Tuesday, July 08, 2014

BALOZI WA TANZANIA NCHINI UBELIGIJI, MH. KAMALA ATEMBELEA BANDA LA MFUKO WA PENSHENI WA PPF KATIKA MAONYESHO YA SABASABA‏


Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni, Lulu Mengele (kushoto) akimkaribisha Balozi wa Tanzania Nchini Ubelgiji, Mh Dodorius Kamala (kulia) wakati alipotembelea banda la PPF kwenye maonyesho ya Sabasaba yanayomalizika hivi leo.
 Afisa Mafao wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Hellen Mollel akitoa maelezo kwa Balozi wa Tanzania Nchini Ubeligiji, Mh Kamala juu ya wanachama wanavyonufaika na mafao wakati wanapostaafu kazini, Wa kwanza Kushoto ni Meneja Uhusiano na Masoko, Lulu Mengele


Afisa Uwekezaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Anna Shayo akimpa maelekezo Balozi wa Tanzania Nchini Ubeligiji, Mh Kamala namna PPF wanavyotumia michango ya Wanachama wao katika kuwekeza katika miradi mbalimbali ambayo baadhi ya miradi hiyo tayari ishaanza kufanya kazi.


Balozi wa Tanzania Nchini Ubeligiji, Mh D.Kamala akiagana na Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele mara baad`a ya kumaliza kutembelea banda la PPF kwenye maonyesho ya Sabasaba yanayomalizika hivi leo.Picha zote na Josephat Lukaza - Lukaza Blog

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...