Kufuatia kufanya vizuri kwa Shule ya Sekondari ya St. Joseph ya Jijini Dar es Salaam ambayo inamilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo Julai 18, mwaka huu alikutana na wanafunzi wa tatu walioongoza Kitaifa na kuongoza kwa masomo na kuwapa pongezi.
Pichani juu ni Muadhama Polycarp Kardinali Pengo, akisalimiana na wanafunzi waliofanya vizuri kitaifa kutoka shule ya Sekondari ya St. Joseph Cathedral ya Dar es Salaam ambayo inamilikiwa na Kanisa Katoliki ambao ni , Joseph Ngobya wa masomo ya Sanaa na Lugha, Isaack Shayo aliyeshika namba moja kitaifa (katikati) na Prince Mwambaja (wapili kushoto) aliyeshika nafasi ya tano kitaifa masomo ya biashara.
Wazazi walimpa Kardinali zawadi kwa kuanzisha shule hiyo na kutoa elimu kwa vijana wao.
Mwalimu Mkuu,Sr. Theodora Faustine akizungumza wakati wa mkutano huo.
Wanafunzi wakiwa katika Mkutano huo wa shukrani kwa Kardinali Pengo.
Sr. Theodora Faustine ambaye ndio Mkuu wa shule ya Sekondari ya St. Joseph Cathedral akizungumza.
No comments:
Post a Comment