyokabidhiwa msaada na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania. Kushoto ni Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)Ally CHangwila   ambaye ndiye aliyekabidhi msaada huo.
004 (1)Watoto wanaoishi katika Mazingira magumu  ambao wanalelewa katika kituo cha Child In The Sun kilichopo Manzese Dar es Salaam, kikiwa chini ya Kanisa Katoliki  wakibeba mizigo ya vyakula mbalimbali na vifaa vya shule baada ya kukabidhiwa msaada na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Idd.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...